Hata mjadala kuhusu masuala ya uchumi pia ni wa kuingiziwa matusi enyi 'great thinkers'? What a shame! Eti na mnajiita wastaarabu? Jielimisheni bana, GDP sio 'figure' zilizotolewa angani. Huwa zinaafikiwa kupitia takwimu ambazo zina viashiria vingi sana kuhusu masuala nyeti ya ukuaji wa uchumi. Kwa mfano shughuli za kibiashara, takwimu zinazohusu fedha, mapato, export/import n.k, n.k.
Matusi ambayo huwa yanatamalaki kila mara, kwa zaidi ya miaka kumi, yamebadilisha nini kwenye uchumi au GDP ya nchi ya Kenya au hata nchi zingine ukanda huu? Hivi hatuna hata uwezo mdogo tu wa kufanya uchambuzi makinifu na mijadala ya maana, kuhusu masuala haya nyeti, kama binadamu wenye akili timamu?
Jambo ambalo huwa najiliwaza nalo sana ni kwamba mijadala ya aina hii, kwenye jukwaa hili, huwa yanafanywa kwa lugha ya kiswahili, kwa asilimia kubwa. Bure sijui tungekuwa tunazificha nyuso zetu wapi mbele ya waafrika wenzetu na wengine wengi duniani. Kisa aibu za umbumbumbu, ulofa na upumbavu mwingine wa sampuli hiyo, ambao huwa tunaundeleza wazi humu.