Geita inaenda kuchukua nafasi na ukubwa wa Mwanza Kanda ya Ziwa

Inakuaje Norway yenye watu Milioni 5 ina uchumi mkubwa kwa kila kitu karibu mara kumi zaidi na maendeleo mara mia kuliko sisi tulio na watu milioni 70 ??
(Population haiwezi kuwa kitu pekee,Bali inapaswa kuambatana na vitu vingine)

Hoja yako inachanganya mambo mawili tofauti. Population haipimwi ili kuonyesha utajiri, bali ni takwimu muhimu za kupanga maendeleo. Kulinganisha Norway na Tanzania kwa idadi ya watu pekee si sahihi, kwa sababu uchumi unategemea tija, elimu, teknolojia, utawala, uwekezaji, na matumizi ya rasilimali. Kwa hiyo, ukweli kwamba Norway ina watu wachache lakini ni tajiri hauonyeshi kuwa population haina maana; unaonyesha tu kwamba idadi ya watu peke yake haitoshi kuamua maendeleo
 
Kama issue ni takwimu tu basi hoja yako ya population kwenye huu mjadala ni haina mashiko, ni redundant tu kwa saba serikali ina takwimu za watu wa Geita pia kupitia sensa.
 
Chato Airport inafanya kazi?
 
Katoro/chato/buseresere/geita hizi zilinganishe na sengerema huko sio mwanza kwenye suala la mzunguko wa pesa.Ungekuja na takwimu hapa kwamba hiyo miji pato lake ni kiasi gani tungekuelewa lakini sio bla bla za mihemko.Mimi pia naweza kuja na bla bla nikasema dar mzunguko wa pesa ni mkubwa kuliko NYC
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…