Mohammed wa 5
JF-Expert Member
- Jun 20, 2022
- 1,215
- 3,035
HABARI Polisi mkoani Geita wamelazimika kufukua ndani ya nyumba ya mwalimu Francis Elizeus wa shule ya msingi Lubanga baada ya ndugu wa mke wake kumtuhumu kuwa amemuua mke wake Jenifer Mashimo na kumfukia ndani hali iliyopelekea ndugu hao kumtishia maisha mwalimu huyo. Mke wa Mwalimu huyo inadaiwa alitoweka tangu Machi 2020
Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Geita Safia Jongo anasema walipata taarifa ya tukio hilo wakafuatilia kibali cha mahakama ili waweze kujiridhishaa juu ya uwepo wa mwili ndani ya nyumba ya wanandoa hao ambapo hata hivyo hawajaupata
“Tarehe 3, Kibali kilipatikana na zoezi la ufukuaji ulianza kwahiyo siku ya tarehe 3, tulifukua mashimo manne ndani ya nyumba ambapo wale ndugu walikuwa wanahisi hayo maeneo kwamba ndugu yao amefukiwa lakini mpaka ikafika usiku hatukuweza kufanikiwa"
Tarehe 5 zoezi lile pia likaendelea ambapo tulifukua kila eneo ambalo tulitilia mashaka kwamba linaweza likafukiwa mwili lakini hatima yake tulikiridhisha kabisa kila eneo ambalo linastahili kufukuliwa ndani ya ile nyumba na lile eneo ndani ya ule mji tulilifukua na hakuna mwili uliopatikana kwahiyo familia na wenyewe wamethibitisha kwamba hakuna mwili uliofukiwa” alisema Jongo.
Kamanda Jongo anasema kwa sababu za kiuchunguzi na usalama imewalazimu kumshikilia mwalimu huyo ili waweze kumuepusha na watu wanaomtishia Maisha.