Geita: Mwalimu atuhumiwa kumuua mkewe

Geita: Mwalimu atuhumiwa kumuua mkewe

Matukio ya Walimu yanaendelea huko Geita.

----
Polisi mkoani Geita wamelazimika kufukua ndani ya nyumba ya mwalimu Francis Elizeus wa shule ya msingi Lubanga baada ya ndugu wa mke wake kumtuhumu kuwa amemuua mke wake Jenifer Mashimo na kumfukia ndani hali iliyopelekea ndugu hao kumtishia maisha mwalimu huyo. Mke wa Mwalimu huyo inadaiwa alitoweka tangu Machi 2020

Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Geita Safia Jongo anasema walipata taarifa ya tukio hilo wakafuatilia kibali cha mahakama ili waweze kujiridhishaa juu ya uwepo wa mwili ndani ya nyumba ya wanandoa hao ambapo hata hivyo hawajaupata

“Tarehe 3, Kibali kilipatikana na zoezi la ufukuaji ulianza kwahiyo siku ya tarehe 3, tulifukua mashimo manne ndani ya nyumba ambapo wale ndugu walikuwa wanahisi hayo maeneo kwamba ndugu yao amefukiwa lakini mpaka ikafika usiku hatukuweza kufanikiwa"

Tarehe 5 zoezi lile pia likaendelea ambapo tulifukua kila eneo ambalo tulitilia mashaka kwamba linaweza likafukiwa mwili lakini hatima yake tulikiridhisha kabisa kila eneo ambalo linastahili kufukuliwa ndani ya ile nyumba na lile eneo ndani ya ule mji tulilifukua na hakuna mwili uliopatikana kwahiyo familia na wenyewe wamethibitisha kwamba hakuna mwili uliofukiwa” alisema Jongo.

Kamanda Jongo anasema kwa sababu za kiuchunguzi na usalama imewalazimu kumshikilia mwalimu huyo ili waweze kumuepusha na watu wanaomtishia Maisha

Chanzo: EATV
 
Hao ndugu wa huyo mwanamke hawana akili au wana akili kama za huyo mwanamke wao
 
HABARI Polisi mkoani Geita wamelazimika kufukua ndani ya nyumba ya mwalimu Francis Elizeus wa shule ya msingi Lubanga baada ya ndugu wa mke wake kumtuhumu kuwa amemuua mke wake Jenifer Mashimo na kumfukia ndani hali iliyopelekea ndugu hao kumtishia maisha mwalimu huyo. Mke wa Mwalimu huyo inadaiwa alitoweka tangu Machi 2020

Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Geita Safia Jongo anasema walipata taarifa ya tukio hilo wakafuatilia kibali cha mahakama ili waweze kujiridhishaa juu ya uwepo wa mwili ndani ya nyumba ya wanandoa hao ambapo hata hivyo hawajaupata

“Tarehe 3, Kibali kilipatikana na zoezi la ufukuaji ulianza kwahiyo siku ya tarehe 3, tulifukua mashimo manne ndani ya nyumba ambapo wale ndugu walikuwa wanahisi hayo maeneo kwamba ndugu yao amefukiwa lakini mpaka ikafika usiku hatukuweza kufanikiwa"

Tarehe 5 zoezi lile pia likaendelea ambapo tulifukua kila eneo ambalo tulitilia mashaka kwamba linaweza likafukiwa mwili lakini hatima yake tulikiridhisha kabisa kila eneo ambalo linastahili kufukuliwa ndani ya ile nyumba na lile eneo ndani ya ule mji tulilifukua na hakuna mwili uliopatikana kwahiyo familia na wenyewe wamethibitisha kwamba hakuna mwili uliofukiwa” alisema Jongo.

Kamanda Jongo anasema kwa sababu za kiuchunguzi na usalama imewalazimu kumshikilia mwalimu huyo ili waweze kumuepusha na watu wanaomtishia Maisha.
Huo Mkoa una ukatili kushinda yote Tanzania
 
Hao ndugu wa huyo mwanamke hawana akili au wana akili kama za huyo mwanamke wao
Huwa nasema binadamu tunaishi Kwa kuviziana sana....hatuaminiani, tena wanandoa ni Ile wazungu wanaitwa "close enemy"
Hata mpendane vipi na mwenzio usiombe afariki ghafla usiku mmelala, au apotee kiajabu Kama hivyo....uliyebaki cha Moto utakiona.
 
Nakala imfikie mpwayungu
20230407_141530.jpg
 
Eti kidogo niulize huyo mwanamke alikuwa na **** ya dhahabu
 
Kwani wewe mwandika uzi una matatizo kwenye ubongo wako,content inasema anatuhumiwa na ufafanuzi unayolewa kuwa hakuna walicho kikuta.
Cha ajabu wewe unahitimisha kuwa mke kauwawa.
 
Ualimu wake unahusikaje kwa kupotea kwa huyo mke?!
Tuheshimu taaluma ya ualimu.

Tunataja taaluma endapo inahusika kwenye tukio...mf. taaluma ya udereva kwenye ajali ya gari.
Hebu tuwaacheni waalimu wapumue kidogo.
kweli haihusik asee, basi tuseme Mwanaume mmoja huko geita ambaye ni mwl anashikiliwa akihisiwa kumuu mke wake
 
Back
Top Bottom