Gen Z ndo kizazi bora na cha watu wenye upeo wa juu wa uelewa

Gen Z ndo kizazi bora na cha watu wenye upeo wa juu wa uelewa

Neture lazima nchi kukua na kuendelea kwa nchi lazima ipitie hiki wa nachokifanya GeZ nchi zote zilizoendelea na kustarabika lazima kuna mstari umechorwa kati ya watawala na watawaliwa. Tuliaona Arabu Spring nchi za kiarabu zilivyokutwa na mshikemshike Afrika hapa Ghadafi akaleta zarau akaliwa kichwa kipindi majirani zake wanakipata cha moto yeye alitakiwa ku step down mapema sana
 
Na ndio kizazi kinachotumika kuwapambania wengine nao wapate nafasi ya kuendesha ma V8 na kujilimbikizia mali za umma ambazo kwa sasa hawazipati
Acheni huu ujinga wa kifikiri gen z wanatumika. Incompetence na corruption katika mifumo ya kiuongozi mbona zinaonekana kwa mtu yoyote mwenye akili timamu. Dogo anasota mtaani kutaguta ajira halafu anaona mtoto wa mkuu wa usalama wa taifa anachezea dola laki 3(kibongo bongo ni takribani milion 700) tena na dole la kati anaonyeshewa. Dogo kama huyu akiandamana utasema amechochewa?

Licha ya hivyo hawa madogo wameingia mtaani na kukuta hakuna kilichobaki kwa ajiri yao. Rasilimali, ajira na njia za kiuchumi zishashikwa na vizazi vya 80's kurudi nyuma, kwaiyo kulipuka ilikua ni suala la muda tu.
 
Sio kuwa wana akili sana , Bali hawakujazwa ujamaa vichwani mwao wala hotuba za kale.
Wao wanajua kujitafutia maisha Yao zaidi
Maneno ya bla bla wameona hayawapi ugali wa kila siku
Mitandao imewafungua sana vijana wa leo na Ndio maana wanajua na kuona kila kitu

Wa zamani tulipewa elimu na kulishwa mengi sana ambayo hayajawasaidia wengi ila kuwa mfanyakazi wa mishahara mpaka ana staafu na mwisho wa siku anakufa bila kuwaendeleza wanae.

Hawa wa sasa labda watoto wao ambao wataitwa Gen Beta watakuwa na maendeleo zaidi
Sisi tu tuliozaliwa early 90's tulipandikizwa ujinga mwingi sana sipati picha wenzetu wa 70's uko. Nakumbuka wakati nipo primary around darasala 3 hivi kuna mwalimu aliniambia Nyerere ndio mtu mwenye akili zaidi kuwahi kutokea Tanzania. Kila nikikumbuka kwamba niliamini kauli ya yule mwalimu huwa nabaki kucheka tu.
 
Sisi tu tuliozaliwa early 90's tulipandikizwa ujinga mwingi sana sipati picha wenzetu wa 70's uko. Nakumbuka wakati nipo primary around darasala 3 hivi kuna mwalimu aliniambia Nyerere ndio mtu mwenye akili zaidi kuwahi kutokea Tanzania. Kila nikikumbuka kwamba niliamini kauli ya yule mwalimu huwa nabaki kucheka tu.
Ujamaa mbaya sana
Halafu walituaminisha ujinga. mwingi sana
 
Hakuna kizazi ambacho ni smart zaidi kwa asili.
Kila kizazi kina aina yake ya ujuzi na aina yake ya akili kulingana na mazingira kilicholelewa ya technology, elimu, changamoto na fursa zilizopo wakati huo)
Gen Z + Gen Alpha ni werevu zaidi katika teknolojia na ku process taarifa, information age, AI
Millennials ni smart zaidi kielimu na kijamii, wasomi wengi (most educated and socially intelligent)
Gen X ni werevu katika fikra huru na uhakiki (independent and critical thinking)
Boomers ni katika ujuzi wa vitendo (practical zaidi) , industrial age
 
Back
Top Bottom