Kwanza ulianza kulaumu kuwa sisi tulifanya nini! Hii ni hoja mfu kwani enzi zetu hakukuwa na mikataba ya hovyo kama iliyopo sasa ya bandari, madini, misitu, Ngorongoro, Loliondo, KIA nk.
Pili idadi ya wasomi enzi hizo ilikuwa ndogo kwa hiyo nguvu yao siyo kama hivi sasa. Sasa kuna vijana wasomi wengi ambao wakiungana wezi na waporaji wataogopa.
Kumbuka enzi zetu hatukuwa na tatizo la ajira kama leo na wala hatukuwa na tatizo la kazi za kuajiriwa au kujiajiri bali tulikuwa na tatizo la elimu na ujuzi wa kufanya kazi! Darasa la saba aliweza kuajiriwa serikalini na sasa ndiyo wanakula pension kitu ambacho kwa sasa ni ndoto!
Tatu ni kuwa wengi wa enzi zetu hawana tatizo la ajira wala kazi, ni wazee ama wamestaafu au wanaelekea kustaafu. Hivyo kwa kuwa tunaona hali ya maisha ilivyo ngumu na tunaona kesho yenu itakuwa ngumu zaidi tuko tayari kuwaunga mkono endapo mtakuwa wamoja kupambania maisha yenu ya sasa na kesho.
Umoja wenu ndiyo kesho yenu njema!