General Tyres Tanzania ilivyohamishiwa Kenya na kuitwa YANA tyres!

Mkuu sijui kama unayafahamu vizuri mambo ya wa Bulgaria wakati wakijenga hicho kiwanda. Walitakiwa wajenge kiwanda cha kuyeyusha chuma na kuunda vitu siyo cha kuunganisha sehemu za machine walizounda kwao. Pili container zilizokuwa zinaleta parts za mashine zilikuwa zinajazwa magunia ya Kahawa zinarudi bila hata kukaguliwa pale bandarini. Wabulgaria waliibuka na kuwa wauzaji wakubwa wa kahawa Eastern Europe. Kilichosikitisha ni pale wanasiasa walipokubali msaada usioleweka bila kutafuta ushauri wa wahandisi. Niliwahi kumtamkia Mzee Mwakawago (wakati huo nadhani akiwa Katibu Mkuu), kwamba hakitadumu maana msaada ulikuwa wa kilaghai.
Nchii Una Mambo mengi ya hivyo yaliyaowahi tendeka. Na bado hatujifunzi..tunazidi tends hovyoooo zaidi.
Wajukuu zetu watatushangaa Kama nasi tunavyomshangaa chifu Magungo
 
Kwa anaye fahamu sababu ya kuiba vinu vya kutengeneza matairi ya ubora wa hali ya juu kutoka kiwanda maarufu Nchini na Duniani kilichokuwepo Arusha juzi juzi tu cha General tyres na kuvihamishia Kenya ambapo wanavitumia kutengenezea matairi ya Yana tyres then wanakuja kutuuzia hayo matairi huku Tanzania, nini chanzo?

============================

==========================================

==================================

=====================================

Haya mawazo ni matokeo ya elimu mbovu

elimu mbovu ndiyo inasababisha tuendelee kulilia General Tyre, Elimu mbovu ndiyo inayosababisha tuamini tuliibiwa technologia general tyre.

Huu ni ujinga.

Badala ya kufikiria tuzalishe nini? tuko tunawaza urithi wetu kutoka kwa mwalimu nyerere. Haya haya mawazo ndiyo unakuta mpaka ngazi ya familia, wanalilia urithi.

General tyre ilikufa kutokana na sababu zilizokuwepo enzi hizo, yawezekana ni uendeshaji mbovu, yawezekana ni soko, yawezekana ni siasa, ni ujinga kukaa kulilia General Tyre.
 
bro umetoa comment kwa kadri ya mfanano wa jina lako.."ego" ..
 
Soma uzi wote, acha kudandia kwa mbele
Uzi nimeusoma wote, mwanzo hadi mwisho. Ila kando na porojo na chuki zako dhidi ya Kenya na wakenya. Hakuna sehemu yeyote ile, ambapo umedhibitisha madai yako kwa ushahidi wa kuridhisha. Kwamba kuna vinu, wala teknolojia ambayo iliibiwa Tanzania na kuhamishwa Kenya. Kisha ikarudi kwenye soko nchini Tanzania, kwa jina lingine.

Kwa taarifa yako Firestone ni brand ambayo ina sifa sana nchini Kenya, tangia zamani. Kama mlizembea na mkasababisha anguko la kiwanda chenu hicho usijaribu kuwalaumu Firestone/Yana Tyres kwa kujaza pengo kwenye soko. Maanake biashara ya matairi ndio shughuli yao kuu na wanafata faida, sio mapenzi wala hisia zingine, sawa tu na wanabiashara wengine kote duniani. Bidhaa zao zimekuwepo sokoni, kote ukanda huu wa Afrika Mashariki tangu zamani.

Kwa ufupi ni kwamba tafuta mchawi mwingine wa kumlaumu kwa uzembe na utepetevu wenu. Wahadae wenzako na hizo porojo zako, kwa raha zako. Lakini usichafue biashara za watu(na wakenya pia), bure tu kisa roho yako nyeusi iliyojawa na chuki. Proudly Kenyan! 🇰🇪
 
Haya mawazo ni matokeo ya elimu mbovu

elimu mbovu ndiyo inasababisha tuendelee kulilia General Tyre, Elimu mbovu ndiyo inayosababisha tuamini tuliibiwa technologia general tyre.

Huu ni ujinga.

Badala ya kufikiria tuzalishe nini? tuko tunawaza urithi wetu kutoka kwa mwalimu nyerere. Haya haya mawazo ndiyo unakuta mpaka ngazi ya familia, wanalilia urithi.

General tyre ilikufa kutokana na sababu zilizokuwepo enzi hizo, yawezekana ni uendeshaji mbovu, yawezekana ni soko, yawezekana ni siasa, ni ujinga kukaa kulilia General Tyre.
Mkuu,nimemsoma Ngongo ameeleza Kwa uelewa wa ndani kabisa akiwa km mfanyakazi wa GTEA.
Wewe unasema "yawezekana". Na kwenye "yawezekana" zako zipo zilizodondekea kwenye sababu alizotaja Ngongo .
Ngongo ametoaa muktadha wa sababu za kufa kiwanda. Na sababu alizoziainisha zinaleta mantiki Sana.
BTW. Kupewa urithi ni Jambo zuri, Sisi wakristo kwenye chuo cha Mithali 13:22A. Inatuasa "Mtu mwema huachia wanaye urithi...
Na Sisi tunalilia urithi ambao tungeachia watoto ana wajukuu zetu wa vitu tulivokua Navo ikiwemo viwanda vilivouliwa.
 
Kwenye biashara sio kila kitu utakisikia kikiekwa wazi.ila walio ndani wanapata za "ndani". Za "ndani" zimetolewa.huenda ulikuwa huzijui. Na wala sio kuchafua biashara na Kenya Kwa ujumla mkuu. Mtu akimwambia unanuka mdomo, hakuchafui, anakupa fact.
 
Inawezekana baba yako alikuwa na biashara kubwa enzi zile lakini leo hakuna kitu, watoto hamuwezi kukaa kulilia yaliyokuwa ya baba yenu.

mimi nikiwa mdogo maduka makubwa yote katika mji niliokulia yalikuwa yanamirikiwa na wahindi, wafanya biashara wachache waliokuwepo walikuwa na maringo, anaweza kufunga duka eti sasa hivi ziuzi au wateja wamekuwa wengi.

Kwa sasa mambo yamebadirika, waafrika wanamiriki maduka makubwa, mteja anabembelezwa.

zipo familia nyingi zilizokuwa na uwezo na zikimiriki maduka makubwa enzi hizo na leo zimefilisika.

maisha ndivyo yalivyo na ukiyatambua hayo hutakaa kulilia vya jana bali kuhangaika leo kutafuta vya kesho.

Kuna watu walikuwa katika familia masikini enzi tukiwa shule, leo mambo yao yamebadirika wamekuwa watu wakubwa, zipo familia watoto walikualia kwenye kupata kila kitu leo watoto ukubwani wanaishi kimasikini.

huu ndiyo mfumo wa maisha.

Changamoto kwa watu wenye elimu mbovu ni pale anavyoona kwao walikuwa na uwezo na leo wamerudi chini wanaanza tulirogwa, kuna mtu alichukua nyota yetu, na kuanza kupiga hesabu kwa nini mali walizokuwa nazo udogoni zimepotea.

Haya ndiyo manyoleta kwenye taifa kuimba general tyre, sijui urafiki, sijui nini

Mazingira ya biashara yanabadirika, na kwa mtu ambaye hajajiandaa akaendelea kutumia maarifa yaliyopitwa na wakati anapotea.

tanzania itapiga hatua kwa kutazama tuwekeze katika nini leo, tufanye nini lakini siyo kulilia viwanda vya zamani
 
Gesi ya kusini nayo n kaa la Moto kipind hiki mafuta yamepanda ges ingekuwa mkomboz kwa magari yetu na umeme pia

Lakn wapi

Sasa tunajenga bwawa la umeme miaka kumi ijayo hutaamin jins tatizo la umeme litakavyotutesa

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Kwa awamu hii tusahau hilo bwawa, kukamilika kwake labda visima vya gesi viishiwe gesi
 
Haya mawazo ni matokeo ya elimu mbovu

elimu mbovu ndiyo inasababisha tuendelee kulilia General Tyre, Elimu mbovu ndiyo inayosababisha tuamini tuliibiwa technologia general tyre.

Huu ni ujinga.

Badala ya kufikiria tuzalishe nini? tuko tunawaza urithi wetu kutoka kwa mwalimu nyerere. Haya haya mawazo ndiyo unakuta mpaka ngazi ya familia, wanalilia urithi.

General tyre ilikufa kutokana na sababu zilizokuwepo enzi hizo, yawezekana ni uendeshaji mbovu, yawezekana ni soko, yawezekana ni siasa, ni ujinga kukaa kulilia General Tyre.
Hayo utajua wewe, sisi tunataka kifufuliwe kwa sababu demand ya soko la ndani tu ni kubwa mno!
 
Uzi nimeusoma wote, mwanzo hadi mwisho. Ila kando na porojo na chuki zako dhidi ya Kenya na wakenya. Hakuna sehemu yeyote ile, ambapo umedhibitisha madai yako kwa ushahidi wa kuridhisha. Kwamba kuna vinu, wala teknolojia ambayo iliibiwa Tanzania na kuhamishwa Kenya. Kisha ikarudi kwenye soko nchini Tanzania, kwa jina lingine.

Kwa taarifa yako Firestone ni brand ambayo ina sifa sana nchini Kenya, tangia zamani. Kama mlizembea na mkasababisha anguko la kiwanda chenu hicho usijaribu kuwalaumu Firestone/Yana Tyres kwa kujaza pengo kwenye soko. Maanake biashara ya matairi ndio shughuli yao kuu na wanafata faida, sio mapenzi wala hisia zingine, sawa tu na wanabiashara wengine kote duniani. Bidhaa zao zimekuwepo sokoni, kote ukanda huu wa Afrika Mashariki tangu zamani.

Kwa ufupi ni kwamba tafuta mchawi mwingine wa kumlaumu kwa uzembe na utepetevu wenu. Wahadae wenzako na hizo porojo zako, kwa raha zako. Lakini usichafue biashara za watu(na wakenya pia), bure tu kisa roho yako nyeusi iliyojawa na chuki. Proudly Kenyan! 🇰🇪
Unaweza kutofautisha kati ya ‘madai’ na ‘swali’?
 
Hayo utajua wewe, sisi tunataka kifufuliwe kwa sababu demand ya soko la ndani tu ni kubwa mno!
Afufue nani?

Hivi viwanda vinavyomirikiwa na serikali ni uchochoro wa watu kupiga hela. Nenda katazame ripoti ya CAG kuhusu kiwanda cha viatu kilichoanzishwa moshi.

Ukitazama soko la viatu hapa nchini ni dogo? lakini kiwanda kila mwaka kinaripoti hasara. Wenzetu walishaona haya na kuamua serikali zao kujiondoa katika kufanya biashara.

Nyinyi mnaoliona soko hilo jiungeni pamoja, uzianeni shea, kakopeni mfufue mpige pesa.
 
Kufufua haimaanishi wakiendeshe wao.., kwakuwa ni mali ya serikali, wafanye wanachotakiwa kufanya ili kifufuke..
 
Kwenye biashara sio kila kitu utakisikia kikiekwa wazi.ila walio ndani wanapata za "ndani". Za "ndani" zimetolewa.huenda ulikuwa huzijui. Na wala sio kuchafua biashara na Kenya Kwa ujumla mkuu. Mtu akimwambia unanuka mdomo, hakuchafui, anakupa fact.
Jombaa nadhani uelewa wako na wangu kuhusu maana ya FACTS unatofautiana sana. Hakuna facts zozote ambazo zipo kwenye uzi huu, zinazohusiana na Yana Tyres, zaidi ya nilizozitupia humu mimi mwenyewe. Kama unabisha kwamba kiwanda cha kampuni yenyewe hakijakuwa kwenye 'operations' tangia 1969 tembea Kenya. Fika pale kwenye kiwanda chao pale Sameer Park, Mombasa Road jijini Nairobi.

Alafu historia ya Firestone/Yana Tyres ipo kwenye tovuti ya wamiliki wa kampuni hiyo, Sameer Africa. Kama hutawaani kunazo vianzo vingine vya habari na kumbukumbu, k.m. Business Daily.
 
Unaweza kutofautisha kati ya ‘madai’ na ‘swali’?
Kwamba una haki ya kutumia madai tu, kueneza chuki zako kwasababu umeyatupia humu kama maswali? Huo sio uchawi Jombaa? Watu wanatumia nguvu na rasilimali nyingi kufanikisha biashara zao bana. Alafu wewe hapo unaona sifa kutumia maneno matupu, bila ushahidi, kuwalimbikizia tuhuma zisokuwa na msingi. Badilika jombaa, hizi chuki hazitakufaidi wewe wala hazitaifaidi Tanzania.
 
Kwahiyo nimeuliza swali na nikajibiwa.
 
Kweli kabisa na kati ya hayo majibu langu lipo. Kwenye faili la juu kabisa, tena halikwepeki. Natumai unazidi kuelimika na kustaarabika.
Aliejibu nadhani umeona nimeungamisha majibu yake kama sehemu ya uzi.
 
Kwahivyo sasa unaendeleza utamaduni na kumlimbikizia lawama, huyo aliyechangia kwenye mada ambayo ni yako mwenyewe?
Acha unafik jombaa, kichwa cha mada ulikiandaa wewe mwenyewe. Alafu ukatanguliza na sentensi hii hapa"...Kwa anaye fahamu sababu ya kuiba vinu vya kutengeneza matairi ya ubora wa hali ya juu...
Kisha baada ya mimi kukupa FACTS, ambazo zipo wazi kabisa na ambazo zinaweza zikadhibitishwa, bado upo tu unaleta ubishi.

Haingii akilini kwamba mtu anaweza akashindwa kufika Ujerumani au Uturuki, kwa mfano. Ambapo asilimia kubwa ya mashine, ambazo huwa zinatumiwa kwenye viwanda vya sampuli hiyo, huwa zinatengenezwa na kuuzwa. Ili aje Tanzania kuiba hiyo 'teknolojia' ambayo unaizungumzia. Kwamba matairi ya magari yalivumbuliwa Tanzania au ndio unamaanishaje?

Jombaa, sitachoka maanake wewe mwenyewe umekiri kwamba uliandaa hizi tuhuma zako na uchafuzi huu wa bure, dhidi ya biashara za watu. Kwa msingi hafifu wa 'madai' tu, jambo ambalo halikubaliki kabisa. Huu utamaduni wa kuendeleza chuki dhidi ya Kenya na wakenya, sio sifa nzuri hata kidogo kwa jukwaa kama hili.

Hapa lazima niwahusishe Moderator huu uzi wako unakiuka maadili na sheria zote, ambazo huwa zinadumisha hadhi na heshima kwenye jukwaa hili.
 
Mi nimeuliza , na nimejibiwa; kuuliza si kosa.
 
Back
Top Bottom