General Tyre siku hizi badala ya kuzalisha tyres na bidhaa nyingine za mpira tumeigeuza sehemu ya sherehe za harusi,bonanza na nyama choma haaa haaa kweli waTanzania tumelogwa na aliyetuloga kesha kufa tumebaki kuchangisha fedha za kujenga misikiti,makanisa ......halafu tunalalamika ajira hakuna.
Tumeanzisha vyuo vikuu vingi wahitimu sijui waende wapi ?.Tumewekeza kwenye siasa katika kila kitu.
Mwezi wa tatu tulianzisha project na jamaa zangu tukahitaji watu wanne tu kwaajli ya hiyo project.Nilishangaa zilikuja barua 300 ndani ya siku tatu nikajua tatizo la ajira Tanzania ni kubwa kuliko tunavyoambiwa na wanasiasa.
Wanahabari wetu badala ya kuangalia tatizo la ajira siku hizi wapo mstari wa mbele kuandika ----- badala ya kuangalia matatizo ya watanzania kwa undani wanaangalia na kusifia ghilba za wanasiasa uchwara.
Serekali baada ya kushindwa kuyasimamia mashirika yaliyokuwa yakiwaingizia fedha nyingi kupitia kodi mbali mbali na kuyaacha yajifie kifo cha mende siku hizi imekimbilia kunyakua fedha kutoka mifuko ya hifadhi ya jamii kama NSSF,PPF...........matokeo yake wachangiaji wa hii mifuko inayokaribia kufilisika ni kutunga sheria na kanuni za kuwabana wachangiaji ambao ni wafanyakazi.Pengo la kuiza NBC ambayo ilimliza Mwl Nyerere na mashirika mengi ya umma ambayo yalikuwa yakilipa kodi bila kukwepa kama mashirika ya watu binafsi labda gasi ya kusini itaweza kuziba kiu ya wanasiasa ya kujilimbikizia mali kila wanapopata nafasi.