Hakuna siku ya furaha kama leo ambapo kwa mara ya kwanza Amiri Jeshi Mkuu wetu, Samia Suluhu amevaa magwanda ya jeshi.
Binafsi kwangu nimefurahi kumuona mama na magwanda yake. Hongera mama yetu Rais Samia.
Zipo porojo za wasiofahamu wanahoji kwa nini kavaa wakati Kikwete, Mkapa na Mwinyi hawakuvaa.
Niwakumbushe tu hawa kama hawakuvaa waliamua kwani mwanajeshi mkuu ni Rais yaani Amiri Jeshi Mkuu.
Rais Nyerere akivaa kijeshi mara kadhaa na alienda hata Kagera kukagua maandalizi ya kumpiga Idi Amin. Tena Nyerere alivaa hadi magwanda ya mgambo.
Hivyo hiyo siyo hoja nimeigusa tu kwa sababu wapingaji wa kila kitu humu wameifanya iwe hoja.
Sasa nije kwenye hoja yangu, hasa iliyonisikitisha kutokea eneo la jeshi.
Utaratibu wa jeshi lolote ni kwamba unafuata seniority, yaani ukubwa. Mkubwa anapigiwa saluti na mdogo, "Jambo Afande" na mkubwa anaitikia "Jambo".
Mkiwa kikundi cha wanajeshi, au askari yoyote mnatembea, mbele yenu anakuja mkubwa kuwazidi, basi aliye senior kati yenu anakaa kulia kisha anapiga saluti kwa niaba yenu wote mlio kushoto kwake.
Hii ndiyo sababu askari hukaa mkubwa (senior) kulia mwa wote na mdogo (junior) anakaa kushoto.
Hata kama hujaishi na askari basi angalia gwaride lao uwanjani wakifika penye mkubwa kikosi kinaamriwa "Heshima Kulia toa" halafu walioko kulia kabisa wanatoa saluti jukwaani.
Hii ni mojawapo ya maana ya senior kukaa kulia ndiyo maana kuna "Heshima Kulia toa" kwa sababu kulia ndiko aliko mkubwa.
Hakuna "Heshima Kushoto" kwa sababu kushoto kuna mdogo (junior).
Ndiyo sababu hata salute ni ya mkono wa kulia siyo ya mkono wa kushoto.
Hata hafla nyingi nchini ukitizama utaona Mabeyo amekaa kulia mwa Simon Siro.
Ndivyo majeshi yalivyo tangu jeshi la Roman Empire hadi leo.
Sasa leo Rais Samia katembelea wanajeshi wake. Kisha akasimama kushoto mwa Mabeyo ambaye ni junior kwake.
Kilichotakiwa ni mama kusimama kulia mwa Mabeyo ili Mabeyo awe kushoto kwake.
Bahati mbaya sana hakuna aliyelidokeza hili matokeo yake waandishi wamepiga picha na tumeipata mitandaoni.
Hili ni kosa na tunasihi lisirudiwe.
Basi hata likitokea ikibidi basi wapiga picha wawe makini kutosambaza picha kama hizi japo ni ukweli.
View attachment 2011963