General Venance Mabeyo kakosea kusimama kulia kwa Rais Samia. Mwanajeshi senior anakaa kulia kwa junior

Tanzania ndo nchi pekee kila mmoja anajua,wewe umejuaje kuwa wamekosea ?uliza ujibiwe
 
Kinachofanya uwe Senior/Junior nafikiri ni mafunzo.
Labda tuseme, Amiri jeshi mkuu hana mafunzo hayo kwasababu hio CDF ataendelea kukaa Kulia kama senior (Kwenye eneo lake la kazi ukizingatia wamevaa kombati) wakivua gwanda tukatumia itifaki atakua junior πŸ€—
au nasema uwongo ndugu zangu?
 
waongo banah wanaweza ht kumkosoa samaki jinsi anavyoogelea, kuna mambo yanaoneka na wazi km mama jinsi mama alivyotokelezea unaacha unaleta habari za kumfundisha mabeyo mambo ambayo kabobea kuliko ww
Hiyo ni kanuni ya Jeshi dogo. Kama hujui piga kimya!
 
Rais anapokuwa amevaa kijeshi namna hii, kwenye mabega kunakuwa na alama za aina gani zinazoonyesha cheo chake kama Amiri jeshi Mkuu? Kwa mfano, CDF yeye ana mkasi na nyota nne, Rais yeye anakuwa na nini mabegani?
 
Kwa vitambi labda polisi Mkuu ila sometime ni maumbile tu ya mtu nimeshuhudia mara nyingi wanajeshi wana vitambi ila wanaonekana kabisa hawa watu wapo vizuri sana,,, Kuna siku nlimuona captain wa jeshi ana kitambi ila jinsi alivyo mwepesi ni atari anafanya kila kitu kwa wepesi mbaka watu wakashangaa na kitambi chake.
 
Okay but nikukosoe kidogo kwanza hakuna amri ya "heshima kulia toa"ila ni heshimaaaaaaa...... Kulia pia iyo ni kwenye pared lakini sio kwamba hakuna heshima kishoto ila heshima kushoto ipo ni pale sinior anapotembeza kikundi cha askari na kiongozi akawa yupo upande wa kushoto huwezi kutoa amri kwamba heshima kulia wakati kiongozi yupo kushoto laazima useme heshimaaaaaaa... Kushoto na ukitoa iyo amri ni kwamba wewe senior wa kikundi utasalute lakini askari wengine watakata macho kushoto au kulia inategemeana na alipo kiongozi


Wewe unapitisha askari kwa mwendo wa halaka popote pale kambini gafra afande ocd au CO akatokea na akawa yupo kushoto kwa kikundi cha askari basi wewe senior unaeongoza bogi la askari utasema heshimaaaaaaa... Kushoto basi wewe utasalute na kusema jambo afande na askari wengine watakata macho kushoto isipokua mstari wa right mark ndio hawata kata macho kushoto maana wao ndio wanalinyoosha bogi kwenye kutembea.Asante
 
Ni kweli kwa hizo emergency cases. Katika mazingira ya Venance Mabeyo hakukuwa na emergency, alitakiwa kuwa right marker, jambo ambali hunipingi.


 
Rais anapokuwa amevaa kijeshi namna hii, kwenye mabega kunakuwa na alama za aina gani zinazoonyesha cheo chake kama Amiri jeshi Mkuu? Kwa mfano, CDF yeye ana mkasi na nyota nne, Rais yeye anakuwa na nini mabegani?
Cheo chake kipo kwenye kofia yake pale mkuu pameandikwa C in C maana yake Commander in Chief chini ya ile alama ya ngao ya rais. Hawezi kuwa na cheo chochote mabegani kwa sababu yeye siyo commissioned officer bali ni commander in chief tu.
 
Magwanda sketi ndio mpango. Hapo bado kuna u"ME" ndani yake
 
Samia akivaa nguo za kijeshi Uchumi wa nchi unapaa? Mataga mna tabu sana
 
Hapo uliposema Mabeyo kukaa kulia Kwa Sirro nadhani unahitaji mjadala mwingine uanze ndani ya mjadala huu
 
Sorry mkuu, unasema picha ipo sahihi, lakini mbona maelezo yako tena yanaikosoa picha hiyo hiyo!
Msamehe tu amehoji na kukosoa jambo asilokuwa nalo uhakika.

Generali Mabeyo pamoja na kuwa Mkuu wa Majeshi, kimsingi ni Mlinzi Mkuu (body guard) wa Rais. Naamini mleta mada atakuwa amenielewa kuhusu jinsi walinzi wa Rais wanavyojipanga wakiwa pamoja naye
 
Wasiojua utaratibu wa kijeshi kufuata seniority watabisha na wengi wameshafanya hivyo. Mleta mada upo sahihi na hii ni kwa mujibu wa majeshi yote duniani senior anakaa kulia over.
 
Halafu pia si huwa kuna kiongozi wa ITIFAKI na sijui kwanini hajaliona na kulizingatia hili !!
Nahisi hii pic ilichukuliwa haraka haraka hata hivyo afande Mabeyo alipaswa amwelekeze CiC position yake.
Labda alishikwa na uoga wa gafra hahaha. Lawama nawapa watu wa kitengo cha habari JW; Ina maana hawakuliona mpaka waisambaze hii picha?!
 
Hizi story za kufikirika hizi πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚
 
Asante mkuu,
Kazi yetu ni kusema ukweli bila kujali mshabiki anabisha au kukubali.

Nimeambiwa kwamba hwta kanisani askofu hukaa kulia kwa mspadri.

Wasiojua utaratibu wa kijeshi kufuata seniority watabisha na wengi wameshafanya hivyo. Mleta mada upo sahihi na hii ni kwa mujibu wa majeshi yote duniani senior anakaa kulia over.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…