Hii ni link ya audio video ya GeZ wakijadiliana namna ya kulianzisha tena pengine kabla hata 25/12 na kuendelea....
View: https://youtu.be/oLG8oqkpG5c?si=8NzhnwgIimcza0Es
Kinachopangwa na kujadiliwa ni maandamano ya kuanzia 25/12.
Lakini kilichonishitua zaidi mimi si maandamano yenyewe. Ni kile kitachoambatana na maandamano hayo, kwamba moja ya watu wanaowalenga kuwachomea moto nyumba zao, mali zao au biashara zao ni viongozi wa serikali za mitaa na vijiji na wajumbe wao...!!
Loooh!!.. Hili limenitisha na kuniogopesha sana. Chondechonde GenZ, hawa ni raia na walala hoi wenzetu tu huku vijijini na mitaani. Hata kama hushiriki kwenye uhalifu na uovu wa kiuchaguzi ni kwa sbb ya njaa tu. Hawajui lolote linaloendelea huko serikali ktk ngazi za juu. Hawa hutumwa tu kama mbwa...
Kwanini tuwaonee hawa wasio na lolote, wasiojua chochote wakati wanaokula nchi na kuiharibu wako huko Dodoma na DSM? Ni Viongozi wakubwa walio ktk vyombo vya mamlaka ya maamuzi kama Samia, Mwigulu Nchemba, mawaziri, wakuu wa mikoa, mapolisi wa ngazi zote? Hawa ndio wa kudili nao....
Chondechonde vijana wetu wa GenZ, tunawaunga mkono kabisa kwenye harakati hizi za kuikomboa nchi yetu ya Tanganyika toka mikononi mwa ukoloni wa Kizanzibari na waarabu wa Oman na Dubai...
Lakini acheni na mpango wa kwenda kuonea watu hawa. Ni ndugu zetu hawa. Hawana hatia yoyote...
WITO KWA SAMIA NA SERIKALI YAKO
Tafadhali acheni kiburi maana kiburi hutangulia na baadae huja mauti...
Kubalini tu na kirini makosa yenu ya kuua watu na kuharibu uchaguzi. Kubalini kuwa hamkupigiwa kura na wananchi 29/10 na mpo ktk nafasi hizo isivyo halali kimaadili na hata kisheria....
Mkifanya hivi, chukueni hatua sahihi na stahiki. Leteni taifa pamoja kwa kurudi pale tulipoangukia na kuanza upya. Acheni kujidanganya na vijitume vyenu vya kufichia uovu wa makosa yenu. HIYO HAITAWASAIDIA kujiponya..!
Vijana wako serous. Maneno huumba na kuwa kitu halisi. Wanasemasema sasa hivi, lakini kwa hakika kabisa tunaweza kuanza kushuhudia ubaya mbaya zaidi kuliko tulivyowahi kuona huko nyuma...!