Mnagangaika na mazao ya zile division 4 za 28 zilizopewa GO AHEAD kwenye utawala wa JK, wengine wapo kwenye uchambuzi kwasababu ya ugumu wa maisha.
Na hata mnaowaona wanabadili gia na kuanzisha nyuzi kila saa, mara VAR haikutumika, mara Simba anacheza mchezo mchafu, mara Mayele angekuwemo angefunga, oooh uwanja haukujaa ni UFUKARA na kukosa kazi za kufanya.
Kama Simba Sc imefikia uwezo wa kuhujumu team kubwa zenye uchumi mkubwa na majina Africa kama Ahly , Kizer, Orlando, AsVita, Saoura na nyinginezo, basi anastahili pongezi. Maana hatuwezi kukaa kila siku tunalalamika Simba Sc inahujumiwa kama jinsi ambavyo Yanga wamekuwa wakili kila msimu. HII NI ISHARA YA UKUBWA.
NB: Kuna ubaya gani kufanya hujuma kwenye mashindano makubwa yenye postive return, ikiwa kuna team inafanya hujuma kwa viteam vidogo vya ndani kushindania kombe la mbuzi???