Jamani eee, anakula kwa nafasi yake. Tutapiga keleleee lakini hatusaidii jamii hii ya Tz. Huyu anakula anakojua, je hawa wanaokula kodi zetu kwa Katiba viza mbona hatuwakemei?? Ale tu, alindwe na chopa, azungukwe na magari, lakini zangu hali simpelekei miye. Wanaopeleka wapeleke. Huwez niambia nimpelekee wakati miye nimeenda kwa miguu naye akaja kifahari hivyo.
Jiulize, hiyo gharama ya ulinzi mkuu hivyo ingesaidia makanisa yake mangapi tunayo yaona huku kwetu, yapo kwenye turubali zilizochoka kuliko, si awanunulie mabati?? Nakuambia waumini wake wamelogwa, wameshikwa fahamu zao na akili zao zote. Hao polisi sawa, wanachotaka posho tuuu lakini siwezi enda hapo nikadanganywe mchana peupe.