PostGE2025 George: Nilipigwa risasi Oktoba 29, 2025 nikapoteza mguu

PostGE2025 George: Nilipigwa risasi Oktoba 29, 2025 nikapoteza mguu

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Kasi ya ufyatuaji risasi ya LMG (Light Machine Gun) inatofautiana lakini kwa kawaida inafyatua risasi 6 hadi 25 kwa sekunde, au raundi 360 hadi 1500+ kwa dakika (RPM).

Kwanini utumie silaha kama hizi kama hujakusudia kuua maelfu kwa maelfu ya wananchi?
Walikusudia kuuwa watu wengi kadiri iwezekanavyo lengo kuwatisha wengine wasitoke kuandamana.
Hii haiwezi kuachwa ipite hivihivi.
Wanategemea watu watasahau na kuendelea na maisha kama zamani bila wao kuwajibishwa.
Lazima watu waliofanya uhalifu huu wa binadamu wawajibishwe.
Jela au .....
Mali zao zikamatwe kufidia wahanga.
 
"Nilikataa kukatwa mguu, lakini madaktari waliniambia nimechelewa kupata matibabu." Huo ni ushuhuda wa kusikitisha wa George Chipeta (24), fundi wa umeme wa magari mkazi wa Banana, mkoani Dar es Salaam aliyetoa maelezo mbele ya Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Oktoba 29, 2025.

George, ambaye sasa analazimika kuishi bila mguu wake wa kulia, ameiambia Tume jana, Januari 19, 2026, kuwa alipigwa risasi na askari polisi mchana wa tarehe 29 Oktoba akiwa katika shughuli zake za kutafuta vipuri (spare parts) maeneo ya Vingunguti.

Siku ya tukio, George alikuwa ametoka ofisini kwake Banana kuelekea Tabata kununua booster ya gari. Wakati akirudi kwa kutumia pikipiki yake kupitia njia ya Vingunguti, alikutana na kundi la watu wapatao 50 hadi 70 wakikimbizana na gari la polisi (Defender). Amesema alipatwa na hofu akageuza pikipiki ili aondoke. Wakati anageuza, ndipo akapigwa risasi ya paja kutokea nyuma iliyokata mishipa ya damu.
Samia atosha tukutane2030 Samia2030 MamaSamia2025
 
Nimesoma comments kwenye social media zingine, Wa Tanganyika hatutakaa tumove on kwenye hili suala.
Bahati mbaya sana watekelezaji wa mauaji huwa wana kale kamsemo hata walikomtishia Melo kuwa "tutakupoteza watu watalia siku chache hadi mwezi halafu watasahau".

Bahati mbaya hili la October 29 liligusa hata watu tofauti tofauti na kila mmoja ana mbinu yake ya kudeal nalo.

Kuna walioamua kukubali, kuna waliosema hata iwe ni kwa wajukuu wa watekelezaji kisasi lazima kilipwe, kuna wengine wanatengeneza kisasi tunavyoongea na hawatojali chochote.

Ukiunganisha hapa hayo makundi ndio utajua kwanini yule muuaji wa siku 100 bado kajificha kwenye kiota.

Hapo ndio unakuja ule msemo wa kimombo "The guilty are always afraid"

Maana anajua alichokifanya na anajua matokeo yake.

Njia mbili tu ndio zitapooza hili suala , uwajibikaji na kisasi.

Ya kwanza imefeli maana mwenyewe alisema nguvu iliyotumika ni sawa na watu hao amewaongeza posho.

Hii ya pili ndio itakua tiba ya hili jambo muda utasema.
 
Damu ni mbaya, wanaweza kutafutwa na kumalizwa kimya, kimya, kuuwa ushahidi.
....hakuna namna mmuaji ghafla anawapenda aliotaka kuwaua...BIG NO!
Hii tume uchwara ya Chande ilitakiwa kuuliza maswali kama haya kwanini silaha kama hizi zilitumika, nani alitoa ruhusa, kuandaa hii mipango na utekelezaji
Hamna tume hapo bro, Kanyanga tu hapo!
 
Hivi hawa wanaoenda kwenye hiyo tume matarajio yao ni nini haswa?? Au wanahisi watalipwa 😅
Wanaweweseka labda watapata kitu chochote cha kuwasukuma mbele (unfortunately hakuna kutokana na asili ya uongozi tulio nao maana haya waliyoyafanya waliyadhamiria).

Kama huyu dogo miezi minne nyuma alikuwa na miguu yote leo mmoja hana,inasikitisha sana though ni jambo la kushukuru anapumua maana wapo waliopotea kabisa.
 
"Nilikataa kukatwa mguu, lakini madaktari waliniambia nimechelewa kupata matibabu." Huo ni ushuhuda wa kusikitisha wa George Chipeta (24), fundi wa umeme wa magari mkazi wa Banana, mkoani Dar es Salaam aliyetoa maelezo mbele ya Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Oktoba 29, 2025.

George, ambaye sasa analazimika kuishi bila mguu wake wa kulia, ameiambia Tume jana, Januari 19, 2026, kuwa alipigwa risasi na askari polisi mchana wa tarehe 29 Oktoba akiwa katika shughuli zake za kutafuta vipuri (spare parts) maeneo ya Vingunguti.

Siku ya tukio, George alikuwa ametoka ofisini kwake Banana kuelekea Tabata kununua booster ya gari. Wakati akirudi kwa kutumia pikipiki yake kupitia njia ya Vingunguti, alikutana na kundi la watu wapatao 50 hadi 70 wakikimbizana na gari la polisi (Defender). Amesema alipatwa na hofu akageuza pikipiki ili aondoke. Wakati anageuza, ndipo akapigwa risasi ya paja kutokea nyuma iliyokata mishipa ya damu.
Sasa sijui tusemeje!
.

Yeye sasa anasema "watatumia ndimi kuwaponya" waathirika na waTanzania wote kwa ujumla.

Yeye yupo madarakani, kishatimiza malengo yake.

Wewe ulikuwa ukihangaikia maisha yako, utimize malengo yako.

Lakini malengo ya Samia yalikuwa ni muhimu zaidi kuliko yako; kwa hiyo ikabidi umzawadie yeye haya yaliyokupata wewe.

Sasa, pengine kwa kuwa umejitokeza mbele na kushiriki katika zoezi la kumsafisha Samia, pengine utaambulia chochote cha ziada kuliko kuponyeshwa kwa ndimi pekee. Lakini mguu ndiyo hivyo tena umekwisha ondoka; na hata muelekeo wa mipango yako inaweza kuwa isitimie tena kama ulivyoipanga huko mwanzo.

Narudia tena kukupa pole.
Pole sana kijana. Wewe ni mmoja wa kielelezo cha zawadi ya Kumbakiza madarakani Samia Suluhu Hassan
 
Walikusudia kuuwa watu wengi kadiri iwezekanavyo lengo kuwatisha wengine wasitoke kuandamana.
Hii haiwezi kuachwa ipite hivihivi.
Wanategemea watu watasahau na kuendelea na maisha kama zamani bila wao kuwajibishwa.
Lazima watu waliofanya uhalifu huu wa binadamu wawajibishwe.
Jela au .....
Mali zao zikamatwe kufidia wahanga.
Watu hawatasahau na hawatasamehe....
 
Vijana wengine ni kama Matahira, nchi kwenye tension, askari wanawadhibiti wahuni wanaotaka kuichoma moto nchi wewe unakatiza mitaani then unakuja kulia lia kijinga.
Anayekutwa kwenye battle field ni adui . Unaua then baadaye itajulikana.
Bila polisi kutumia nguvu kubwa ile October 29 nchi ingekuwa majivu sasa hivi na wajinga kama nyie ndio mngefurahi
 
Wangemuua mama yako na mume wako waliopumzika nyumbani, ndiyo ungeshika adabu.

Kisa tu vijihela vya Tanganyika unavyopewa kutukana wasiohusika na ushetani wenu.

Na watoto waliobebwa mgongoni waliwakosea nini mkawauwa.

Huna uzalenda, wala uchungu.
 
Maria Sarungi, Mangekimambi na nyie nyumbu mnaojificha nyuma ya keyboard na kuchochea vurugu sahivi nyie ni wazima ila watoto wa watu wamekua vilema

Tokeni na nyie mkaandamane nyumbu nyie.
 
Back
Top Bottom