George Stinney, mtoto wa kwanza kuwahi kuhukumiwa kifo na kunyongwa nchini Marekani

George Stinney, mtoto wa kwanza kuwahi kuhukumiwa kifo na kunyongwa nchini Marekani

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
18,037
Reaction score
33,681
Video hii hapo chini inaonyesha namna mtoto mweusi mwenye miaka 14 kwa jina George Stinney alivyo nyongwa.

Mtoto huyu alinyongwa mnamo mwaka 1944 huko South Carolina akituhumiwa kuwaua watoto wawili wasichana wa kizungu, Betty June Binnicker (11) na Marry Emma Thames (8). Mtoto huyu alitiwa hatiani kwa ushahidi wa kimazingira tu na hakukuwa na uthibitisho wa uhakika kwamba yeye ndio alihusika na mauaji hayo. Angekuwa mtoto wa kizungu pengine angepewa adhabu tofauti kabisa na aliyopewa mtoto huyo mweusi.

Unaweza kutazama mwenyewe hapo chini.


george-stinny-jr.jpg


----

Anaitwa George Junius Stinney, Jr. alizaliwa Oktoba 21, 1929 na kufariki kwa kunyongwa Juni 16, 1944 akiwa na umri wa miaka 14 tuu. Ni mtoto, muamerika mweusi maarufu sana duniani kutokana na simulizi yake ya kusikitisha ya hukumu ya uonevu juu ya kosa lisilo lake.

Anajulikana zaidi kwa tukio la kupewa hukumu isiyo yake, hukumu ya kifo ya kuonewa ya kuhusika na vifo vya mabinti wawili weupe wa umri wa miaka 7 na 11 mwaka 1944 huko Alcolu, South Carolina alikokua akiishi na familia yake.

March 23, 1944 watoto wa kizungu Betty Binnicker (11) na Mary Thames (7) walipatikana wamefariki karibu na kiwanda cha mafuta mjini Alcolu, South Carolina, baada ya kutorudi nyumbani mapema.

Polisi wakamkamata George aliyekuwa akiishi karibu na kumlazimisha akiri kosa, maelezo yote 'feki' ya kukiri kosa yaliandikwa katika notebook, ndani ya dakika 10 tuu za kusomwa kesi hiyo mahakamani George alihukumiwa kifo huku akinyimwa kujieleza chochote.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa March 24 siku moja tuu baada ya watoto hao kukutwa wamefariki ni kwamba walibondwa vichwani na chuma kizito ambacho kwa vyovyote kwa umri wa George asingeweza kabisa kukinyanyua chuma hicho, lakini kikafichwa.

Toka anakamatwa hadi ananyongwa ilikuwa ni ndani ya miezi mitatu kasoro, kwa muda huo wote wazazi wake waliruhusiwa kumuona George mara moja tuu, na hawakuwahi mruhusu ajitetee kwa lolote.

Historia imemtaja George kuwa ndiye muamerika wa kwanza mwenye umri mdogo kuwahi kuhukumiwa kifo na kunyongwa katika historia ya taifa hilo kubwa duniani, mwaka 2014 mahakama ilikiri kuwa mtoto huyo alinyongwa kwa kuonewa.

Mapitio ya kesi yake yalianza tangu mwaka 2004 ambapo kwa miaka 10 yote uchunguzi ulikuwa ukifanywa na hatimaye mwaka 2014 ikabainika kuwa mtoto George hakua na kosa, alipewa hukumu ya kifo kwa kuonewa ikiwa ni miaka 70 imepita.

Mwaka 1944 mji wa south Carolina, Marekani.

Kijana mdogo aitwaye George stinnery alihukumiwa kifo akiwa na umri mdogo wa miaka 14.

Siku 82 kabla ya hukumu, George alikuwa akitembea na rafiki yake alikutana na mabinti wawili mmoja aitwaye Betty benicka mwenye umri wa miaka 11 na mwingine aitwaye immathams mwenye umri wa miaka 7 walikuwa wakiendesha baiskeli kuelekea shambani kuchuma maua.

Kesho yake ya tr 23-3-1944 walionekana polisi wakivamia nyumba ya kijani George stinnery walidai kua mabinti hao wawili wameuwawa na walitupwa kwenye bwawa nje kidogo na nyumba anayoishi George pamoja na wazazi wake na nduguze wanne
polisi waliwakamata George pamoja na kaka yake kesho yake polisi walitoa taarifa nyingine kua George alikili kwa polisi kua ametekeleza mauaji hayo kwamba aliwapiga mabinti hao na kipisi kidogo cha chuma cha reli.

Mabinti hao walifanyiwa vipimo kubaini kama walifanyiwa ukatili, lakini ripoti ilionyesha kwamba hakuna ukatili wowote walio fanyiwa zaidi ya kupigwa vibaya tu na kipande hicho cha chuma.

Hatimaye George alipandishwa kizimbani kwa kosa la mauaji ya kukusudia lakini pia polisi hawakuruhusu George apate wakili wa kumtetea wala wazazi wake hawakuruhusiwa kumuona George gerezani kwa siku zote 81 alizo kaa gerezani george alijitetea mahakama kua hakupewa hata chakula kwa siku zote.

Askari wa kizungu walisema watampa chakula endapo akikili kua aliua lasivyo atakufa kwa njaa akiwa gerezani.

Lakini jaji filips alikataa utetezi wowote juu ya George na mbaya zaidi mahakama ilijaa wazungu pasi mwafrika hata mmoja.

George alisimama katika hukumu yeye pekee, lakini pia jaji fillips alisema George atampa wakili mmoja ambaye jaji alimuchagua akiwa na yeye ni mzungu.

Wakili huyo hakumutetea george kwa chochote yeye alisema George kakili kufanya mauaji kwa mabinti hao wawili.

Mnamo tarehe 6-6-1944 jaji fillips alitamka hukumu ya kifo kwa kijana George. alisema kifo hicho kitakuwa cha kupigwa na shot na umeme mkali mpaka kufa.

Kijana mdogo huyo George alisimama na kukumbatia kitabu cha dini akisubiri kufanyiwa kama hukumu ilivyo tolewa.
Hukumu ilitekelezwa George alifungwa kwenye kiti cha umeme akifungwa mikono na miguu yake ili wamuue kwa umeme.
Lakini George aliambiwa kusema neno lolote la mwisho, lakini george alitikisa kichwa tu wala hakusema chochote huku machakozi yakimtoka huku akitazama kitabu chake cha dini.

Hatimaye volt nyingi za umeme zikanunua uhai wake.

Baba ake George alifukuzwa kazi na alipo kua akiishi.

Lakini haki ya George ilitafutwa kwa miaka mingi sana hatimaye baada ya miaka mingi ilisemekana George hakuwa na kosa lolote.
Mahakama ilijilisha upya na kugundua George hakuwa na kosa lakini george alipata hukumu kisa yeye ni mweusi.

Na hii ilipelekea watu wengi weusi kusoma sheria ili kupingana na hukumu ya mzungu.

Hiyo ndiyo ilikuwa kesi ya George stinnery.
 
Last edited by a moderator:
Inasikitisha sana.

Kisha wao ndio wanajifanya wanajua haki za Binadamu.

Kwa kuwa ni miaka mingi imepita tumuachie Mungu tu.


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Hizi movies za aina hii zimeshamiri miaka ya hivi karibuni.

Kuna mwandishi mmoja mweusi alihoji do black people have something else positive to turn into movies badala ya hizi stories?


Nyani Ngabu, Kiranga
 
Last edited by a moderator:
Nimeitoa Wikipedia

On October 25, 2013, Steve McKenzie, Ray Chandler and Matt Burgess of Coffey, Chandler & McKenzie, P.A., filed a Motion for New Trial Pursuant to South Carolina Rule of Criminal Procedure 29(b).


South Carolina lawyers Steve McKenzie, Ray Chandler and Matt Burgess are supporting George Frierson in an attempt to obtain a posthumous pardon, if not a complete judicial exoneration, for Stinney. Frierson is a historian from Alcolu who came across the case in 2004 while doing historical research. McKenzie in an interview in 2011 said he has no doubt this case was an injustice.

He said that the lack of preserved evidence made clearing Stinney's name difficult, but he hoped that the affidavits of three new witnesses, one of which could provide an alibi, would be enough to re-open the case.

If we can get the case re-opened, we can go to the judge and say, ‘There wasn't any reason to convict this child. There was no evidence to present to the jury. There was no transcript. This case needs to be re-opened. This is an injustice that needs to be righted.' I'm pretty optimistic that if we can get the witnesses we need to come forward, we will be successful in court. We hopefully have a witness that's going to say - that's non-family, non-relative witness - who is going to be able to tie all this in and say that they were basically an alibi witness. They were there with Mr. Stinney and this did not occur.
-Steve​

George Frierson stated in interviews that "...there has been a person that has been named as being the culprit, who is now deceased. And it was said by the family that there was a deathbed confession." Frierson said that the rumored culprit came from a well-known, prominent white family. A member, or members of that family, had served on the initial coroner's inquest jury which had recommended that Stinney be prosecuted
 
Hicho ni kisa cha ukweli kaka, not just a movie

Sijasema kuwa siyo kisa cha ukweli.

Point yangu ni kuna visa vingine vinavyohusiana na weusi vimefanyiwa movie miaka ya hivi karibuni and some people wanauliza kinachotafutwa ni nini?

Sympathy kutoka kwa weupe, kuwaonyesha what things they did to black people in the past au nini hasa?

Au ni weusi kufanikiwa kutawala kwenye sekta ya filamu?

I am interesting to know the intention or motive behind ya hivi visa kufanyiwa movies.
 
Sijasema kuwa siyo kisa cha ukweli.

Point yangu ni kuna visa vingine vinavyohusiana na weusi vimefanyiwa movie miaka ya hivi karibuni and some people wanauliza kinachotafutwa ni nini?

Sympathy kutoka kwa weupe, kuwaonyesha what things the did to black people in the past au nini hasa?

Au ni weusi kufanikiwa kutawala kwenye sekta ya filamu?

I am interesting to know the intention or motive behind ya hivi visa kufanyiwa movies.

Ok nimekusoma kaka...
 
Duuh! Inasikitisha sana, na kinacho sikitisha zaidi ni kwamba ntill now bado hawamwoni mwafrika kama kiumbe anayesitahiri kuthaminiwa kama wao.
 
Masikini yarabi weee. Mzungu na Myahudi, wapi na wapi? Kama hujui kitu, kwa nini kukiandika?

Mzungu - Christian, Myahudi- Judaism, hizi dini hazipendani kabisa. Soma zaidi uwe na ufahamu.

Subiri waje mayahudi weusi hapa uone povu litawatoka kutetea mzungu
 
Back
Top Bottom