George Stinney, mtoto wa kwanza kuwahi kuhukumiwa kifo na kunyongwa nchini Marekani

George Stinney, mtoto wa kwanza kuwahi kuhukumiwa kifo na kunyongwa nchini Marekani

Naamini yupo mahali salama huko juu
Hii video yake niliitazama kwa mara ya kwanza na ya mwisho mwaka 2018 na sikutaka na sitaiangalia tena, iliniliza hii video na nilikuwa napata tabu sana usiku, hakika wazungu hawawapendi kabisa watu weusi na wanatamani wawamalize ila mipango ya Mungu tu.
 
Kweli mkuu inauma sana
 
Full story kuhusu George stinnery Jr ipo hapa
 
Video hii hapo chini inaonyesha namna mtoto mweusi mwenye miaka 14 kwa jina George Stinney alivyo nyongwa.

Mtoto huyu alinyongwa mnamo mwaka 1944 huko South Carolina akituhumiwa kuwaua watoto wawili wasichana wa kizungu, Betty June Binnicker (11) na Marry Emma Thames (8). Mtoto huyu alitiwa hatiani kwa ushahidi wa kimazingira tu na hakukuwa na uthibitisho wa uhakika kwamba yeye ndio alihusika na mauaji hayo. Angekuwa mtoto wa kizungu pengine angepewa adhabu tofauti kabisa na aliyopewa mtoto huyo mweusi.

Unaweza kutazama mwenyewe hapo chini.

----

Huyu hakunyongwa bali aliuawa kwa kiti cha umeme. Ukisemwa alinyongwa lazima kitanzi cha kamba kihusike. Kwahiyo kwa Kiswahili fasaha kauli yako ina walakini.
 
Hivi kuna utaratibu gani wa familia yake waliobaki kulipwa fidia.Kwa vyovyote ni vigumu baba na mama yake kuwepo lakini huenda kuna dada,wajombo ukoo
 
Back
Top Bottom