Gerald Hando hata Wewe?

Gerald Hando hata Wewe?

Na hichi ndicho wengi hawafahamu, wanadhani tunapinga uwekezaji au tunampinga DPW. Uwekezaji ni mzuri, na hata DPW anaweza asiwe mbaya lakini tatizo tunampa bandari kwa makubaliano yepi?
Mazwazwa hayaelewi
 
Kila Nikiwaza kuandika huu uzi nilikuwa najishauri sana, mwishowe nimeona tu bora niandike ili dukuduku langu liishe.

Hivi karibuni watangazaji wakituo cha Wasafi FM Gerald Handom Maulid Kitenge na Zembwela walienda mpaka ziliko ofisi za DP Word kwenda kufanya mahojiano na wafanyakazi mbalimbali wa kampuni hiyo juu ya utendaji wao katika masuala mbalimbali ya bandari.

Kwangu ziara hiyo haikua na maana sana sababu kinachopingwa na watanzania wengi sio utendaji wa hao jamaa, hakuna anaepinga kua jamaa wako vizuri. Ila kinachopingwa ni aina ya mkataba. Sasa katika watangazaji hawa ningeweza kuelewa kama Maulid Kitenge na Zembwela wakifanya ushabiki wa haya masuala sababu upeo wao wa kuchambua mambo kama haya sio mkubwa kama Gerald.

Maulid Kitenge hua anaropokaga tu anadhani akiongea kwa sauti na ushabiki mkubwa ndio watu wataelewa. Sio mjenga hoja kwenye issues nyeti za msingi. Zembwela anaweza kua anajua kujenga hoja lakin mara nyingi huonekana kwenye vipindi ambavyo sio serious sana hivyo uwezo wake unaweza ukawa unafichwa na hilo.

Lakin Gerald Hando wewe toka ukiwa Clouds FM msimamo wako ulikua ni wa kutetea wanyonge. Wewe ulikua hutetereki kuongea ukweli. Ulikua huogopi kabisa na kipindi hicho uko clouds ulikua hot kweli kaka. Kipindi chako cha Power Breakfast kilikua hot sana kwenye ile segment ambayo ulikua ukizungumzia mambo mbalimbali yanayoihusu jamii. Umejadili mengi sana na kwa weledi sana kwenye hicho kipindi cha PB. Nadhan hata leo hii kama bado ungekua pale ungepinga hili.

Hata ulipoingia EFM bado ulikua hujaacha kuongelea mambo mbalimbali yanayohusu jamii. Nakumbuka ulisimamishwa hata EFM sababu ulikua ukitetea juu ya nchi kukopa kulikopitiliza. EFM yatangaza kumchukulia hatua Hando, yadai maoni yake kuhusu Serikali kukopa si msimamo wa taasisi.

- Hando aungana na Ndugai kupinga Serikali inavyokopa kopa ovyo

Sasa Gerald Hando wa sasa umekuaje? NIni kimekubadilisha msimamo? Ni wewe kweli unaungana na Mtu roporopo kama Maulid Kitenge kutetea kitu ambacho unajua sio sahihi? Najua mtakua mmelipwa ili mtetee ulaji lakini roho yako kweli haikusuti kwa usaliti unaoufanya? Au kuna mahali umebanwa kifedha ukaona ufate msemo wa "mtumikie kafiri upate utajiri"??

Ukweli sijaamini na sintoamini kama kweli eti wewe Gerald Hando unaamini kua ule mkataba wa DP World na Serikali hauna dosari yoyote ile,
Unamshangaa Gerald Hando kwa hili, kwa nini usiwashangae Rais wa nchi pamoja na Waziri Makame Mbarawa kwa "ujasiri mkubwa" wa kutuuza Watanzania wenzao kwa Waarabu wa Dubai??? Unatakiwa kuwa na roho ngumu ya Shetani Jini Makata kufanya usaliti mkubwa wa aina hii.
 
Kitenge sio mtu wa kawaidah before wamasai wa serengeti kutolewa yeye ndio alikuwa wa kwanza kwenda serengeti na kurecod kipindi na kwenye ishu ya bandari kaenda mbka Dubai uyu jamaa sio mtu wa kawaidah
 
Hujaelewa hata. Na pengine hujasoma andiko langu lote. Kweli ukitaka kumficha mbongo neno litie kwenye maandishi.

1) Serikali hailaumiwi kwa kuweka mwekezaji. Hata kabla ya DPW walikuwepo TICTS kwenye makontena hivyo kwa DPW kuwekeza sio issue.

2) DPW halaumiwi kwamba ni mbaya. Amewekeza sehemu mbalimbali tu Kwa mafanikio makubwa. Na hata akija hapa tuna imani tutapiga hatua.

3) Shida ni kua tunakaa nae Kwa muda Gani?
Na kipindi hicho tuko nae ye atapata nini na sie tutapata nini
Tukiona haturidhishi tunaweza kumtoa?
Atatuletea mitambo, workers, technology au nini hasa?
Na siku akiamua yeye kuondoka (manake sie hatuwezi kumtoa labda) ataacha nini alivyokuja navyo na alivyovikuta?
Haya ndio maswali yanatakiwa yajibiwe
Acha kutupigia mikelele yako hapa,ungekuwa na guts hizo ungeenda kupiga mikelele kwenye mikataba ya madini huko kwanza almasi na dhahabu zimetengenezewa mpaka viwanja vya ndege....we kubali maisha ya kuishi kwa chaneli ya shemeji hapo bandarini yashafika mwisho wengi tu mtarudi kwenye uhalisia wenu.
Nilikuwa namchukia mama samia kipindi anaziba masikio kwenye kelele za tozo na miamala ila sasa nampenda mnooo anavoziba masikio kwenye hili la dp world.
 
Acha kutupigia mikelele yako hapa,ungekuwa na guts hizo ungeenda kupiga mikelele kwenye mikataba ya madini huko kwanza almasi na dhahabu zimetengenezewa mpaka viwanja vya ndege....we kubali maisha ya kuishi kwa chaneli ya shemeji hapo bandarini yashafika mwisho wengi tu mtarudi kwenye uhalisia wenu.
Nilikuwa namchukia mama samia kipindi anaziba masikio kwenye kelele za tozo na miamala ila sasa nampenda mnooo anavoziba masikio kwenye hili la dp world.
[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Back
Top Bottom