Gerald Hando: Mbowe aachie ngazi, amekaa sana CHADEMA

Mbowe yuko kibiashara zaidi. Usidanganyike kamwe kudhani kuwa ana uchungu na wananchi. Yeye anatengeneza mabilioni kwa kuwatumia nyinyi.

Mwaka 2015 alikunja Tzs 10 Bilioni kwa kumpokea Lowasa na kumpa nafasi ya kugombea uRais kupitia CDM.

Mwaka 2021 alipotoka Ukonga rumande alipita Ikulu kubeba mzigo wake. Na kama unabisha nitakuletea picha ya hekalu lake alilojenga huko Machame kwa fedha hizo
Huko CCM nani hayupo kimasilahi? Watu wanafikia hatua ya kuuza bandari, mbuga za wanyama, mikaba ya hovyo kwenye madini, viwanja vya ndege na ufasadi mwingine mwingi, unatuletea propaganda za Mbowe kupokea bill. 10 toka kwa Lowassa. Sijuhi ni lini watza tutaanza kujielewa
 
Unalinganisha nyanya na kuku! Hivi unafikiri uongozi kwenye chama cha upinzani ni sawa na kuwa kiongozi wa CCM?

Uongozi CCM ni ulaji lakini uongozi chama cha upinzani kama CHADEMA, ni kujitoa sadaka kwaajili ya wengine.

Katika hao wote uliowataja, tutajie japo mmoja ambaye aliwahi kubambikiziwa kesi au kulala mahabusu kama wanavyofanyiŵa viongozi wa upinzani.
Bams, nakuelewa sana hisipokuwa unaelimisha watu wasio elewa. Sijuhi ni kweli hawaelewi au wamepofushwa na siasa. Ni wangapi wanaweza kujitoa mhanga kama Lissu na Mbowe kwa ajili ya wengi. Alafu wanaohumia Mbowe kuendelea kuwa m/kiti wa Chadema sanasana ni CCM pamoja na ACT-Wazalendo.
 
Huyu hando ndonani? Amefanyia Nini nchi? Hii haja yake mbona mbaya inachafua hali yahewa!!?
 
Gerald Hando akiwa katika kipindi cha Good Morning cha Wasafi FM leo Machi 7, 2024 ametoa hoja ya kumtaka Mwenyekiti wa CHADEMA kuachia ngazi ya Uenyekiti wa chama hicho kwa kile alichodai amekaa sana, tazama video hapo juu.

Hoja hii inakuja siku chache baada ya kumshuhudia Zitto Kabwe akiachia nafasi ya Uongozi kwenye chama chake Cha ACT Wazalendo.

Upi mtazamo wako kuhusu hoja hii ya Hando?
Mmmh !
 
Wahenga walisemaga Pilipili iko shamba wewe inakuwasha nini. ??!

Masuala ya Chadema yanayohusu chama chao yatashughulikiwa na vikao vya wajumbe wao wa Chama !!

Inaonekana Mbowe anatisha I 😅😅🙏
 
Huko CCM nani hayupo kimasilahi? Watu wanafikia hatua ya kuuza bandari, mbuga za wanyama, mikaba ya hovyo kwenye madini, viwanja vya ndege na ufasadi mwingine mwingi, unatuletea propaganda za Mbowe kupokea bill. 10 toka kwa Lowassa. Sijuhi ni lini watza tutaanza kujielewa
Nionyeshe ushahidi wa mbuga ya wanyama iliyouzwa?
 
Gerald Hando akiwa katika kipindi cha Good Morning cha Wasafi FM leo Machi 7, 2024 ametoa hoja ya kumtaka Mwenyekiti wa CHADEMA kuachia ngazi ya Uenyekiti wa chama hicho kwa kile alichodai amekaa sana, tazama video hapo juu.

Hoja hii inakuja siku chache baada ya kumshuhudia Zitto Kabwe akiachia nafasi ya Uongozi kwenye chama chake Cha ACT Wazalendo.

Upi mtazamo wako kuhusu hoja hii ya Hando?
Lipumba & Cheyo hawamo huyu kazidisha unafiki.
 
Mtu anajiita mende chooni ana akili ya kunyambua utimamu wa siasa za hila za chama cha mapinduzi na mapandikizi yake kweli?????
 
Gerald Hando akiwa katika kipindi cha Good Morning cha Wasafi FM leo Machi 7, 2024 ametoa hoja ya kumtaka Mwenyekiti wa CHADEMA kuachia ngazi ya Uenyekiti wa chama hicho kwa kile alichodai amekaa sana, tazama video hapo juu.

Hoja hii inakuja siku chache baada ya kumshuhudia Zitto Kabwe akiachia nafasi ya Uongozi kwenye chama chake Cha ACT Wazalendo.

Upi mtazamo wako kuhusu hoja hii ya Hando?

Ajabu sana wanachama wala hawana nongwa ila yeye ndo kawashwa.
 
Wadau UZI MMEUSOMA sasa tujadili.
Narudia tena KWANINI UENYEKITI wa FREEMAN MBOWE unajadiliwa sana tena sana na Wafuasi wa CCM na ACT badala ya WANACHADEMA wenyewe?
Je MBOWE kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA CCM na ACT wanadhurika nini?
Je CCM na ACT ina kwama wapi Iwapo MBOWE ataendelea kuwa MWENYEKITI wa CHADEMA?
Mbona CHADEMA hakuna sehemu yoyote Wamejadili kuondoka Kwa MWENYEKITI wa CCM na Wa ACT?
 
Tuwe nao makini hao. Hawachelewi kumdhuru
 
Back
Top Bottom