"Mbowe aachie ngazi amekaa sana Chadema"
Nimeitazama hiyo kauli nimeiona imekaa kidikteta, na sio hiyo kauli ya Hando pekee, wote wanaomtaka Mbowe aachie ngazi nao wamekaa kidikteta hurudia kauli hiyo hiyo wakijidai kutaka demokrasia ifuatwe, hii demokrasia yao ni ya ajabu sana.
Hawa viumbe wanajiona wao ndio wapo juu ya maamuzi ya wengine, hawajui demokrasia inasema wengi wape wachache wasikilizwe, sasa kama wengi wameamua kumpa Mbowe, hawa viumbe wengine wachache kwanini wanateseka?!
Halafu wanaposhangaza zaidi, wanamtaka Mbowe afuate mfano wa Zitto, ni kama vile wanataka kulazimisha Zitto aondoke na Mbowe, sijui wanataka iwe hivyo kwa lengo gani..
Hawajui hata huyo Zitto wanaemuona ameondoka uongozini ACT, anaenda kuwa "mshauri mkuu wa chama" chake kulingana na Katiba yao, hawajui huyu ni sawa na ametoka kwa mlango wa mbele, lakini anarudi ndani kwa mlango wa nyuma, sijui huu ujinga ndio wanataka Mbowe nae aufuate?!.
Sent from my SM-G900H using
JamiiForums mobile app