Geranimo E.K.I.A: Kutoka Makao Makuu ya CIA Langley, Oparesheni Ya Kukamatwa Osama Bin Laden

Inamaana Yericko hapendi kuona wengine wakiandika?
 
Senetor john McCain anasema Khalid sheikh yassin alitoa information ya uongo kuhusu makazi ya Osama baada ya kufanyiwa waterbodies Mara 180 akaamua kujisemea tu ili aondokane na Yale mateso lkn information zote alizotoa hazikuwa sahihi ,Khalid alisema Abu Ahmed kuwaitii alihamia Peshawar na alioa huko jambo ambalo siyo kweli ,uhusiano wa Kuwaiti na Osama haukutokana na enhance interrogative
 
Sina tatizo na wewe kabisa mkuu, wala sijapungukiwa na kitu chochote wewe kutoniheshimu kwakuwa sikupata chochote wewe uliponiheshimu....na wala sikujua heshima yako kwangu...

Hoja ni wewe kusema nime "iba" makala "yako" inayohusu DB Cooper,


Mimi nikakupa blogu niliyoandika makala hiyo tangu 2015 na kumtaja mwandishi/msimulizi Mr Jeff Harison na zaidi nikaweka video kabisa katika blog ile... Siku ile nilidhani umeghafilika tu ulipolalamika na kunitusi kwamba nimeiba kwako...

Lakini leo umeleta nyingine kwamtindo uleule na ukanishambulia, ndipo nikaamua kuwasaidia wasomaji hapa kwamba wapi unakoiba hizi hadithi... Na zaidi ninawapa na video kabisa...

Stori ya lep hii hapa.....

Mohammedal-Qahtani au Gerenimo huyo hapo na simulizi yake neno kwa neno...

 

Hii video hiyo simulizi ya neno kwa neno iko wapi ? Nilichoona kwenye video hii ya dakika tatu na sekunde 11 ni mwanamke anaelezea hali ya jamaa kama kupoteza kumbukumbu nk

Kama nimesoma hii makala ya The Bold vizuri hakuna sehemu amesema jamaa alikua na tatizo la kupoteza kumbukumbu hoja yako ya neno kwa neno mpaka hapa imeshapoteza mantiki ,


Halafu ni kitu gani hasa mnachobishania ? Jamaa katafsiri hiyo documentary sijui ya Martin au ya DoD ila yeye kaileta kwa kiswahili shida ni nini hasa ?


Video yako hii haina uhusiano wowote na mada ya The bold


NB Gerenimo ilikua code ya Mohamedal au Osama Bin Laden ?
 
Hukupata chochote kivipi mkuu?? Kama hakukuheshimu unadhani angenunua hicho kitabu chako??
 
Jamaa ana kipaji kizuri sana cha kusimulia.. Wewe mbona inakuuma sana?? Hata kama amekopi mahali ila anatutendea haki sisi tunaosoma makala zake..

Wewe ulitaka jamaa apate inside infos kwani yeye anafanya huko CIA??
 
Mkuu, kwa mujbu wa maelezo ya majirani waliokuwa wanaishi mtaa huo, wanasema kwamba umeme ulikatika mji mzima siku hiyo ya tukio na mawasiliano ya simu nayo yalikata (kuna taarifa za uhakika kuwa CIA walihusika katika uzimaji huo) kwa hiyo hata raia wangetaka kutoa taarifa ingekuwa ni mtihani..

Pia, jeshi la Pakistan wanapata msaada wa kimafunzo na fedha kutoka jeshi la marekani hivyo wamarekani wanawajua udhaifu wao nje ndani.. Kwa mfano ndege za kivita za Pakistan aina ya F-16 haziwezi kufanya mashambulizi mpaka wapate 'clearance' kutoka jeshi la marekani!!

Nadhani sababu hizi zilichangia kufanya oparesheni kuwa ya mafanikio pasipo mushkeli kutoka kwa jeshi na vyombo vya ulinzi vya Pakistan!!
 
Jamaa ana kipaji kizuri sana cha kusimulia.. Wewe mbona inakuuma sana?? Hata kama amekopi mahali ila anatutendea haki sisi tunaosoma makala zake..

Wewe ulitaka jamaa apate inside infos kwani yeye anafanya huko CIA??
Nadhani hujaelewa shida ya The Bold na mimi..

Tatizo ni moja tu, yeye anasema mimi niliiba makala "yake", mimi nimempiga kwamba sikuiba makala yako bali nimeichukua kwa Youtube FBI files za Martine, nikamletea na video hiyo... Nikamwambia wewe ndio unaweza kuwa unaiba kwakuwa unasema " zako" wakati ni za Martine wa Shirika la Ujasusi la FBI.
 

Mkuu kuhusu tukio la 9/11 nadhani kwa suala la uwezo wa wapiganaji wa All Qaeda kutekeleza tukio lile sina shaka kabisa uwezo huo walikuwa nao. Kwa mfano Mohammed Atta alijiunga mpaka na Chuo cha urubani ili afahamu namna ya kuiendeshe ndege.

Pia hii nadharia kuwa wamarekani walijilipua wenyewe huwa nashindwa kuamini nadharia hiyo kwa sababu moja rahisi sana. Sioni sababu ya msingi ya wao kufanya hivyo! Wengi wanasema walijilipua hivyo ili wapate sababu ya kuvamia nchi za kiarabu hasa Iraq na Afghanistan!! But was it worth it??? Yani waingie hasara ya mabilioni ya madola ili wapate excuse ya kuingia uarabuni, hata kama walikuwa wanataka mafuta, lakini was it really worth it??? Yani hasara yote ile, jumlisha hasara ya human capital???
Hapana aisee, nachelea kuamini walijilipua.

Kuhusu kwanini alikuwa na ulinzi Mdogo, hiyo ni mbinu ya kiusalama. Unapokuwa na ulinzi mzito unaattract attention pia uwezekano wa taarifa kuvuja kupitia watu ulionao unakuwa mkubwa

Na kuhusu hili la kwanini hawajauonyesha mwili au Picha za bin laden huwa najiuliza kwanini waonyeshe??? Walikuwa wanahitaji kujiridhisha wao kuwa waliyemuua ndiye mwenyewe, hawana kiu ya kushow-off kwa ulimwengu.
Actually nahisi hawataki hata watu wamuone mwili wake au hata Picha!! Kwanza kuna raha gani kuonyesha Picha za binadamu aliyepasuliwa kichwa kwa risasi na matundu ya risasi kifuani??? Haki za binadamu si wangepata sababu ya kuchachamaa kuwa wanadhalilisha utu wa binadamu???

Kwa mfano; hata ile nyumba yake baada ya kuuawa serikali ya Pakistan waliibomoa haraka sana ili kuepuka watu wenye msimamo mkali wasije kuifanya sehemu ya 'Hija'. Kwahiyo wakabomoa na kujenga michezo ya watoto.
 
Dah mkuu mimi ndio maana nimeona nikae kimya tu! Maana ameweka zaidi ya video tatu tofauti alafu kila moja anasema ndiyo hiyo imetafsiriwa 'neno kwa neno'.. Ukiifungua video si kweli.!

Nimeona nikae kimya tu!
 
All in all sisi tumefurahi Mzee bold.Naomba uni julishe pindi unapotupia Uzi Mpya...nime print nimehifadhi. Safi sana.

Mimi ni shabiki wako na 1
 
All in all sisi tumefurahi Mzee bold.Naomba uni julishe pindi unapotupia Uzi Mpya...nime print nimehifadhi. Safi sana.

Mimi ni shabiki wako na 1
Nashukuru sana mkuu!!
Bila shaka Mkuu, nikiweka uzi mpya ntakujulisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…