Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Baada ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere kusema alibaini upungufu katika mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Mpira wa Arusha, ambapo ulikadiriwa kugharimu Tsh. Bilioni 187 lakini mkataba ukasainiwa kwa Tsh. Bilioni 338 katika ripoti ya ofisi yake ya Mwaka 2024/2025, Machi 30, 2026 hatimaye Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema "Ongezeka au kupungua kwa gharama za miradi ni utaratibu wa kawaida"
Ripoti ya CAG kuhusu Uwanja: CAG: Mradi wa ujenzi wa Uwanja Arusha ulikadiriwa bilioni 187, mkataba ukasainiwa bilioni 338
Maoni ya Mdau;
Ripoti ya CAG kuhusu Uwanja: CAG: Mradi wa ujenzi wa Uwanja Arusha ulikadiriwa bilioni 187, mkataba ukasainiwa bilioni 338
Maoni ya Mdau;
Uwanja wa Prince Moulay Abdellah uliopo Morocco wenye kuchukua idadi ya Mashabiki 69500 umeigharimu serikali ya Morocco kiasi cha Usd M 75 ambazo ni sawa na Tsh Bilioni 183
Tulioshuhudia ule uwanja wakati wa Afcon ulikuwa ni uwanja ambao ulitumika siku ya Ufunguzi wa Michuano ya Afcon kati ya Mwenyeji Morocco na Comoro!
Ule uwanja standard ya dunia,na bahati nzuri siku wanacheza Morocco na Comoro mvua ilikuwa ikinyesha lakini hakukuwa na tone la maji lilionekana uwanjani!,Ni moja ya kiwanja ambacho kitatumika pia kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka 2030!
Leo haya Majambazi yanajenga Banda la Kufuga nguruwe lenye uwezo wa kubeba nguruwe elfu 30 tu yanakuja kutuambia gharama ni Bilioni 330 yaani ni mara mbili ya gharama zilizotumika kwenye uwanja bora kabisa duniani kwa sasa uwanja wa Prince Moulay Abdellah!
Mbaya zaidi,Yamepiga pesa zote hizo na bado hilo banda la kufugia nguruwe halijakamilika,Ni juzi tu hapa yalikuwa yanaomba msaada china ya kukamilishwa kwa banda hilo,Maana yake ni kwamba,Pesa yamekula na uwanja haujakamilika!
Ni mtu Mjinga na asiyekuwa na akili timamu tu ambaye anaweza kuambiwa hilo banda ya nguruwe lenye kubeba nguruwe elfu 30 tu linaigharimu serikali Zaidi ya Bilioni 300,Ni tahira pekee ndiye anaweza kuamini huu ujinga!
