Gerson Msigwa: Uwanja Mpya wa Mpira Utakojengwa Arusha Utaitwa Samia Suluhu Hassan Stadium

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687

My Take
Naunga mkono hoja ila prefix ya Dr iondolewe ndio jina litapendeza zaidi.

Pili Mtu apewe maua yake mapema kabla hajafa sio mtu amefariki kama Lowassa ndio mnaanza kujisemesha ooh sijui alijenga nini tutunze historia nk.

Kazi iendelee πŸ‘‡πŸ‘‡


---
Uwanja huo unaosubiriwa kwa hamu kujengwa Arusha utapewa jina la Rais wa sasa Samia Suluhu Hassan endapo tu atakubali pendekezo hilo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Gerson Msigwa, alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana.

β€œKama Wizara, tunapanga kuupa jina la Uwanja wa Samia Suluhu Hassan baada ya kukamilika kwake endapo atakubali pendekezo hilo.

"Utakuwa uwanja wa kisasa wenye uwezo wa kuchukua watu 30,000 na utakuwa miongoni mwa viwanja vya kuandaa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027," anasema.

Aidha, Msigwa anafichua kuwa kazi za ukarabati katika Viwanja vya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam zimepangwa kukamilika Agosti 24 mwaka huu.

"Viti vyote 60,000 ndani ya uwanja vitabadilishwa na vipya na niamini, kazi ya kuinua itakapokamilika, ukumbi utaonekana tofauti kabisa," anasema.

Anaongeza kuwa zaidi ya 31bn/- zimetengwa kwa ajili ya ukarabati wa Uwanja wa Benjamin Mkapa.
 
Kwani hana mwanae? Wampe huyo.
 
Chema chajiuza kibaya chajitembeza/chajitangaza.

Benjamin Mkapa wakati akiwa hai alikataa kata kata kuita Uwanja wa Taifa aliojenga chini ya utawala wake kwa jina lake, badala yake uliitwa tu Uwanja wa Taifa.
 
Chema chajiuza kibaya chajitangaza.

Benjamin Mkapa wakati akiwa hai alikataa kata kata kuita Uwanja wa Taifa aliojenga chini ya utawala wake kwa jina lake, badala yake uliitwa tu Uwanja wa Taifa.
Saizi unaitwaje? Akijenga Benjamin ni sawa ila akijenga Samia sio sawa si ndio? 😁😁😁😁😁😁😁🀣🀣🀣🀣🀣
 
Saizi unaitwaje? Akijenga Benjamin ni sawa ila akijenga Samia sio sawa si ndio? 😁😁😁😁😁😁😁🀣🀣🀣🀣🀣
Umebatizwa kwa jina lake kwa kulazimisha baada ya yeye B. W. Mkapa kufariki dunia, lakini yeye mwenyewe kwa kinywa chake alikataa kabisa wakati akiwa hai.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…