Gerson Msigwa: Waandishi wa habari kama kuna kasoro andikeni Serikali itafanyia kazi

Gerson Msigwa: Waandishi wa habari kama kuna kasoro andikeni Serikali itafanyia kazi

Dr PL

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2024
Posts
688
Reaction score
1,039
Akijibu maswali ya waandishi wa habari mbali mambo mengine bwana Msigwa aliwaambia waandishi hao kuwa kama kuna kasoro waandike na serikali itafanyia kazi.

Mojawapo ya kasoro kubwa ambayo ipo na vyombo vya habari vya Tanzania haviandiki, havisemei au hata kufanya uchunguzi (documentary) ni suala la utekaji na kupotezwa kwa watu.

Kwa hiyo kutokana na ruhusa ya serikali kupitia Msigwa:

Ninategemea kuona waandishi hao wakiandika kwenye vyombo vyao malalamiko ya wananchi hasa kuhusu suala la utekaji wa watu unaoendelea nchini mwetu.

Ninategemea kuona vipindi vya redio vikiendesha vipindi vya kujadili kuhusu utekaji, wawahoji wananchi ili serikali isikie mtazamo au mawazo yao kuhusu suala hili.

Magazeti yaandike kuhusu utekaji na jinsi inavyoathiri nchi, jinsi inavyochochea chuki ya wananchi kwa serikali, jinsi inavyoumiza familia na watu wote.


View: https://youtu.be/OrixoV5UXeU?si=2j_eD7IVcG1PdkT6

Rejea link hiyo hapo juu kusikiliza maswali na majibu ya bwana Gerson Msigwa.
 
Back
Top Bottom