Gesi asili: Is it "day light robbery?" Watanzania tunaibiwa mchana kweupe!

Kwenye madini ndio tumeona sasa, hili la gesi ninalolizungumza leo, litakuja kubainishwa na tume rais wa 2025!.
Hongera sana rais wetu, Dr. John Pombe Magufuli, inapokuja kwenye suala la maslahi ya taifa, amethibitisha pasi shaka kuwa hana mchezo wala mswalie Mtume!.
Paskali
 
Nikisikia kuhusu gas yaani moyoo wangu unavunjika kabisa, najua haitatusaidia na itavunwa sana...yaani napatwa na ubaridi moyoni halafu mafanikio nayaona kwa mbali sana...tutabakia mifupa tu hapa kwenye gas
Twarudi pale pale, tuisome mikataba kimakini, sisi ni wavivu au hatuna uzalendo wa kwenye hili, au labda zile clauses zinatupa shida, na wale wazungu sababu ni wazoefu wa haya mambo basi wana take advantage hapo hapo.

Mikataba jamani mikataba jamani, isomwe hata mara milioni, maana ukidondoka saini ni ntolee, au labda wanasheria wetu wa haya mambo ndiyo yale ya vyeti feki?!
 
Mkuu Jebs, TPDC ina wanasheria, Ofisi ya mwanasheria Mkuu ina wanasheria, tatizo ni mikataba yote ya PSA imekuwa drafted kwao, na yote itaonyesha sheria zinazotumika ni za JMT lakini arbitration ni ICC London na uamuzi wa ICC ni final na conclusive. Ile tozo ya Dowans wabunge wetu waliojiapiza kuwa hatulipi, kiukweli tumelipa kimya kimya!,ingekuwa China ,kuna watu wangenyongwa! .

Jambo la ajabu kabisa baada ya kuumizwa kwenye madini, bado hatuamki na kwenye gesi asili, tunakuja kupigwa na kuumizwa.

Paskali
 
Sasa hawa wanasheria wetu hawajabobea kuwa challenge hawa mabeberu kuwa this is not fair?! Au ndiyo yale yale ya kulainishana halafu hela za wanasheria wetu zinatumbukizwa Jersey? Yazidi kuuma ndugu zetu waliosomeshwa na serikali wanavyolitumikia taifa aise..
 
Mkuu pascal,

Nadhani sasa ni wakati muafaka kwa raisi wetu kuelewa kuwa sio mawazo/mapendekezo yote yanayotolewa na watu kuyaona kuwa ni wapinzani wake.Mfano hili la kuipitia mikataba upya ni muhimu sana tena sana na yamesemwa sana bungeni ila kwa kuwa watu wanaendekeza UCHAMA wakaona sio muhimu.Nna uhakika huko kwenye Gesi na maliasili ndo kuna uvundo wa kufa mtu
 
Sheria mpya ya serikali kuhodhi 16% stake kwenye extractive industry ndio ukombozi wa kweli wa kuibiwa madini yetu na kama itatekelezwa, huo ndio utakuwa mwisho wa hii daylight robbery niliyoizungumzia hapa!.

Hongera Prof. Kabudi, Hongera Rais Magufuli, ila msilazimishe, kaeni mezani na watu hawa, mkubaliane a win win situation.

Paskali
 
 
Ilipoletwa miswada ya mafuta na gas Bungeni kwa hati ya dharura, walio na uchungu na nchi hii walikataa hadi kususia kuijadili.
Hawa wenzetu wa [HASHTAG]#ndiyoooo[/HASHTAG] wakawazomea wenzao na walipomaliza wakagawa rasilimali hiyo!!!
Leo wanamuunga mkono Mheshimiwa Magufuli kupigania mali waliyoigawa muda si mrefu uliopita!!!!
 


pascal

Pascal Mayalla kwasababu nimeona unapenda kusoma na unapenda kuelewa mambo, Kabla hujaandika chochote kuhusu Mafuta na gesi naomba pitia website ya TPDC halafu tafuta document inayoitwa PSA Yaani production sharing agreement.
 
Mambo yaliyoubuliwa na Kamati ya Mhe. Spika japo jana pale Bungeni Dodoma, yanaonekana kama mapya na kuna watu wanashangaa!. Angalia bandiko hili ni la lini na kilisemwa nini humu?.

P.
 
Mambo yaliyoubuliwa na Kamati ya Mhe. Spika japo jana pale Bungeni Dodoma, yanaonekana kama mapya na kuna watu wanashangaa!. Angalia bandiko hili ni la lini na kilisemwa nini humu?.

P.
Mkuu, wahenga wanasema bendera hufuata upepo.

Pamoja na kuchelewa kwa hatua husika tupongeze bunge kwa hatua waliyochukua. Tungependa sana kuwalaumu hata hivyo tutaishia kubezwa na kubeuliwa kwa kukosa uzalendo [emoji2] .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…