Gesi asili: Is it "day light robbery?" Watanzania tunaibiwa mchana kweupe!

Gesi asili: Is it "day light robbery?" Watanzania tunaibiwa mchana kweupe!

Kilio kimojawapo ulichokidai katika bandiko lako Mkuu Pasco ni sera na sheria ya gesi. Hilo limepatiwa ufumbuzi walau sasa tutaangalia ufanisi wake kama umeleta faida kwetu.

Pili, PSA zote zilizoingiwa zifanyiwe marekebisho. Nataraji hili litapata msukumo wa kisiasa na kimamlaka kupitia Azimio la Bunge. Kamati husika imeshawasilisha taarifa tusubiri utekelezaji wa wakubwa.
 
Kaka tatizo linaazia kwenye katiba na miaka ya uraisi kukaa madarakani ipunguzwe hii itatusaidia kujua yupi anafaa yupi hafai pia tuwe na Uhuru wa kumtoa madarakani raisi ambaye hatufai raisi anakaa miaka mitano anatuingiza mkenge bado akitoka hatuna haki ya kumshitaki huoni huo ni ujinga wa hali ya juu tatizo lipo kwenye katiba tunaitaji katiba yenye nguvu "MTU kasaini mkataba feki bado anatoka madarakani tunamchekea tu ameisha haribu nchi sisi tunafurahi tuu yaani inatakiwa kiti cha uraisi wakione kama kifo na ubunge ndio wataheshimu maliasili zetu" my idea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanabodi,

Nimekutana na hii kitu, nimeisoma, sio tuu nimeshangaa, bali nimechoka, imeniacha hoi, ukisoma ukaona jinsi tunavyoibiwa rasilimali zetu, na wanaofanya tuibiwe, ni wenzetu tuliowapa dhamana ya kutuongoza, mtu unaweza kupata wazimu, ukarukwa na akili, ukikamata SMG, unaweza kuwamiminia risasi Watanzania wenzetu wanaoiuza nchi yetu na maliasili zake kwa bei ya bure kwa wageni kwa jina la wawekezaji kwa kisingizio kuwa sisi hatuna uwezo wa kuwekeza ili kuvuna rasilimali hizo zitufaidie!.

Mpaka hapa tulipo, Tanzania tumesha ibiwa sana kwenye madini kutokana na mikataba mibovu ya kinyonyaji na mpaka sasa ninapoandika haya, bado tunaendelea kuibiwa kwa mikataba hiyo hiyo mibovu iliyoingiwa na wenzetu. Sasa Mwenyeenzi Mungu katupa gesi asili angalau ituokoe kutoka katika hili lindi la umasikini uliotopea...lakini kumbe..., masikini Watanzania!, sijui nani katuloga!, maana na huku kwenye gesi asili, Watanzania tunaendelea kuibiwa mchana kweupee! huku wenyewe na hawa makuwadi tunaowaita ni viongozi wetu, tukiangalia tuu kama mazuzu!. Nchi hatuna sera ya gesi, hatuna sheria ya gesi!, hatuna lolote tulijualo kuhusu uchumi wa gesi, lakini ndio bado tunashadadia kugawa vitalu vya gesi kama njugu!.

Hadi hapa ninapopandisha uzi huu, mwaka huu wa 2012, nchi yetu hatuna sera ya gesi wala sheria ya gesi lakini tumeingia mikataba 23 ya PSA ambayo in reality, we are getting almost nothing!, nil!. Hii ni "day light Robbery!" na inafanywa na viongozi hawa hawa tulio nao tukidhani ni wenzetu lakini kumbe. ..

Hebu soma hapa chini!.

After studying the experience from other countries, the following lessons were learnt:
  • Location of LNG Plant &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; should be constructed on land (not floating LNG on sea)

  • Reasons: Mainly for monitoring and control purposes &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; monitoring is challenging because of lack of technology and control means

  • There should be only one plant.
  • The GoT/Tanzanians/Public should have majority shares to the entire
  • Infrastructure say not less than 51% &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; to have authority say and decisions making for the benefit of the country. It may be on PPP model.

  • The proposed land for construction of LNG and other industries utilizing natural gas should be owned by the government. Facilities like roads, water and electricity should be put by GOT and appropriate tariff should be determined for the government.

  1. KWA GESI ALIYOTUJALIA MWENYEZI MUNGU, TUKIJIPANGA VIZURI, TUTAPATA MAENDELEO MAKUBWA KULIKO AMA KAMA SOUTH AFRICA.
  2. MAKAMPUNI MAKUBWA YA UTAFUTAJI WA MAFUTA NA GESI YANAELEWA NA YANATAKA TUBAKI KWENYE HALI YA KUTOELEWA HALI YA BIASHARA YA GESI. YANATULAGHAI KWA NJIA YA UZOEFU NA WALIONAO.
  3. GAS HATA KAMA IKO CHINI YA BAHARI AU CHINI YA ARIDHI NI MALI YETU NA INAYO VALUE YAKE NA SIO MWENYE UWEZO WA KUITOA ARIDHINI BASI NDIE MWENYE GAS DARWIN THIORY ISITUMIKE KWA MALIASILI YA NCHI YETU.
MY TAKE!.
1. Kwa kukosekana sera na sheria ya gesi, kumbe gesi yote inayovunwa nchini sasa na itakayoendelea kuvunwa miaka ijayo, siyo yetu!, ni ya mwekezaji!.

2. Kumbe eti hiyo gesi huko ilipo haina thamani yoyote kwetu, its zero value, ikiwa huko chini ardhini ilipo, na wala sio mali yetu!, bali ni mali ya mwekezaji anayeichimba na sisi tunauziwa kwa bei ya soko, na faida yote ni ya mwekezaji anayechimba, ila taifa litafaidika na kodi!. Huu ndio upuuzi tulioufanya kwenye madini, madini yote ni ya mwekezaji!, sisi tunalipwa mrahaba na kodi tuu za serikali!.

Bila ya sera na sheria, tuna haraka gani?. Baada ya mkataba wa Songas, tumeshindwa nini kuandaa sera na sheria kwanza ndipo tukaendelea kugawa vitalu vya utafutaji na uchimbaji wa gesi asilia?.

Nimeshindwa kuendelea kwa sasa kutokana na hasira!, unaweza ukaua mtu! . Labda mbele ya safari, kutakuja kutokea kichaa mmoja akiyajua haya ambayo hawa viongozi wetu wametutendea kwa kutokujua kwetu anaweza kupandwa hasira na kuwamiminia risasi wahusika wote wakuu walio yafanya haya au kuachia yafanyike katika ardhi ya Tanzania na kama wametangulia mbele ya haki, akawachapa bakora juu ya makaburi yao!.

Haya akinasisi tunayaona leo, tunayapigia kelele, huku wahusika wakuu wakijifanya kutia pamba masikioni, halafu akija kujitokeza kiongozi mzalendo kwa siku zijazo, akayaibua haya, Watanzania tutajifanya kushangaa na kuingia hasira kwa jinsi tunavyoibiwa!.

Baada ya kuipokea hii document, nilifanya personal initiative ya kuifungia safari hadi Bungeni Dodoma, nikaikabidi kwa baadhi ya wabunge, akiwemo Mwenyekiti wa POC, Mhe. Zitto Zuberi Kabwe na Waziri Kivuli wa Madini, Mhe. JJ Mnyika, hebu tusikilizie if anything will be done about this, vinginevyo ni Watanzania tunaendelea kuibiwa mchana kweupe, na wanaofanya tuibiwe ni hawa wenzetu tuliowaamini na kuwakabidhi nchi yetu hii!.

Sijui ni nani aliyetuloga!.

Mungu Ibariki Tanzania!.

Paskali

Just a hint: huu mradi ndiyo ulikwamisha mradi wa Stieglers Gorge tangu siku nyingi huko nyuma. Ukipenda unaweza ukaniuliza swali kwa nini nasema hivi!
 
Just a hint: huu mradi ndiyo ulikwamisha mradi wa Stieglers Gorge tangu siku nyingi huko nyuma. Ukipenda unaweza ukaniuliza swali kwa nini nasema hivi!
Mkuu Makanyaga, naomba nisikuulize, kwasababu mradi Stieglers gorge ulikuwepo siku nyingi sana tangu enzi za Mwalimu na ulikwamishwa na environmental issues na Word Heritage site ya Unesco, wakati huo hata gesi ya Songosongo haijagunduliwa, achilia hii gesi ya Mtwara ya juzi, hivyo huwezi kusema gesi ya Mtwara ndio imekwamisha Stieglers gorge.
P
 
Mkuu Makanyaga, naomba nisikuulize, kwasababu mradi Stieglers gorge ulikuwepo siku nyingi sana tangu enzi za Mwalimu na ulikwamishwa na environmental issues na Word Heritage site ya Unesco, wakati huo hata gesi ya Songosongo haijagunduliwa, achilia hii gesi ya Mtwara ya juzi, hivyo huwezi kusema gesi ya Mtwara ndio imekwamisha Stieglers gorge.
P

Umefanya vyema kutokuniuliza, maana mjadala wake ungeweza kuwa mrefu sana. Hata hivyo naomba nikutonye tu kuwa, oil and gas ilikuwa inajulikana tangu huko nyuma kuwa ipo, isipokuwa tu ilikuwa haijulikani kuwa iko wapi! Swala lilikuwa si kwamba haipo hapana, ila ilikuwa ni kwamba iko wapi! Uhakika wa kuwa Gas ipo tangu huko nyuma ulikuwepo, kwa sababu wataalamu wa mambo ya fossils walikuwa wameshaona tayari!Teknolojia yake kwa hapa nchini ndiyo ilikuwa haijakamilika kisawasawa.

Hizo sababu zingine unazozijua wewe kuhusiana na swala hili ni za kisiasa na si za kisayansi!
 
Naomba unambie sababu za kisayansi
Umefanya vyema kutokuniuliza, maana mjadala wake ungeweza kuwa mrefu sana. Hata hivyo naomba nikutonye tu kuwa, oil and gas ilikuwa inajulikana tangu huko nyuma kuwa ipo, isipokuwa tu ilikuwa haijulikani kuwa iko wapi! Swala lilikuwa si kwamba haipo hapana, ila ilikuwa ni kwamba iko wapi! Uhakika wa kuwa Gas ipo tangu huko nyuma ulikuwepo, kwa sababu wataalamu wa mambo ya fossils walikuwa wameshaona tayari!Teknolojia yake kwa hapa nchini ndiyo ilikuwa haijakamilika kisawasawa. Hizo sababu zingine unazozijua wewe kuhusiana na swala hili ni za kisiasa na si za kisayansi![/QUO
 
Naomba unambie sababu za kisayansi

Tayari nimeshazitaja kwenye post hiyo, isome vizuri. Yaliyobaki unatakiwa sasa ujiongeze wewe mwenyewe, ya kuambiwa chnaganya na ya kwako. Huwezi ukaanza kudadavua issues za namna hiyo kwenye mtandao kama uko makini!
 
Mkuu Makanyaga, naomba nisikuulize, kwasababu mradi Stieglers gorge ulikuwepo siku nyingi sana tangu enzi za Mwalimu na ulikwamishwa na environmental issues na Word Heritage site ya Unesco, wakati huo hata gesi ya Songosongo haijagunduliwa, achilia hii gesi ya Mtwara ya juzi, hivyo huwezi kusema gesi ya Mtwara ndio imekwamisha Stieglers gorge.
P
Lakin kwann tunafanya vitu nusu nusu, kwann tusinge malizana na gesi kwanza ndio tuanze hilo bwawa? Je nini hatma ya gesi baada ya magu kusema imechukuliwa na mabeberu?

Kama gesi imekua hivyo je hili bwawa hatutaambiwa nalo limechukuliwa na mabeberu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom