Gesi asili: Is it "day light robbery?" Watanzania tunaibiwa mchana kweupe!

Kilio kimojawapo ulichokidai katika bandiko lako Mkuu Pasco ni sera na sheria ya gesi. Hilo limepatiwa ufumbuzi walau sasa tutaangalia ufanisi wake kama umeleta faida kwetu.

Pili, PSA zote zilizoingiwa zifanyiwe marekebisho. Nataraji hili litapata msukumo wa kisiasa na kimamlaka kupitia Azimio la Bunge. Kamati husika imeshawasilisha taarifa tusubiri utekelezaji wa wakubwa.
 
Kaka tatizo linaazia kwenye katiba na miaka ya uraisi kukaa madarakani ipunguzwe hii itatusaidia kujua yupi anafaa yupi hafai pia tuwe na Uhuru wa kumtoa madarakani raisi ambaye hatufai raisi anakaa miaka mitano anatuingiza mkenge bado akitoka hatuna haki ya kumshitaki huoni huo ni ujinga wa hali ya juu tatizo lipo kwenye katiba tunaitaji katiba yenye nguvu "MTU kasaini mkataba feki bado anatoka madarakani tunamchekea tu ameisha haribu nchi sisi tunafurahi tuu yaani inatakiwa kiti cha uraisi wakione kama kifo na ubunge ndio wataheshimu maliasili zetu" my idea

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Just a hint: huu mradi ndiyo ulikwamisha mradi wa Stieglers Gorge tangu siku nyingi huko nyuma. Ukipenda unaweza ukaniuliza swali kwa nini nasema hivi!
 
Just a hint: huu mradi ndiyo ulikwamisha mradi wa Stieglers Gorge tangu siku nyingi huko nyuma. Ukipenda unaweza ukaniuliza swali kwa nini nasema hivi!
Mkuu Makanyaga, naomba nisikuulize, kwasababu mradi Stieglers gorge ulikuwepo siku nyingi sana tangu enzi za Mwalimu na ulikwamishwa na environmental issues na Word Heritage site ya Unesco, wakati huo hata gesi ya Songosongo haijagunduliwa, achilia hii gesi ya Mtwara ya juzi, hivyo huwezi kusema gesi ya Mtwara ndio imekwamisha Stieglers gorge.
P
 

Umefanya vyema kutokuniuliza, maana mjadala wake ungeweza kuwa mrefu sana. Hata hivyo naomba nikutonye tu kuwa, oil and gas ilikuwa inajulikana tangu huko nyuma kuwa ipo, isipokuwa tu ilikuwa haijulikani kuwa iko wapi! Swala lilikuwa si kwamba haipo hapana, ila ilikuwa ni kwamba iko wapi! Uhakika wa kuwa Gas ipo tangu huko nyuma ulikuwepo, kwa sababu wataalamu wa mambo ya fossils walikuwa wameshaona tayari!Teknolojia yake kwa hapa nchini ndiyo ilikuwa haijakamilika kisawasawa.

Hizo sababu zingine unazozijua wewe kuhusiana na swala hili ni za kisiasa na si za kisayansi!
 
Naomba unambie sababu za kisayansi
 
Naomba unambie sababu za kisayansi

Tayari nimeshazitaja kwenye post hiyo, isome vizuri. Yaliyobaki unatakiwa sasa ujiongeze wewe mwenyewe, ya kuambiwa chnaganya na ya kwako. Huwezi ukaanza kudadavua issues za namna hiyo kwenye mtandao kama uko makini!
 
Lakin kwann tunafanya vitu nusu nusu, kwann tusinge malizana na gesi kwanza ndio tuanze hilo bwawa? Je nini hatma ya gesi baada ya magu kusema imechukuliwa na mabeberu?

Kama gesi imekua hivyo je hili bwawa hatutaambiwa nalo limechukuliwa na mabeberu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…