Mangi shangali
JF-Expert Member
- Feb 9, 2023
- 533
- 820
Natumaini wote wazima humu,japo changamoto zipo ila tunatakiwa tukomaye nazo maana haina jinsi:
Hizo changamoto tumeumbiwa sisi binadamu,hata uende wapi zipo pale zinakusubiri.
Nimependezewa niwaletee niliyoyapitia katika ukuaji wangu mpaka nilipofikisha 20s,najua utajifunza moja au lingine.
Mangi shangali..
ARUSHA,TANZANIA.
YAFUATAYO YANAFURAHISHA..
UTANGULIZI:-
NIlizaliwa katika hospital ya mount meru iliyopo katika jiji la arusha.kipindi hicho baba alikuwa anafanya kazi katika benki ya nbc,mama alikuwa mfanya biashara soko kuu arusha kipindi hicho soko lilikuwa linaitwa soko la bondeni kitambo hicho..
Katika ukuaji wangu na story nilizopewa na wazazi wangu pamoja na ndugu zangu waliokuwa nami nilipokuwa mtoto.
Mama anasema nilikuwa mtundu sana tena ujeuri,nilipokuwa na miaka 4 nilikuwa najifungia kwenye friji,kwa watu wanajua yale mafriji ya zamani yalikuwa makubwa sana sasa nilikuwa naingia ndani,nakujifungia humo mama ananitafuta kumbe nipo ndani ilikuwa tafurani sana.
Mama anasema nilikuwa nashika kiwembe najikata mwenyewe mkononi na hata sitoi chozi,nilikuwa na matukio ya hatari kuna siku nilichomeka pasi mkutani nikipigwa na shoti nikazimia kwa masaa 6 watu walijua nimekufa.
Tulikuwa na mtindo wa kudandia gari kwa nyuma, lilechuma lakupanda lilikuwa limeoza kuwa kutu silikakatika bana niliburuzwa mpaka ngozi kwenye tumbo zikatoka.
Aisee ngoja nifupishe maana nilikuwa na matukio ya hatari sana ambayo kama sio kudra za mwenyenzi MUNGU nisingekuwa hai leo hii..
Nilipofikisha umri wa kwenda darasa la kwanza nilijiunga katika shule ya sanawary iliyepo arusha,nilisoma vinzuri mpaka kufika darasa la 4 ndio tatizo lilianza maana nilikuwa ujeuri shuleni na mkorofi,wanafunzi niliyesoma nao kipindi hicho walipata joto ya jiwe maana nilikuwa sionewi ovyo,nilikuwa napigana na walionizidi darasa tena la saba.
Shule tulikuwa na tabia ya kupigana
Tunaenda mtoni huko hakuna watu,natafutiwa mbabe wanaomuona ubabe wao natembeza kichapo heavy nikawa naogopeka shule nzima mpaka vijana wa darasa la Saba waliniwazia maana nishawatandika wababe wao .walimu walipata tabu nilipogoma kusoma hakuna mwalimu alithubutu kunichapa nilipochelewa namba na usafi sikupe ratiba yeyote ya usafi darasani.
Niliingia shule mda walimu wanaingia tena mikono mfukoni,nilikuwa mkorofi ila darasani sikuwahi kushuka chini ya mtu wa 5,matokeo ya mitihani nilifanya vyema.
Itaendeleea...