Get Rich or Die Tryin: Niliyoyapitia katika ukuaji wangu

Get Rich or Die Tryin: Niliyoyapitia katika ukuaji wangu

SEHEMU YA PILI:=..
baada ya kufika merelani moja kwa moja nilipelekwa maghetoni wanapoishi mabrother.daah chumba cha matope kichafu hakuna anayefanya usafi,machupa ya bapa za konyagi kibao na mapusha ya bangi,unga wa ugali wa dona na dagaa kwenye kiroba ndo zilikuwa kwenye hicho kichumba kifupi fupi.

Nikaweka begi kwenye moja ya msumari uliokuwa nyuma ya mlango,basi brother Joseph akaniambia twende nikakuonyeshe site nikamwambia site gani??akasema wewe twende.
Nikadandia bike safari kuelekea site,mitaa miwili mitatu tukaibuka machimboni,aisee nilishangaa kuona vibanda kibao chini kuna mashimo ndo migodi yenyewe.

Nilikutana vijana kibao wakiwa wamejaa ulanga mpaka machoni,wengine wamelala juu ya michanga wamechoka kwakupigika na msoto wa merelani,
Aisee merelani juu ni kali sana yani kuna ukame wa maana vumbi na funza wasio na idadi,maji ni shida sana watu wakipata kiu wanashushia pombe.

Mabroker ndo wanamaisha manzuri utawakuta wamevaa cheni za silver wamezungukwa na machawa kibao ndo walinzi wao:
Kule kuna migodi mingi sana,kuna inayotumia machine kushuka chini amabayo ina air conditioner mpaka chini,mingine isiyona machine inatumia kamba kushuka mantle,inayotumia digger kuchoronga mwamba.

Basi brother akaniambai hautazama kwa sasa,nikamwambia mimi nataka kushuka akaniambia kule ni pabaya na mpaka uwe na udhoefu kidogo maana chini watu ni wanyama sana,mtu kukuchoma kisu ni jambo la kawaida sana,akaniambia wewe utakaa juu kujaza udongo kwenye maroba na kusupply mahitaji mpaka pale utakapo zoea kazi.

Basi sikuwa na lakubisha maadamu kabonga kaka mkuu nikaitikia kishingo upinde.harakati zikaanza za maisha ya pale mgodini.
Kazi yangu ilikuwa ni kutafuta maji mtaani na kupeleka mgodini,kusupply mahitaji yawanapolo,na kuuza maroba ya kujazia udongo wa mantle.


Kweli niliparangana Kule bila kuchoka,sasa nikaanza uvutaji wa bangi kwa mara ya kwanza,maisha ya kule lazima uvute bangi kuna msoto wa kufa mtu,hakuna cha utoto wa mama,ukiwa kule automatic unakuwa katili tuu,chakula cha kule ni ugali dagaa,maharage kabichi.wali utanunua kwa mama ntilie mtaani.

Nilipiga kazi kwa bidii nikawa peace kwa kila mtu..
 
Acha utoto, eti nilizaliwa miaka ya 90 kitambo hiyo. We bado mdogo ndiyo maana unaandika mambo ya kitoto
Aisee mnaboa kishenzi asa kama umeona ya kitoto unaendelea kusoma ya nn Kuna maelfu ya nyuzi humu ndani si ukasome hizo? Mtu katoa time yake kushare Cha kwakwe [emoji1745]afu mnadiss kijinga ...
 
Aisee mnaboa kishenzi asa kama umeona ya kitoto unaendelea kusoma ya nn Kuna maelfu ya nyuzi humu ndani si ukasome hizo? Mtu katoa time yake kushare Cha kwakwe [emoji1745]afu mnadiss kijinga ...
Big up
 
SEHEMU YA TATU:=...

Baada ya kuparanga kwa miezi 5 juu bila kuzama shimoni,siku hazigandi niliruhusiwa kuingia mgodini kwa mara ya kwanza ila niliambiwa utakuwa unaenda duniani kuleta bidhaa kwa ajili ya wazamiaji nikasema asante MUNGU..

Basi kesho yake tuliingia shimoni mda wa saa 3 usiku,aisee kuzama chini kama wewe mtoto wa mama unaweza kuachia kamba ukasababisha wengine kufa,maana ni parefu sana.
Sasa mimi nilipewa kazi ya kufuatilia mahitaji dunia,aisee ukipewa hicho kitengo sio powah maana ndani ya dakika 50 unaenda duniani alafu upo mwenyewe chini kuna giza la kufa mtu.

Huko chini kuna routes nyingi unaweza ukakosea njia ukajikuta unazunguka tu,mara huone kitu kimesimama mbele yako omba MUNGU tochi isiishe nguvu,kama muoga unadata mwenyewe ndo maana bangi inavutwa sana na pombe kali.

Nilipewa jina la kiberenge maana nilikuwa naenda dunia kwa dakika 45 na kugeuza fast,nilikomaa kwenye hicho kitengo mpaka nilipofikisha miaka 21 nikaanza kupiga tindo,na kufanya kazi zote za wanapolo.

Kuna siku inakuwa ni kazi ya kujaza viroba udongo,unaweza ukapewa sekta ya kushikilia viroba ili vijazwe udongo yani unainama mpaka ugongo unauma.
Alafu unatakiwa uwe fasta kiroba kinawekwa chepe 2 za udongo kinarushwa pembeni.hapo unapokusanyia viroba hata mtu aliyepembeni humuoni kwa wingi wa viroba.

Kazi ya kujaza viroba inachukua siku 2 au 3,ikishamalizika inakuwa kazi ya kupandisha viroba juu hapo ndo kwenye msoto wa maana,kiongozi anasema kila mtu ashikilie kamba yani tunajipanga kwanzia chini mpaka juu kwa umbali wa mita 15 kila mtu.
Aliyechini yako anakuwekea kiroba pembeni wewe unakichukua unakiweka kwa mwenzako aliyejuu yako yani fast fast hakuna kupoa,ukichelewa tu unarundukiwa viroba vingi.
 
SEHEMU YA 4:=....
Ikanibidi niendelee na shughuli za uchimbaji,nikawa nachimba hapa ma pale.
Kiukweli hali ya kule ni ngumu sana kuna msoto wa kufa mtu,na ukishahamua kwenda kule lazima huupitie tuu hakuna jinsi.

Kama hujawahi kuyaona au kuyasikia maisha ya kule aisee kuna mda nilitamani kukimbia mazima.
Kufa kule ni kitu cha kawaida,mtu kukuchoma kisu ni kawaida mnoo.

Nilipata tag la kuwa na mabrother karibu,kwa kuwa nilikuwa mdogo hiyo ndo ilikuwa afueni yangu.basi nikawa naendelea na harakati za uchimbaji madini.

Shimoni tunaingia usiku na matorch yetu,kazi yetu ni kutindua na kupiga nyundo mwanzo mwisho,kuna siku tu apiga baruti.

Kulala kule huwezi yani utasinzia kwa dakika kadhaa na kushituka kwa sababubya hali ya kule.

Kuna siku bahati ilikuwa kwangu,nilizama shimoni nikawa na mabrother wakaniambia leo utatindua sisi tutakuwa pembeni,katika kutindua MUNGU sio athumani nikaona bonge la jiwe hakuna mwingine aliyeona zaidi ya mabrother maana linangaa sana gizani.
 
Back
Top Bottom