Get Rich or Die Tryin: Niliyoyapitia katika ukuaji wangu

Get Rich or Die Tryin: Niliyoyapitia katika ukuaji wangu

SEHEMU YA 6:=.....
INAENDELEEEEA...
Basi tukanywa na kuvuta bangi mpaka saa 3 asubuhi tumelewa kinyama,brother Fred akasema kasha wasiliana na broker mmoja tuende tukauze jiwe.

Tukafika officine kwa broker kwa jina anaitwa laizer,tukaaza kubagain bei ya jiwe jamaa akatupa million 65 aisee kipindi hicho cha 2005 pesa hiyo ilikuwa kubwa mnoo asikuambie mtu.

Mzigo akakabidhiwa kaka Fred,moja kwa moja safari kuelekea maghetoni kufika tu ndani kaka Fred akasema dogo tunakusikiza wewe pesa zako hizi hapa amua utazifanya nini..

Nilawaambiwa hapa ni pasu pasu basi pesa zikagawanywa kwa watu wa4,wao watatu wakachukua million 15 kila mmoja mimi ndo wakanipa million 20.

Kwa mara ya kwanza nashika million 20 tena nikiwa na miaka 21,toka utoto wangu sijawahi kushika hata 10000 ya kwangu nilijiona nina bonge la bahati.

Ilikuwa siku ya j5 asubuhi wote wa 4 tukadandia bike tukiwa na ulanga mwilini..

Tulifika chugah saa 7 mchana, mama nikampa 1million dingi nikamkabidhi 3 million nikabakiwa million 17 hivi.

Nikaenda kisongo nikanunua heka 20 za shamba kwa million 7..
Nikabakiwa na million 10, kwetu sisi kila kijana anapewa eneo lake dingi alinipaga room 4 zilikuwaga za udongo, wapangaji nikawapa notice wahame zile room 4 nikajenga za matofali.
Katika matumizi yangu ya ujenzi nilitumia million 6 mpaka nyumba kuisha hiyo nazungumzia 2005.cement ilikuwa inauzwa 5500, bati linauzwa 6000 tofali moja lilikuwa linauzwa 500.

Basi nikabakiwa na million 4, nikatoa million 1 nikanunua vitu vya ndani kitanda, makochi, tv la chogo,friji na mazaga mazaga mengine kipindi kile ukinunua tv hesima mtaani..

Katika matumizi yangu yote niliyofanya nikabakiwa na million 1.5.
Kwakuwa nilipendaga kupendeza kwa pamba nikazama soko la kilombero kipindi kile lile soko la mwanzo lipo, sasa hivi wamefanya stend ya daladala.

ITAENDELEA........
 
Kwa mara ya kwanza nashika million 20 tena nikiwa na miaka 16,toka utoto wangu sijawahi kushika hata 10000 ya kwangu nilijiona nina bonge la bahati
Huko nyuma si ulisema uliingia mgodini ukiwa na miaka 15 kwakua ulikua mdogo wakasema usizame shimoni.
Ukaanza kuingia chini ukiwa na 21 yrs, hapa tena unasema umepata mpunga mrefu ukiwa na 16 yrs, umri wako unarudi nyuma??
 
Huko nyuma si ulisema uliingia mgodini ukiwa na miaka 15 kwakua ulikua mdogo wakasema usizame shimoni.
Ukaanza kuingia chini ukiwa na 21 yrs, hapa tena unasema umepata mpunga mrefu ukiwa na 16 yrs, umri wako unarudi nyuma??

Time traveler [emoji1787]
 
Time traveler
emoji1787.png

Time traveler [emoji1787]
Sio kweli siamini time travel
 
Huko nyuma si ulisema uliingia mgodini ukiwa na miaka 15 kwakua ulikua mdogo wakasema usizame shimoni.
Ukaanza kuingia chini ukiwa na 21 yrs, hapa tena unasema umepata mpunga mrefu ukiwa na 16 yrs, umri wako unarudi nyuma??
Huyu jamaa ni Muongo Muongo mnooo toka mwanzo nimemshitukia
 
SEHEMU YA SABA:=....
basi baada ya kuzama soko la kilombero nilinunua viatu na nguo za kutosha.

nilikaa kitaa kwa miezi huku nikiwa nakula bata mara triple A,silk club na ma wingu kila weekend,katika kukaa kwangu mtaani kuna demu alikuwa student nilikuwa natoka naye bahati mbaya alipata ujauzito,msala ulikuwa mkubwa sana ikanibidi nikimbie kitaa.

Nikaenda mgodini kupigika tena,dingi akapambana na wazazi wa yule binti,wakakubaliana kuwa nimchukue binti yao ila faini nilitozwa pia.

Basi binti akaenda kuishi kwenye zile room 2 maana zingine nilipangisha akawa mke wangu,mimi nikiwa machimboni..

Nikaendelea na msoto wa kila siku,mawe yakawa magumu kutoka,hali ikazidi kuwa mbaya,siku nimejilaza kwenye udongo nikiwa nimechafuka hatari,mzee akanipigia simu na kuniambia kuna mtu kapenda shamba langu yupo tayari kulinunua.

Basi nikafunga safari kurudi arusha,kufika wife tumbo tayari kubwa na zimebaki siku chache ili ajifungue na ukicheki sina kitu,na wapangaji washanipa kodi siwadai.

Nikaona bora niliuze,kumbe mtej mwenyewe alikuwa geor davie wa ngurumo ya upaka,tukafikia makubaliano ya kuuza akanipa million 17,maana shamba lilikuwa barabarani na anataka kufungua kanisa,kipindi hicho bado hajawa maarafu kama alivyosasa.

Basi nikapokea pesa,nikaona niachane na uchimbaji madini ile kazi inamsoto sana na nihatari sana,nikaona niachane nayo.
Nikafungua account bank nikatia million 15,wife tayari siku zimewadia akajifungua mapacha wawili wote wanaume.




Itaendeleeeea..................
 
Kwanza hyo migodi ya dhahabu au almasi.....

Yaani kidonge cha dhahabu kiwe na garama ya mili 75 tena miaka ya 2000...[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom