Get Rich or Die Tryin: Niliyoyapitia katika ukuaji wangu

Get Rich or Die Tryin: Niliyoyapitia katika ukuaji wangu

SEHEMU YA NANE:=......

BAADA YA wife kuleta mapacha tulifurahi sana,mzee akachinja beberu la mbuzi kwa furaha,basi tukala ndafu na beer za kutosha ikawa furaha siku zikasonga mbele.

Nika kaa chini na wife nikamwambia kuwa sitaenda tena mgodini akasema asante baba,basi katika kitu cha kutafakari ni fanyie ile million 15 nini likaja wazo la kusoma,katika kuchunguza nitarudije darasani nikapata mtu akaniambia nisome qt ambayo ni form 1 mpaka 4 kwa miaka 2 tu.

Nikaona kipindi nikiwa nasoma niwe na kitega uchumi kitakacho niingizia pesa
Kila siku,basi nikanunua hiace nikapata route ya stand kwenda USA river,pesa nyingine nikamfungulia wife saloon ya kike, pesa iliyobaki nikalipa qt ya miaka 2.

Nikasoma qt kwa miaka 2 MUNGU akanisaidia nikamaliza,ila matokeo hayakuenda vinzuri nikapata division 4 ya 27,nikaone nisome tour guide,nika apply mweka chuo cha utalii na wanyama pori pale nikapiga kwa miaka 3,nikamaliza nikapata kazi ya kwanza katika kampuni ya zara tours.
Nikafanya kwa miezi 8,MUNGU akaninyooshea mkono nikaajiriwa na leopard tours..


Itaendeleeeea...maana huku ndo kwenye utamu ,maana katika kuwa professional tour guide nimepitia mambo makubwa sana,na kufanya mambo makubwa nipeni mda maana mchana nakuwaga na wageni,ila jioni kama hivi ndo napata mda wa kuandika,kama kuna wengine nawakera nisameheni,au kama kuna pengine nilipo andika hamjaelewa tusamehane mimi binadamu nina mapungufu yangu.

Kuna mtu kaandika huku kuwa nadanganya,labda nikuulize wewe sasa nikudanganye wewe nifaidike na nini??
Kwani huku jamii wanatoa pesa??
Au sifa zinaleta pesa??

Yote niliyoandika nimepitia mimi,na nimeandika yawe kama funzo,maana kuna wazazi wanawapangia watoto zao nnjia za maisha,ndo maana sasa hivi kuna jobless wengi mtaani,mimi nilifuata nnjia zangu,na leo nakula matunda ya mawazo yangu..

Wale niliosoma nao shule ya msingi wakaendelea secondary sasa hivi maisha mabovu,wamekata
ringi mazima.

Basi ndugu usi judge kitu usichokuwa na uhakika nacho..
 
SEHEMU YA TISA:=.......
BASI baada ya kuajiriwa na leopard rours shida ikaanzia hapo,ghafla nikaanza kufilisika kazi nikasimamishwa,ile hiace niliyonunua ikapata ajali,mpaka saSa hivi ipo pale central imeshikiliwa,kwangu na kwa familia mambo yakawa magumu,dingi akafariki daah nilipata majanga sana.

Huwezi amini nikaanza kuwa mlevi,ni kawa boda boda mtaani tena namtafutia mtu hesabu nilifikisika manzima,afya ikadorora kwa unywaji wa pombe,bangi ndo ikawa chakula kwangu toka asubuhi mpaka jioni navuta bangi tu mpaka mdomo ukawa mweusi kama wa kunguru,macho mekundu yani ulikuwa ukinitizama unajua huyu mvutaji bangi.

Kipindi hicho zile pombe ya vijogoo na banana ndo imepamba moto,nikawa mlevi sana,mama kila kukicha akawa analia tu,wife akarudi kwao watoto tayari washakuwa na umri wa kwenda chekechea sina kitu chochote.

Nikauza vitu vyote vya ndani,nikawa na lala chini,nguo sibadilishi wala siogi hata week 2 zinaisha,mvua ikininyeshea ndo tayari nimeoga.

Nilikuwa siamini uchawi kama upo,toka nikiwa mtoto sijawahi kuamini ila nikaanza kuamini nimerogwa,usiku silali nanyongwa nikaanza kukimbia nyumba na kulala club za gongo,siku nyingine mtaroni popote pale nilikuwa nalala.

Watu wakawa wananicheka nimefulia,madharau mtu hujamchokoza anakupiga makofi bila sababu kweli hali kwangu ilikuwa mbaya,ndugu wakaanza kugombania mali halizoacha baba,ikawa vita juu ya vita.

Siwezi kuamini siku napata taarifa ya msiba kuwa kaka zangu wawili wamepata ajali ya pikipiki ngurero nawamekufa hapo hapo,aisee nililia sana,basi tukafanya msiba tukawapumzisha kaburini.

Tatizo likaja nyumba zile waliojenga kaka zangu hati waliwakabizi wake zao,wakazingangania kuwa nizao basi tukaona tuwaachie.

Ndugu upande wa baba wakagombania mali za kaka yao,ikawa uchawi live unaona bila chenga,mara kwenye mpaka wa shamba unakuta sanda,nazi zimevunjwa yani ikawa tabu juu ya tabu.

Mali za baba zikagawanywa ndugu wakachukua zote mama akabaki na room 3 tu tena za udongo,wewe sikia ndugu tu yani hakuna watu wabaya kama ndugu..
Kipindi hicho nadharaulika sisikikizwi tena kwenye kikao cha familia sikuruhusiwa kuingia ndani waliniita mlevi sina point ya kutoa daah haya maisha yasikiye tu..

Boda boda nayo akapewa mtu,nikawa sina kazi yeyote ile yani nikawa mweupe ile room 4 zangu zikaanza kupasuka ukutani,ukuta wa nyuma ukaanguka,zile bati nikauza zote ela niliyopewa nikalowea pombe yote.

Yani sijui nikumbiaje,akili ilifungwa manzima nikawa nafikiria pombe na bangi mda wote,chakula nilikiona sumu hali ikazidi kuwa mbaya,aisee nilikuwa nimekufa nikiwa bado hai..

Huwezi kuamini kama ndo yule niliyekuwa na hiace,familia bora mtu yeyote alipokuwa anahadithiwa maisha yangu ya zamani yalivyokuwa manzuri aligoma kuwa sio mimi.

Aisee itaendeleeea.....
Haya maisha haya anajua MUNGU tu...
 
Back
Top Bottom