SEHEMU YA PILI:=..
baada ya kufika merelani moja kwa moja nilipelekwa maghetoni wanapoishi mabrother.daah chumba cha matope kichafu hakuna anayefanya usafi,machupa ya bapa za konyagi kibao na mapusha ya bangi,unga wa ugali wa dona na dagaa kwenye kiroba ndo zilikuwa kwenye hicho kichumba kifupi fupi.
Nikaweka begi kwenye moja ya msumari uliokuwa nyuma ya mlango,basi brother Joseph akaniambia twende nikakuonyeshe site nikamwambia site gani??akasema wewe twende.
Nikadandia bike safari kuelekea site,mitaa miwili mitatu tukaibuka machimboni,aisee nilishangaa kuona vibanda kibao chini kuna mashimo ndo migodi yenyewe.
Nilikutana vijana kibao wakiwa wamejaa ulanga mpaka machoni,wengine wamelala juu ya michanga wamechoka kwakupigika na msoto wa merelani,
Aisee merelani juu ni kali sana yani kuna ukame wa maana vumbi na funza wasio na idadi,maji ni shida sana watu wakipata kiu wanashushia pombe.
Mabroker ndo wanamaisha manzuri utawakuta wamevaa cheni za silver wamezungukwa na machawa kibao ndo walinzi wao:
Kule kuna migodi mingi sana,kuna inayotumia machine kushuka chini amabayo ina air conditioner mpaka chini,mingine isiyona machine inatumia kamba kushuka mantle,inayotumia digger kuchoronga mwamba.
Basi brother akaniambai hautazama kwa sasa,nikamwambia mimi nataka kushuka akaniambia kule ni pabaya na mpaka uwe na udhoefu kidogo maana chini watu ni wanyama sana,mtu kukuchoma kisu ni jambo la kawaida sana,akaniambia wewe utakaa juu kujaza udongo kwenye maroba na kusupply mahitaji mpaka pale utakapo zoea kazi.
Basi sikuwa na lakubisha maadamu kabonga kaka mkuu nikaitikia kishingo upinde.harakati zikaanza za maisha ya pale mgodini.
Kazi yangu ilikuwa ni kutafuta maji mtaani na kupeleka mgodini,kusupply mahitaji yawanapolo,na kuuza maroba ya kujazia udongo wa mantle.
Kweli niliparangana Kule bila kuchoka,sasa nikaanza uvutaji wa bangi kwa mara ya kwanza,maisha ya kule lazima uvute bangi kuna msoto wa kufa mtu,hakuna cha utoto wa mama,ukiwa kule automatic unakuwa katili tuu,chakula cha kule ni ugali dagaa,maharage kabichi.wali utanunua kwa mama ntilie mtaani.
Nilipiga kazi kwa bidii nikawa peace kwa kila mtu..