Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Mathalani, muungwana amewasilisha hoja au maoni yake jukwaani, labda ni ya kisiasa, kijamii au kiuchumi, kitaifa au kimataifa.
Anajitokeze muungwana mwingine ambae labda amechoka au amefikia ukomo wa mawazo mapya au fikra mbadala dhidi ya hoja ya msingi mezani anaibuka from no where, hajasoma wala kuelewa hoja yenyewe kiundani anaishia kuonyesha ghadhabu, mihemko, hasira na wakati mwingine anatukana na kuporomosha matusi bila sababu yoyote. Chimbuko la hali hii ni wapi hasa?
Sifahamu anakua ametumia kitu gani kabla, kinachowachochea na kuwahamasisha kuibuka na jazba zilizojaa dhihaka na maneno mbofu mbofu, tofauti kabisa na hoja iliyowasilishwa mezani, aise ni huruma sana. halafu wako uniform dah.
Utofauti wa mawazo, maoni au mitazamo miongoni mwa jamii ni jambo la kawaaida na ndio afya ya majadiliano na utangamano mwema na imara wa jamii nyingi.
Sijui huwa ni mzigo wa mateso mazito, yenye maumivu makali kiasi gani wanapitia, hususani wanasiasa walio ishiwa maono, mbinu, mipango, na mikakati yenye ushawishi wa kuvutia wananchi wengi zaidi upande wao katika jamii ya eneo fulani kwenye majukwaa ya kisiasa.
Dhana ya kujipa umuhimu usio stahili kwamba awazacho yeye ndio mwanzo na mwisho, hakistahili kupingwa au kua challenged, na ndio cha maana na sahihi zaidi kuliko mengine, na saa zingine, mpaka kufikia hatua ya kulazimisha kuhitimisha mjadala au hoja, kwa mihemko, ukali, hasira, ghadhabu, dhihaka na wakati mwingine kuporomosha matusi mazito mazito dhidi ya mwenye mawazo tofauti nae, kitu ambacho sio ungwana na sio msaada kwa yeyote, na wala haibadili chochote.
Na kwamba aliefikia hatua hiyo au anaepitia hali hiyo, ni dhahiri amefilisika kisiasa na ana jaribu kujitambulisha kwa kujifedhehesha mwenyewe, machoni pa wanao muona, wanaomskiza au kumsoma mitandaoni, kwa tabia yake hiyo hiyo kwamba hana tena wazo jipya au fikra mbadala dhidi ya hoja iliyoko mezani, kilichobaki ni kutukana tu.
Kukubaliana kutokubaliana ni dhana muhimu sana kujengeka akilini na mioyoni mwa vibrant and visionary politicians. inasaidia sana kukujengea ustaarabu, ustahimilivu na subra lakini pia hauwezi kupeteza lengo na uelekeo wa siasa zako kwenye medani ya kisiasa 🐒