Ghadhabu, mihemko, hasira na kuporomosha matusi bila sababu yoyote kwenye mijadala ya kisiasa chimbuko lake ni wapi?

Ghadhabu, mihemko, hasira na kuporomosha matusi bila sababu yoyote kwenye mijadala ya kisiasa chimbuko lake ni wapi?

Mathalani, muungwana amewasilisha hoja au maoni yake jukwaani, labda ni ya kisiasa, kijamii au kiuchumi, kitaifa au kimataifa.

Anajitokeze muungwana mwingine ambae labda amechoka au amefikia ukomo wa mawazo mapya au fikra mbadala dhidi ya hoja ya msingi mezani anaibuka from no where, hajasoma wala kuelewa hoja yenyewe kiundani anaishia kuonyesha ghadhabu, mihemko, hasira na wakati mwingine anatukana na kuporomosha matusi bila sababu yoyote. Chimbuko la hali hii ni wapi hasa?

Sifahamu anakua ametumia kitu gani kabla, kinachowachochea na kuwahamasisha kuibuka na jazba zilizojaa dhihaka na maneno mbofu mbofu, tofauti kabisa na hoja iliyowasilishwa mezani, aise ni huruma sana. halafu wako uniform dah.

Utofauti wa mawazo, maoni au mitazamo miongoni mwa jamii ni jambo la kawaaida na ndio afya ya majadiliano na utangamano mwema na imara wa jamii nyingi.

Sijui huwa ni mzigo wa mateso mazito, yenye maumivu makali kiasi gani wanapitia, hususani wanasiasa walio ishiwa maono, mbinu, mipango, na mikakati yenye ushawishi wa kuvutia wananchi wengi zaidi upande wao katika jamii ya eneo fulani kwenye majukwaa ya kisiasa.

Dhana ya kujipa umuhimu usio stahili kwamba awazacho yeye ndio mwanzo na mwisho, hakistahili kupingwa au kua challenged, na ndio cha maana na sahihi zaidi kuliko mengine, na saa zingine, mpaka kufikia hatua ya kulazimisha kuhitimisha mjadala au hoja, kwa mihemko, ukali, hasira, ghadhabu, dhihaka na wakati mwingine kuporomosha matusi mazito mazito dhidi ya mwenye mawazo tofauti nae, kitu ambacho sio ungwana na sio msaada kwa yeyote, na wala haibadili chochote.

Na kwamba aliefikia hatua hiyo au anaepitia hali hiyo, ni dhahiri amefilisika kisiasa na ana jaribu kujitambulisha kwa kujifedhehesha mwenyewe, machoni pa wanao muona, wanaomskiza au kumsoma mitandaoni, kwa tabia yake hiyo hiyo kwamba hana tena wazo jipya au fikra mbadala dhidi ya hoja iliyoko mezani, kilichobaki ni kutukana tu.

Kukubaliana kutokubaliana ni dhana muhimu sana kujengeka akilini na mioyoni mwa vibrant and visionary politicians. inasaidia sana kukujengea ustaarabu, ustahimilivu na subra lakini pia hauwezi kupeteza lengo na uelekeo wa siasa zako kwenye medani ya kisiasa 🐒
Vibaka wa ufipa hao wanao daiwa mabum!
 
si utiririke tu vizur taratibu gentleman 🤣

unatambaa na mihemko kama kawaida dah 🤣

ni vuzuri ukajikita na kudeal na hilo wazo sio mimi. mimi nimetaka tu kufahamu chimbuko na hali ya maumivu na mateso unayoyapitia baada ya kufikia ukomo wako wa wazo jipya na fikra mbadala wa hoja zinazowasilishwa humu na wadau 🐒
Wewe ndio utakuwa unaishi kwa maumivu na mateso hadi umeamua kuwa chawa ili uweze kuishi..
Tatizo langu ni kuona machawa kama wewe unapotosha ukweli ambao upi kwenye jamii.
Acha uchawa wewe boya
 
Unajua maana ya kuchukia UOVU?

Yaani unapata wapi njia za kukemea Hawa wezi wa pesa za umma wenye kuumiza Watanzania Kwa upole?

Kwani Kuna mtu amekuzuia kutumia akili zako sawa sawa?
Hata Bwana Yesu alipoenda kwenye nyumba ya Ibada na kukuta biashara inafanyika humo...hakuwakemea kwa upole. aliwakemea kwa ukali
 
Wewe ndio utakuwa unaishi kwa maumivu na mateso hadi umeamua kuwa chawa ili uweze kuishi..
Tatizo langu ni kuona machawa kama wewe unapotosha ukweli ambao upi kwenye jamii.
Acha uchawa wewe boya
maumivu ya kuporomoshwe matusi na kutukanwa matusi mazito mazito kwa mihemko na ghadhabu za kiwango cha juu sana, si eti?🤣
 
Hata Bwana Yesu alipoenda kwenye nyumba ya Ibada na kukuta biashara inafanyika humo...hakuwakemea kwa upole. aliwakemea kwa ukali
kwahiyo anaweza kuingia mpaka hapa JF?🐒
 
Ulichagua mwenyewe kuwa chawa sasa ni nini kinakuuma
kinachoniuma zaidi nashindwa kabisaa kupata mihemko na ghadhabu ili nami niweze kuporomosha matusi na kutukana kama wewe gentleman ?🐒
 
Watu wana uchungu, huzuni na hasira za maisha magumu wanayoyapitia mitaani, maisha yaliyosababishwa na viongozi uchwara. Mfumuko wa bei, tozo zisizo na vichwa wala miguu, miondombinu dhaifu, kutokuwepo kwa ajira sio upungufu tena. Alafu hapohapo utakuta viongozi husika hata habari hawana wala kuonesha kujali au at least kuongelea hali halisi ya maisha ya Mtanzania wa kawaida.

Utakuta wanaongelea maswala ya kipuuzi na kutoa matamko ya ajabuajabu. Mara asilimia ya vyoo imepanda. Au utasikia mchezaji fulani kapewa million 20 kisa tu katupia mpira kwenye neti ya kamba au timu fulani imehaidiwa million 50 kwa kila goli. Alafu utakuta msomi mwenye degree yupo nyumbani mwaka wa 7 hana ajira. Lakini yule mkimbiaji uwanjani kapewa 20 million na kiongozi mkubwa wa nchi kwa kodi za wananchi. Msomi anajiuliza kwa lipi? Anakosa majibu, kilichobaki ni mvua ya matusi.

Mimi nina hasira na hili liserikali sababu mpaka leo hawajaruhusu PayPal itumike Tanzania. Vijana tunashindwa kutumia fursa za kimataifa ipasavyo. Kama nyie mtakula vya nchi, sawa. Basi tuachieni na sisi tutafute vya nje. But no, tunafungiwa humu ndani. Goddamnit!!!


Watu wanatukana watu wenye hoja za kipuuzi sababu hazileti maana, faida wala mabadiliko yoyote at the end. They don't care anymore. So be it. Fuk everybody.
 
tuelekezane ndrugo nzango, kweli mihemko mnafurahia wennyewe tu, hii si sawa hata kidogo aise [emoji205]
Pole ila nina ushauri kidogo,kama we ni mtu wa kujaa,achana na uchawa.Jifunze kwa ndumila kuwili yohana mbatizaji
 
dah,
Gentleman? 🤭
Umeulizwa swali, kama mleta mada unatakiwa ujibu sio kujichekesha tu mkuu. Kuleta mada ni lazima uwe na ngozi ngumu, uwe na uwezo wa kujibu hoja za watu, sasa ukijichekesha ovyo wakato umeleta mada nzuri ya kujadiliwa hatukuelewi.

Umeulizwa, kijana ameona mmoja wa waliopewa dhamana amekutwa na 7B fedha za walipa kodi, baada ya hayo hakuna hatua zozote za kisheria anazochukuliwa, unataka huyo kijana afanye nini? Achekecheke kama wewe? Akae kimya? Apaze sauti kwa namna gani ili asikike?
 
Back
Top Bottom