Ghana wamefikia default; IMF wamesema watawadhamini. Je, tupo salama kiuchumi huko tuendako?

Waturuhusu wazungu watutawale sema wasije kutufanya watumwa. Yaani hizi afrika countries ziwe states zao tu jamani pia kuwe na free movement, afrika bado umasikini upo Sana. Yaani kidogo ukipata kahela hata $100k huna benki kitambi umeota huku dogo wa fb, Elon musk , Jeff benzos,jack na Wana billions of dollars Ila kitambi hawana wanawaza how to make the Earth to be the best planet. Mie napiga kura kuwa afrika itawaliwe tena
 
Hakuna hard days kwa tanzania hata siku moja, mh. Anakopa kwa kasi kwa wakati huu ili kumaliza miradi iliyoanzishwa jana, kwani muanzishaji alikuwa ameitimiliza kwa asilimia 15-25 tu, tukumbuke miradi ilikuwa ni mingi iliyoanzishwa kwa mkupuo, na isiyowezekana kusitishwa kwa aina ya mikataba yake ambayo mingi ilikuwa migumu kweli baadhi ikiwa ni mwiko kuchelewesha malipo mara baada ya invoice kutolewa, ukichelewesha inakula mazima, point tunakopa tuikamilishe, kazi ibakie kulipa na shughuli za kimaendeleo kwanza without launching heavy projects, which is good too!, uzuri tutakuwa na grace period nzuri sana kulipa, times will comes our nation will breath well.
#Stay tune, kuna akili kubwa zinafanya kazi awamu ya sita.
::Jamaa yao alikopa kweli kwa miradi hii, sisi tunakopa tukamilishe inakuwa nongwa!
 
"Economic mismanagement" ni tatizo kubwa sana kwa nchi maskini. Kwa kuwa maamuzi mengi ya kiuchumi hufanywa na wanasiasa uchwara ambao hawana maono sahihi wala dira makini katika masuala ya "macro & micro economics".

Mathalani, mijadala bungeni kuhusu hali halisi ya kiuchumi hapa nchini, mikakati endelevu ya kuinua "aggregate economy" na hata mipango ya muda mrefu na mfupi huwa inakosa umakini na pia inajadiliwa kisiasa zaidi.

Wachumi wengi wabobezi wamegeuka kusa wanasiasa wachumia tumbo. Badala kusimama imara katika nafasi zao kama washauri wa kiuchumi, wamebaki kumsifia Rais na kuipongeza serikali hata pale inapokuwa ikifanya makosa.
 
kilimo cha biashara under government control to boost state economy.

Serikali ikihusika rasmi kwenye hiyo biashara itawekewa vikwazo na uchumi utakwama kama Afghanistan. Serikali ikiiwaachia cartels waendeshe hiyo biashara nchi itavurugika kama unavyoona Mexico au Colombia ilivyokuwa.
 
Tukisema hapa tunaishia kuitwa Sukuma Gang au washamba.

Watu wanasifia mikopo as if kukopa ni ushujaa na uzalendo uliotukuka.

Time Will Tell....
 
Tukisema hapa tunaishia kuitwa Sukuma Gang au washamba.

Watu wanasifia mikopo as if kukopa ni ushujaa na uzalendo uliotukuka.

Time Will Tell....
Loan for special reason!, and target na sio kipuuzi puuzi tu.
 
Kwa taarifa fupi ni hivi these are the failed states , nyingine nyingi zipo mbioni na Tz ikiwemo .
 
Ukiangalia trend ya deni kuongezeka na percent ya bajeti inayotumika kipa deni , ni suala la muda tu kabla hatujafika kwenye default au kutumia mapato karibu yote kulipia mishahara na .madeni tu. Hakuna fungamano la uongezekaji wa tija kutokana na mikopo inayokopwa hivyo uwezekano wa uwezo wa kiuchumi kuongezeka kutokana na mikopo hiyo( isipokuwa kwenye SGR na bwawa la umeme kana tunakopa ndani maana .abenki ya nje yalikataa) haupo.
 
Source ya taarifa yako ni ipi? Tuwekee link
 

Attachments

  • FB_IMG_1658858827825.jpg
    51.6 KB · Views: 5
Tusikope kwa
Nguvu kubwa izidishwe kwenye miradi mikubwa ,yenywe ndo itakuwa na impact kubwa sana huku mbeleni .Sio kukopa sana kwa vitu vya huduma tu kama sasa.
Tusikope kwa ajili ya elimu,afya,Barbara,reli..tukope kwa ajili ya nini..yaani project gani!?
 
Hizo GDP zao walizipata kwa madeni ya kibiashara kama alivyokuwa anataka kufanya Mwendazake..

Walikurupukia mamiradi makubwa wakati ni Maskini kama tuu alivyofanya Mwendazake..

Kwa hiyo kufa Mwendazake ni nafuu maana unapokopa lazima uwe na rasilimali za kulipa.

Ghana ana mafuta na dhahabu na Kakao lakini amezidiwa na deni kwa sababu ya kukurupukia mamiradi hewa kama huu wa sgr na Bwawa la Nyerere bila kujipima..
 
Tusikope kwa

Tusikope kwa ajili ya elimu,afya,Barbara,reli..tukope kwa ajili ya nini..yaani project gani!?
Angalia kwenye ripoti za BoT, ni bidhaa gani zinatuletea fedha za kigeni kwa wingi na zipi zinachukua fedha za kigeni wingi.
 
Unajua lile genge linampotosha sana Rais Samia. Maana wanamuwekea mitego kibao ili aonekane kashindwa kumanage uchumi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…