Ghana wamefikia default; IMF wamesema watawadhamini. Je, tupo salama kiuchumi huko tuendako?

Hatuwezi kuepuka miradi mikubwa kwa sababu miradi mikubwa ni ya kimkakati. Hata sasa serikali ya A6 imeshasaini makubaliano ya awali kwa ajili ya ujenzi wa mradi mkubwa wa gesi asilia. Nadhani SGR na JNHPP ni cha mtoto kwa huo mradi au unasemaje?
 
Serikali iliyoingia ikaanza kwa kasi kukopa mikopo isiyokwenda kwenye miradi ya uzalishaji. Mikopo kwa ajili ya utoaji wa huduma za jamii.
Hapa ndipo umeharibu kwasababu kuna ushabiki wa kiawamu. Awamu iliyopita ilikopa hadi commercial loans kutoka conventional commercial banks (Credit Suisse Bank). Labda ungetukumbusha ni miradi gani hiyo iloyokuwa ikikopewa hadi commercial loans ambapo kwa sasa haitekelezwi na badala yake pesa zinaenda kwenye kuhudumia Serikali.
Kwa maoni yangu, awamu ya 6 imekuwa very smart na innovative kwenye namna ya kutumia mkopo wa covid-19. Sehemu kubwa wa mkopo huu haukutumika kwenye OC. Pesa zimeenda kwenye miradi ya maji, miradi ya elimu (madarasa), miradi ya afya na miradi ya Kilimo hivyo kwa kiasi flani kuna spillover impact itapatikana. Pesa pia imeenda ku-boost domestic demand (purchasing power), eneo ambalo lilikufa kabisa wakati wa awamu ya 5. Hakuna awamu ambapo kumekuwa na business closure nyingi kama kipindi hicho. Dead demand kwenye uchumi ndio tatizo kubwa sana hususan kwa nchi maskini kama Tanzania. No demand means no purchase, means no production means no auxiliary activities zinazotokana na uzalishaji.

Tatizo pekee ambalo naliona ni ukame na vita ya Ukraine ambapo kwa pamoja zitakuwa na fiscal challenge kwenye kuendelea kutoa ruzuku kwa mafuta na kuagiza chakula nje ya nchi.
Nini kifanyieke? Ni dhahiri dunia itakumbwa na baa kubwa la njaa maana Russia na Ukraine pamoja na makubaliano yanayofanyika hawatakuwa katika peak ileile ya uwekezaji. Serikali ingeweka mkazo wa kuendeleza mashamba kwa kutumia ground water. Ingetoa ofa kwa kila mwenye Shamba linaloanzia acre 30 na kuendelea itoe ruzuku ya kumchimbia kisima na kumpa mkopo wa pump za umwagiliaji (other terms and conditions must apply).
Serikali ingeanza kutenga ecomic production zone kwa ajili ya shughuli za kilimo, uvuvi na ufugaji ili kuuza katika masoko mbalimbali ya arabuni, mashariki ya Kati na kusini mwa Afrika.
 
Hatuwezi kuepuka miradi mikubwa kwa sababu miradi mikubwa ni ya kimkakati. Hata sasa serikali ya A6 imeshasaini makubaliano ya awali kwa ajili ya ujenzi wa mradi mkubwa wa gesi asilia. Nadhani SGR na JNHPP ni cha mtoto kwa huo mradi au unasemaje?
Hata huko Ghana waliita hivyo hivyo..

Mradi WA gas , serikali haingizi Pesa ni WA investors..

Shida ya Jiwe ni kukurupuka bila kuja uanze na kipi na kipi kifuate kulingana na uwezo WA Nchi.
 
Unajua lile genge linampotosha sana Rais Samia. Maana wanamuwekea mitego kibao ili aonekane kashindwa kumanage uchumi.
Hivi nyie mnajua Serikali iliyoshindwa kumanage uchumi? Uchumi unaoshindwa unawezaje kuwa na data zinazoongezeka za matumizi ya saruji na vifaa vya ujenzi?
 
Madai yako yanakosa miguu ya kusimamia kwa sababu kuna mikataba ya SGR iliyosainiwa wakati wa awamu ya 6. Je, kama ni mikataba ilikuwa inalazimisha kumalizia, mbona mipya imesainiwa?
 
1. Miradi ya elimu, maji, afya na madarasa itasaidiaje kurudisha foreign currency tulizopokea? Unajua kwenye kuvurugika kwa uchumi hauangalii upatikanaji wa huduma za jamii wala ubora wake?
2. Je, kuna kiasi chochote cha mkopo wa COVID-19 kilichopelekwa kwenye kilimo kama ulivyodai katika hii post?
3. Kuna sehemu nakubaliana na wewe katika aya za mwisho. Nadhani labda umeanza kuchangia kwa mhemko kwa kudhani nimekaa sana kiawamu.
4. Sipo hapa kushindanisha awamu. Awamu haileti ugali mezani kwangu. Uchumi ndio huleta ugali mezani kwangu. Ni muhimu kutajadili na kuangalia kwa mapana mustakabali wa uchumi wetu bila mihemko ya kisiasa hasa katika eneo la uzalishaji na utafutaji wa foreign currency na jinsi tunavyozitumia.
5. Kwa karne hii kuanguka kwa uchumi sana sana hutokana na nchi kukosa fedha za kigeni au kuwa na matumizi ya fedha za kigeni kuliko uwezo wake na mwisho kukosa kabisa. Hii ni kwa sababu kuagiza kitu kutoka nje kwa sasa ni lazima kutokana na nchi nyingi, TZ ikiwepo kutojitosheleza pakubwa katika uzalishaji lkn pia na maswala ya globalization.
Madeni ya eneo mojawapo linalohitaji fedha za kigeni kwa ulazima na ukishindwa kulipa ndio tunaita ume"default" na hivyo hukopesheki tena. Yaani unakosa cha kulipa unachodaiwa na unakosa hata cha kukopa ili hata uendelee kuingiza bidhaa kutoka nje. Nini kitafuta baada ya hapo kama sio economic collapse?
 
Madai yako yanakosa miguu ya kusimamia kwa sababu kuna mikataba ya SGR iliyosainiwa wakati wa awamu ya 6. Je, kama ni mikataba ilikuwa inalazimisha kumalizia, mbona mipya imesainiwa?
Iliyosainiwa awamu ya sita ni ile iliyokuwa inaelekea katika maeneo ya kimkakati katika kutoa mizigo nje ya nchi na yenye gharama nafuu.
Nadhani umenielewa!
 
Exprience yangu kwa nchi za ngambo mf. America nchi yao kimiundo mbinu imekamilika kwa %99,Maji,umeme, barabara, railways na etc, so haina tena budget kwa mambo ya aina hii, labda repairing tu. So budget kwa miradi mikubwa kwa Tz ipo siku itapungua kabisa,mfano baada ya kumaliza hizi project kubwa ni vema taifa likaingia kwenye feeder roads nchi nzima.
Nimesema feeder road kwa sababu za kimkakati, ya kwamba, bila kutanguliza hizi barabara kwanza, ukaweka makazi kwenye kilimo zaidi, matokeo wananchi watalima sana n then washindwe kufikisha mazao yao sokoni yaharibikie shambani that nonsense, feeder road zikamilike halafu heavy energy iwekwe kwenye kilimo.
 
1. (a)Elimu ni knowledge build up hivyo huongeza tija katika uzalishaji. Lakini katika elimu haikupelkwa pesa za uviko kwa ajili ya kuiendesha shule bali zimapelekwa pesa kujenga infrastructure za elimu, so hapa hakuna components za "social" kama unavyoona wewe. Kupitia ujenzi kuna production imefanyika, saruji, bati, mbao nk.
(b) maji ni hivyohivyo, jamii yenye maji safi na salama huifanya jamii hiyo iwe productive. Lakini pia kama ilivyo kwenye elimu, pesa zilizoenda kwenye maji hazikwenda kulipia bill za maji, zimeenda kujenga MIUNDOMBINU ya maji. Kupitia humo kuna pesa zimeenda kwenye pipes, mashines na other capital goods.
(c ) kwenye afya pia hazikwenda kulipia bill za wagonjwa au kufanya semina kwa madaktari. Zimeenda kujenga MIUNDOMBINU ya afya na mashine za kisasa za afya. Hurahisisha afya ya wananchi ili wakafanye uzalishaji lakini pia kwa kujenga vituo vya afya kuna uzalishaji umeongezeka.
2. Jawabu ndiyo. Sehemu ya pesa za covid zimeagiza mitambo ya kuchimba mabwawa kwa ajili ya mifugo na umwagiliaji wa mazao na visima kwa ajili ya maji na umwagiliaji pia. Sichangii kwa mihemko cause sina private interest na yeyote.
5. Hapo nakubaliana na wewe. Ndio maana nikasema kuna haja ya kubadilisha mfumo wa kilimo kutoka cha seasonal production to mass production ili tuuze bidhaa misimu yote.
Uchumi bora kabisa ni uchumi wa viwanda/manufacturing lakini huu uchumi na zaidi ya kusema uchumi wa viwanda kama tunavyosema. Kwanini? Kwasababu import substitution may not work in today's economic environment. Degree of economic dependants ziko juu sana na duni sio closed tena. Nchi zinategemeana kwenye malighafi, mitambo, masoko, labor, technology nk. Msingi mkubwa wa uchumi wa sasa ni ushindani (competitiveness)- reduce production cost kufanya bidhaa zako ziwe of quality and cheaper. Hapa ndipo unaona China's products are everywhere. Kuna mengi muda hautoshi.
 
Excellent!! Tukijumlisha A.I,katika uzalishaji na uendeshaji mitambo ili kuendana na kasi ya dunia na katika kuhakikisha unapata faida.
 
Excellent!! Tukijumlisha A.I,katika uzalishaji na uendeshaji mitambo ili kuendana na kasi ya dunia na katika kuhakikisha unapata faida.
Very true, pasipo kuweka misingi na ujuzi wa kuzalisha kisasa nothing tangible will take off. Na tukiendelea na akili za maprofesa wetu huko vyuoni za kujisifu wanafunzi aliowapa supplementary badala ya aliowapa ujuzi huenda tukaendelea kulaumu viongozi tu lakini ukweli ni kwamba shida ipo everywhere.
 
Sisi Tanzania tuliweza kuvuka salama wakati wa "lockdown" duniani kwa ukakamavu na ushujaa wa serikali iliyokuwa madarakani.
Hapana. Hii ni sababu ya hovyo. Siyo Ghana pekee walioweka "lockdown"

Kutakuwa na sababu nyingi kadhaa zilizofanya Ghana ikie hapo ilipofikia.

Ghana, si wanayo mafuta, dhahabu, cacao, n.k.? Inakuwaje wanakuwa hoi kiasi hiki?

Kuna mambo kadhaa hayako sawa!

Majirani zetu hapo Kaskazini, wao wanasemaje, bado wanadunda?

Hawa vipenzi wa WB na IMF. haya mashirika yatakuwa na kazi kubwa miaka hii.

Na mikopo ya kiChina nayo wataidhamini? Ngoja tusubiri kuona.
 
Lakini nchi nyingi wamesema hali mbaya za uchumi zimesababishwa na "lockdown". Sio Ghana tu.
Na sababu zinaeleweka kwa sababu covid-19 ilipunguza flow of foreign curencies into many countries.
 
Walamba asali wa pale SALAMANDER awatakakuelewa kabisa
 
Lakini nchi nyingi wamesema hali mbaya za uchumi zimesababishwa na "lockdown". Sio Ghana tu.
Na sababu zinaeleweka kwa sababu covid-19 ilipunguza flow of foreign curencies into many countries.
Mkuu, COVID itakuwa imechangia kwenye matatizo mengine yaliyokuwepo.
 
Sababu zako kwenye 1(a), (b) na (c) ni minor sana na haziwezi kutuokoa popote. Hayo ni maeneo ambayo tunayaweza na hayahitaji kuyakopea. Ungeniambia kuna mradi mkubwa wa maji kama ule wa Arusha au ule wa Shinyanga miaka ile ya mwisho wa utawala wa Ben Mkapa uliotoa maji kutoka ziwa Victoria, basi ningekuelewa. Nitajie mradi mmoja wa maji uliojengwa au ulioanzishwa kwa mkopo ule wa 1. 3T. Kwa upande wa elimu ungesema kuna chuo kikuu tumejenga,basi ningekubali kidogo lakini pia miradi kama hiyo haiwezi kuokoa uchumi wa nchi. Watafaidika wazabuni, baada ya hapo, hadithi inaisha.
Kwa sehemu zingine na michango yako mingine juu ya uzalishaji, nakubaliana nayo.
 
Watu wengi wapumbavu hawapendi mambo ya Msingi na ndio wanaotuongoza,wenye akili hawapewi nafasi na wapumbavu hivyo unaweza ukaona danadana zilizopo ni ujinga ujinga na mizaha kwenye maisha ya watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…