Gharama kufuru za matibabu hospitali za umma ni kwa uhalali upi?

Gharama kufuru za matibabu hospitali za umma ni kwa uhalali upi?

Kwani Kwa hesabu zako mgonjwa anatumia kiasi gani cha umeme hospitalini?

Kwanini kama hivyo hIzi hospitali zisiondelewe kuwa ni za umma angalau zikawa zenu ikaeleweka?
Kasome water and electricity requirements per facility level by WHO Standards.
 
Bei kwa item kwa consumables zote za mgonjwa mmoja wa dialysis ziko wapi tujiridhishe ndugu?
Hivi anaetakiwa kuleta ushahidi ni mshitaki au mshitakiwa ili kushawishi mahakama?

Maana haya mambo tulizunhumzia tangu asubuhi bado unayarudia tu?
 
Kasome water and electricity requirements per facility level by WHO Standards.
Hapana ndugu tofautisha hospitali ya umma na private.

Kwa hakika wizara hii inahitaji a very comprehensive audit.

Kumbe mnadhani hospitali hIzi ni zenu.

Kumbe bajeti ya matumizi ya kila mwaka ni ya nini?
 
Bei kwa item kwa consumables zote za mgonjwa mmoja wa dialysis ziko wapi tujiridhishe ndugu?
Fanya reserch yako njoo na data. Nenda vituo vya dialysis Gov vs Private na oversees njoo na data. Compare and contrast then sema hii ni ghali mno. Bila hivyo huna base ya kuuelezea ughali wowote.
 
Hivi anaetakiwa kuleta ushahidi ni mshitaki au mshitakiwa ili kushawishi mahakama?

Maana haya mambo tulizunhumzia tangu asubuhi bado unayarudia tu?
Kwani umeona kuna kesi? Mshitaki na mshitakiwa wanatoka wapi basi?

Kwanini mnaona kuulizwa itemization na gharama zake kwa mgonjwa ni kuwa mko kizimbani?

Wenye machine hIzi si ninyi? Kwanini tokea asubuhi kushindwa kutoa bei hizo Ili nasi kama wateja tujiridhishe?
 
Hapana ndugu tofautisha hospitali ya umma na private.

Kwa hakika wizara hii inahitaji a very comprehensive audit.

Kumbe mnadhani hospitali hIzi ni zenu.

Kumbe bajeti ya matumizi ya kila mwaka ni ya nini?
Tulishasema bajeti si 100% coverage.
Inaacha makusanyo ya tasisi husika tofauti kulingana na uchumi wa sehemu husika kiuwezo. Kama ingekuwa 100% kusingekuwa na maneno COST SHARING.
 
Kwani umeona kuna kesi? Mshitaki na mshitakiwa wanatoka wapi basi?

Kwanini mnaona kuulizwa itemization na gharama zake kwa mgonjwa ni kuwa mko kizimbani?

Wenye machine hIzi si ninyi? Kwanini tokea asubuhi kushindwa kutoa bei hizo Ili nasi kama wateja tujiridhishe?
Unaogopa kizimba, hii ni mahakama huru leta ushahidi wa gharama kufuru. Kufuru ukilinganisha na nini vs wapi?
 
Wanaanza kuumbuka 7,500 manzese huduma binafsi, 24,000 Muhimbili hospitali ya walalahoi....
Kabla ya kujua hizo cost, kwanza ni kujua unazungumzia Enalapril ipi na ya wapi?

Mbona hata Co-amoxyclav zinatofautiana ndani ya duka moja?
 
Tz hii kila kitu ni hovyo kuanzia viongozi wa ngazi za juu hadi wataalamu wa ngazi za chini.

Mfano unapeleka mtu hospitali kufanya operation madaktar wanakosea operation wanatengeneza tatizo jingine kubwa nnje na tatizo ulilo endea mwanzo hapohapo wanataka tena ugharamikie tatizo walilo lisababisha wao.

Tumbi na mlongazila tunawaZoom tu nyie madaktari wa hizo hospitali ni watu wa hovyo sana wanauwa watu,mnatia watu umaskini,mnawapa watu misongo ya mawazo
Kukosea kupo nawe si mkamilifu. Na kuna aina ya makosa kwa mtaalamu kwa mazingira yake na adhabu.

Soma medical errors misconduct in healthcare setting worldwide.

Labda kama wewe u-mkamilifu.
 
Fanya reserch yako njoo na data. Nenda vituo vya dialysis Gov vs Private na oversees njoo na data. Compare and contrast then sema hii ni ghali mno. Bila hivyo huna base ya kuuelezea ughali wowote.
Siyo dialysis tu. Tuna na MRI, CT scan, Ventilator, ICU, operation nk. List ni ndefu.

Kulikoni kutokutoa ushirikiano tukajiridhisha kama bei ni halali?

Huo sI ndiyo uliokuwa msingi wa hoja?
 
Unaogopa kizimba, hii ni mahakama huru leta ushahidi wa gharama kufuru. Kufuru ukilinganisha na nini vs wapi?

Niogope kizimba Kwa kosa lipi? Nakuona mwogopa kizimba ni wewe. Au ni yale ya "the quilty are always afraid?"

Isikupe taabu tumedhamiria kweli kweli suala hili ni la dharura zaidi.

Dhana yenu ya kuitumia bima ya afya kama conduit yenu ya kutuibia lazima na at any cost kieleweke.

Watu gani msiokuwa na utu nyie?
 
Siyo dialysis tu. Tuna na MRI, CT scan, Ventilator, ICU, operation nk. List ni ndefu.

Kulikoni kutokutoa ushirikiano tukajiridhisha kama bei ni halali?

Huo sI ndiyo uliokuwa msingi wa hoja?
Fanyia kazi zote, ongeza wigo wa utafiti pia malipo kwa wafanyakazi na uwepo wa vitendea kazi. Itasaidia sana.
 
Kukosea kupo nawe si mkamilifu. Na kuna aina ya makosa kwa mtaalamu kwa mazingira yake na adhabu.

Soma medical errors misconduct in healthcare setting worldwide.

Labda kama wewe u-mkamilifu.
Sasa nani agharamie hiyo errors ?

Kama umnakiri huwa mnakosea kwanini mnabebesha gharama zisizo tuhusu?
 
Niogope kizimba Kwa kosa lipi? Nakuona mwogopa kizimba ni wewe. Au ni yale ya "the quilty are always afraid?"

Isikupe taabu tumedhamiria kweli kweli suala hili ni la dharura zaidi.

Dhana yenu ya kuitumia bima ya afya kama conduit yenu ya kutuibia lazima na at any cost kieleweke.

Watu gani nyie msiokuwa na utu nyie?
Hilo liache, kwani wao wana utaratibu wao wa kujiridhisha dhidi ya wanacholipa hiyo ni isdue nyingine. Na sasa kwa hospitali kubwa wana online system ambayo inawasaidia sana mambo yao mengi. Usilichukue hilo jukukumu. Maliza hili la leo kwanza.
 
Fanyia kazi zote, ongeza wigo wa utafiti pia malipo kwa wafanyakazi na uwepo wa vitendea kazi.

Malipo ya wafanyakazi siyo mjomba? Si tulikubaliana cost sharing iwe kwenye consumables na kama pia hizo bajeti tokea kwenye raslimali za taifa kweli hazitoshi?

Kumbe wenzetu wagonjwa na marehemu ni bidhaa? Mnaangalia mapato yenu binafsi kwa wagonjwa na marehemu wakati mishahara mnalipwa na SerIkali?

Kwani salary scales zenu ni kutoka kwa wagonjwa au kutoka serikalini?

Mbona makubwa?
 
Mjadara mzuri huu.

Tips.
1.Wananchi/clients wanahitaji mchanganuo wa huduma na gharama zake.
2.Kuna concept kwa wananchi kuwa hospital na vituo vya Afya vya umma vinaendeshwa na Govt 100%..... kwa hili inabidi watu waelewe kuwa si kweli kuwa Govt inagharimia 100% cost za uendeshaji ... kuna percentage imeachwa kwa mtumiaji kuchangia. Na jukumu la kupanga bei limekaimishwa kwa bodi za uendeshaji wa vituo/hospital so wao ndio wanapanga bei ya hudumu ambazo mgonjwa atachajiwa ili ku-compliment kiasi kilichotolewa na serikali ili kukamilisha mzunguko mzima wa matibabu... hapa utakutana na pesa ya kufungua file, kitanda n. k

3.kuna baadhi ya gharama za uendeshaji zinategemea mapato ya kituo/hospital chenyewe eg. umeme, maji, posho za overtime na extra duty, on call allowances , Ulinzi, Usafi ...hapa si ajabu kituo cha kawaida kabisa kinahitaji 60M ku-cover hizo cost, so watu waelewe tanesco na mamlaka za maji zinatoza pesa as usual.

4.kuhusu itemization.. hili liko kwenye miongozo/maandishi kama wao wanavyopenda kusema .. BUT nani ana muda wa kuanza kumfafanulia clients item moja moja ...so huduma zimekuwa fixed kwenye mfumo wa package ... na kila package na bei yake(boards za uendeshaji ndo wazee wa shoo hizi).

5.Kuhusu Gharama kuwa juu ... inabidi tufanye comperative ... unasema gharama iko juu ukilinganisha na wapi? kwa ukanda wetu sisi ndio tunatoa huduma cheap sana.... kama refference point ni uchumi wa watumiaji (mimi nikiwemo) hapo huwezi kuturidhisha wotee.

WHO IS RESPONSIBLE.

again .. mwananchi eg mwanzilishi wa maada anatakiwa aihoji mamlaka(mhimili uliojichimbia zaidi) kuhusu gharama hizi na itemazation.

CRAZY OPINION FROM MY COLLEGUE.
Turudi sera ya nyuma kidogo ... huduma za Afya na Elimu ziachiwe Govt tuuu na ziwe buree ... private sector abakie huko kwingine ... hii haitatuhitaji BIMA wala mbwembwe nyiingi .. kwanza wahudumu hawatakuwa na choices za kukimbia kimbia mara yuko kituoni kwake muda kidogo yuko private ... hakutakuwa na upotevu wa bidhaa za Afya .. hata akiiba cormodity atapeleka wapi?

Kongole mleta mada .. but kuwa flexible wa Tz hatuko serious hivyo .. tunasubir Afe tukachange msibani at the time hatukuweza kuchangia gharama ya Tiba.
 
Tuambizane ukweli mchungu,gharama za matibabu ni ghali kwa sababu uendeshaji ni gharama na sera yetu ni cost sharing..suluhu pekee ni bima ya afya inasaidia kidogo
 
Sasa nani agharamie hiyo errors ?

Kama umnakiri huwa mnakosea kwanini mnabebesha gharama zisizo tuhusu?
Kasome vizuri Conset form uliyosaini ina mambo mengi ya msingi.

Pia nimesema kuna aina na kiasi cha makosa na adhabu. Suala lilikuwa ni kuwasilisha tatizo la msingi na kushughulikiwa kulingana na shida halisi.

Huku hatuna details, ila makosa yapo. Kama hukuridhika nenda ngazi ya juu.
 
unajua nauli ya kutoka mbezi ubungo kwa mwendo kasi ni sh elfu moja na something, wakati daladala ni mia tano mpaka mia nne unafika? We unaishi dar kweli?

Kuusu gharama za hospitali unajua bei ya panado kwenye hospitali za serikali ni kubwa kuliko phamacy za mtaani? Ndio maana tunauliza kwa nini hospitali za serikali gharama ni kubwa hi hali majengo , mishahara, madawa nk wananchi tunatoa kupitia kodi zetu?
Hospitali Kuna Panadol??

Au unaongelea Paracetamol?
Kama unaongelea Paracetamol, Hospitali kidonge ni Tsh 20, pharmacy ni Bei gani?
 
Hilo liache, kwani wao wana utaratibu wao wa kujiridhisha dhidi ya wanacholipa hiyo ni isdue nyingine. Na sasa kwa hospitali kubwa wana online system ambayo inawasaidia sana mambo yao mengi. Usilichukue hilo jukukumu. Maliza hili la leo kwanza.
Dharura ni wizi kwenye malipo haya hayo hayapaswi kusubiri.

Tutahitaji kupata break down ya malipo haya.

Tunafahamu ni nia yenu tusijue break down hIzi. Kumbe ni kwa sababu ya maslahi binafsi.

Manesi 20 registrars 8 health attendants 4 ... Ili mhalalishe bei kubwa siyo? Mbona hatuwaoni hao kwenye sessions hIzi za dialysis?

Staff hewa ...

Mwogopeni japo mola basi? Watanzania hawa huko vijijini na hata mijini ni maskini mno!
 
Back
Top Bottom