Gharama kufuru za matibabu hospitali za umma ni kwa uhalali upi?

Gharama kufuru za matibabu hospitali za umma ni kwa uhalali upi?

Ninafurahi kusikia ukweli kuwa mashine za zipo na wafanyakazi wa umma wapo na bajeti ya serikali ipo Kwa maana kuwa minus consumables gharama A dialysis zilipaswa kuwa bure.

Hapa sasa ndipo palitakiwa uwepo wa uzalendo kujua bei gani na kipi kinachopungua kwa mgonjwa mmoja mmoja Ili hiyo kuwa sehemu halali ya mchango wake. Ikawa zero kama haihitajiki au 5/- kama ndicho kinachopungua.

Hamuoni aibu kuibia wagonjwa au marehemu?
Kakutisha tu na hiyo orodha yenye items nyingi, havina hiyo bei anayotaka kuaminisha hapa.
 
Ilikuwa muhimu mambo yote yakawekwa wazi. Tusiongee kama tusioelimika.

Tunalinganisha vipi na wapi ambapo:

1. Kwetu investment cost yote ni umma?
2. Kwetu kuna mgao wa bajeti toka kwa umma Kila mwaka?

Unataka tulinganishe na ambao uwekezaji wao ni binafsi 100%?

Tuwe serious kidogo basi.

Anyway hoja hapa ni hii:

"Kupata breakdown ya gharama halisi mfano za dialysis 1, MRI 1, CT Scan 1, operation 1 nk, Ili kujiridhisha na bei hizi ambazo kwa hakika ni kubwa sana kwa mtu au hata kwa bima."

Ni hayo tu ndugu.
Una uhakika kwamba kila kitu ni gvt,upo kwenye Afya ukajua mambo yalivyo au unazungumza tu...unafahamu kwamba zamani matibabu ilikua bure na sasa kuna cost sharing?...punguza kuandika kitu usichokijua,...tatizo letu wa Tz tunapenda kujifanya wajuaji wa kila kitu....kata bima nenda katibiwe...mtu anafika hospital anaanza kusumbua wahudumu kwamba gvt inachangia kila kitu kwa nn dawa hakuna,sasa huyo dr au nurse unayemuuliza yeye atakujibu nn?nendeni mkapeleke malalamiko kwa viongozi wa juu huko,hao watumishi nao wana maisha magumu tu.
 
That mean its not an automated mathematics. Huwezi kusema ni replica.
Unaelewa maana ya fraction of a replica? Yaani private kama ni bei flani kwenye umma mkachukua a fraction. Kwamba fraction hiyo si lazima iwe constant.

Ndivyo Bei zilivyopatikana hizi? Ndiyo sababu ya huu ujasiri wa kuuliza kwani private hicho huko bei gani?

Ndiyo hivyo mkuu?
 
Uko sahihi, utatuzi wa hii changamoto lipo kwenye sera ya wizara/serikali.
Mfano; hospitali A kwa mwaka huu wa fedha inahitaji bilioni 5 ili iweze kutoa huduma kwa ufanisi/kwa bei nafuu; badala ya kupelekewa bilioni 5 wakapelekewa bilioni 1; hapo patatokea nini?
Kwanini unakimbilia kuona mahitaji ni 5bn/- na wanapewa 1bn/-?

Huyu mbuzi kwenye gunia mbona mnapenda sana kumwuuza muda wote?
 
Una uhakika kwamba kila kitu ni gvt,upo kwenye Afya ukajua mambo yalivyo au unazungumza tu...unafahamu kwamba zamani matibabu ilikua bure na sasa kuna cost sharing?...punguza kuandika kitu usichokijua,...tatizo letu wa Tz tunapenda kujifanya wajuaji wa kila kitu....kata bima nenda katibiwe...mtu anafika hospital anaanza kusumbua wahudumu kwamba gvt inachangia kila kitu kwa nn dawa hakuna,sasa huyo dr au nurse unayemuuliza yeye atakujibu nn?nendeni mkapeleke malalamiko kwa viongozi wa juu huko,hao watumishi nao wana maisha magumu tu.

Wapi namwuliza doctor au nurse ndugu? Ninajua hao wala pesa hizi haziendi kwao ila hao ninao wauliza.

La msingi wangejiunga nami tumkabilibmbaya wetu aliyepanga bei hIzi kama kuku mtaga mayai.

Ninao uhakika kuwa hospitali ya umma:

1. 100% investment cost ni umma.
2. Zinapata budget allocation kutokea katika resources za umma na si kidogo.

Wewe hujui hayo?

Hata umeelewa kinachohojiwa au umekurupuka tu ndugu?
 
Kwanini unakimbilia kuona mahitaji ni 5bn/- na wanapewa 1bn/-?

Huyu mbuzi kwenye gunia mbona mnapenda sana kumwuuza muda wote?
Hospitalini hakuna tatizo; tatizo lipo kwa wale wanaotakiwa kuwapelekea mafungu.
 
Utaikuta MNH, ili ujue gharama zake. Hiyo IV catheter/filter pita dukani uulize kwanza.

Kama huzijui bei zake kwa nini tusiwasubiri wajuzi waje?

Tunakubaliana si halalali bei kuzihusisha mashine wala wafanyakazi kwani hao ni wa umma.

Hata hivyo kuna mashaka ya msingi kuwa bila kuwa na mwakilishi wetu kwenye bei hIzi tunabambikwa sana.

Zingatia tatizo letu ni mchanganuo wa bei hIzi si nani analipa.
 
Kumbuka pia, wao wananunua kwa fedha za kigeni; kwa matumizi ya Tsh. lazima gharama ipande.
 
Hospitalini hakuna tatizo; tatizo lipo kwa wale wanaotakiwa kuwapelekea mafungu.

Ila kumbuka tungemaliza hili la itemization za actual costs Kwa mfano dialysis. Kuna mdau kasema bei pekee inabidi kuwa ni consumables kwani machine, infrastructure na wafanyakazi ni wa umma.

Bila kuweka bei hIzi wazi huoni wagonjwa wabaibiwa?
 
Cost sharing. Zinahitaji fedha kwa ajili ya kujiendesha bila kutegemea ruzuku kutoka mfuko mkuu wa Hazina. Ruzuku inabaki kama sehemu tu ya mapato ya hospitali.
Ndiyo gharama ziwe kubwa hivyo?
 
Kumbuka pia, wao wananunua kwa fedha za kigeni; kwa matumizi ya Tsh. lazima gharama ipande.

Tunaamini hakuna biashara haramu kwenye ofisi ya umma. Ndiyo maana tunauliza actual costs.

Tuuziane mbuzi tukiwa sote tumeridhika.
 
Sidhani kama kuna taasisi inajiamulia gharama bila kuwasilisha kwa kwa umma na wadau kwa ajili ya kutoa maoni Bodi na Waziri mwenye dhamana. Tena gharama hizo zitangazwe kwenye gazeti la serikali na kupewa GN number kama jina na utambuzi. Bila hivyo ni batili na wakishtakiwa hawachomoki.
Umeshawahi kuziona kwenye Gazette au tangazo la maoni ya wadau ?
 
Ila kumbuka tungemaliza hili la itemization za actual costs Kwa mfano dialysis. Kuna mdau kasema bei pekee inabidi kuwa ni consumables kwani machine, infrastructure na wafanyakazi ni wa umma.

Bila kuweka bei hIzi wazi huoni wagonjwa wabaibiwa?
Consumable- zinatumia fedha za kigeni/ gharama itapanda kwa kutumia Tsh.
Wafanyakazi- huwa wanaposho zao, nje na mshahara; itahusishwa kwenye vipimo.
Infrastructure - zinahitaji maji, umeme n.k/ itategmea ni nani anayelipa hizo bill, kama ni hospitali itahusishwa kwenye vipimo.
Kitendea kazi/mashine- matengenezo/ ni nani anatoa fedha ya matengenezo, kama ni hospitali itahusishwa kwenye kipimo n.k
 
Tunaamini hakuna biashara haramu kwenye ofisi ya umma. Ndiyo maana tunauliza actual costs.

Tuuziane mbuzi tukiwa sote tumeridhika.
Ukifuatilia sana, unaweza usipate majibu, kuna baadhi ya maofisi watu wanatoka na posho ya 15m + nje ya mshahara; halafu leo hii unategemea daktari bingwa wa upasuaji aishi kwa mshahara tu.
 
Consumable- zinatumia fedha za kigeni/ gharama itapanda kwa kutumia Tsh.
Wafanyakazi- huwa wanaposho zao, nje na mshahara; itahusishwa kwenye vipimo.
Infrastructure - zinahitaji maji, umeme n.k/ itategmea ni nani anayelipa hizo bill, kama ni hospitali itahusishwa kwenye vipimo.
Kitendea kazi/mashine- matengenezo/ ni nani anatoa fedha ya matengenezo, kama ni hospitali itahusishwa kwenye kipimo n.k
Hayupo anayekataa. Sisi ni nani kusema itemized costs ni zipi?

Ziwekwe zote wazi tujiridhishe kuwa tunacholipa ni halali.

Bei haiwezi kuwa % fraction ya kilichopo kwenye hospitali za binafsi ambako uwekezaji ni 100% private.
 
Kwenye hospital kama zile za mikoa na rufaa kuna kitu kinaitwa HMT(Hospital Mgt Team) hupendekeza na board baada ya kulipwa posho hubariki bila kuangalia maslahi mapana kwa wananchi, upande wa council bei hupangwa na baraza la madiwani
Baraza la madiwani huwa linapanga au huwa linapokea na kupitisha mapendekezo ya bei ?
 
Back
Top Bottom