Gharama kufuru za matibabu hospitali za umma ni kwa uhalali upi?


Staajabu ya Mussa ndugu mrejesho wa wengi waliokwenda India na South Africa Bei huko ni nafuu zaidi na cases za "wrong diagnosis" kutokea nyumbani zimekuwa zikisikika:

Mgonjwa adai fidia TMJ, Hindu Mandal
 
Niliwahi kukutana na situation kama hiyo pale MOI na sikuwahi kupata majibu, Mpaka nililalamika kwa waziri wa afya kupitia page yake ya Twitter niliambulia kujibiwa kuwa nipe details zako ili niufuatilie but mpaka mgonjwa anaruhusiwa sikupata msaada wowote.
 
NHIF wameifanya kichaka cha kupiga pesa kwa hizi hospitali kuweka gharama kubwa za vipimo na matibabu zisizo na uhalisia. Ndo maana ili NHIF iweze kuwa sustainable itabidi wafungue hospitali zao wenyewe....
Mimi huwa najiuliza ikiwa tuu NHIF, ambayo wenye hiyo bima nchi nzima ni wachache, je hii bima ya afya kwa wote ndiyo itawezekana kweli?
 
Bajeti ya Wizara ya afya huwa ni kwa ajili ya kugharimia nini? Lakini kama mleta mada ulivyouliza hizi bei hupangwa kwa kuzingatia vigezo gani?
 
Well said [emoji120] [emoji120]
 
mkuu mada yako ina mashiko sana ila serikali ya ccm inajua jinsi gani inawanyonya wananchi ilo uwezi kuwafundisha, kwanza hawakomi kudhulumu, ili la afya ndio sehemu zao pendwa kuwapiga walalahoi
Huwa najiuliza hypothetically kwamba hivi ingekuwa Bima ya afya kwa wote imefanikiwa je bei za vipimo, madawa na gharama zingine zingekuwa za kawaida mfano kupima malaria elfu 2 au napo ingekuwa zaidi (mara 2 ya bei ya kawaida) kwa sababu ni bima?
 

Waziri katumwa pesa:

Watendaji CCM jukumu la kwanza ni kusifia sifia

Hicho ni kigezo #2 muhimu kutimba kitchen cabinet.
 
Ndio mana kuna ishu ya bima ya Afya ambayo malipo yake ni kidogo lakini ita cover haya mambo yote, leo mtu anapinga 340,000 km malipo ya bima ya Afya Kisha akipewa gharama halisi qnalalaika inakuwaje? Tujifunze
Umeambiwa hapo juu mtu Kalipa bima ya afya 340,000 lakini kaambiwa kipimo cha MRI hakipo kwenye Bima na anatakiwa kulipa cash laki mbili na ushee, sasa anaenda kulipia anaambiwa huyo mgonjwa ana bima (ambayo wahusika wamesema hicho kipimo hakiko covered) hivyo anatakiwa kulipa laki 4 na ushee, yaani mara 2 zaidi ya mtu asiye na bima. Sasa tuambie wewe nini hasa logic behind that? Hivi from that experience next time si mgonjwa ataamua aseme hana bima?? Mbona kwenye elimu ambako serikali imewekeza huduma ya elimu siyo ghali kihivyo? Hatukatai kuchangia gharama lakini hii kitu iwe transparent kwa kila mtu na kwenye mahospitali...
 
Hivi mgonjwa akikaa hospital siku 10 huwezi kumpa bili kuonyesha gharama za kitanda kwa siku, madawa etc?
 
Hii BIMA ya wote unayong'ang'ania bado ni kitendawili kwa sababu kwanza kwa maisha ya watanzania milion 61 ni wangapi wana uwezo wa kulipa let's say laki 3 kwa mwaka ili apate full treatment? Imagine wafanyakazi tuu under NHIF yenye uhakika wa malipo kila mwezi, bado kuna vipimo na dawa utaambiwa havimo kwenye Bima, sasa najiuliza hiyo bima kwa wote itaweza kweli? Ngoja tuone muswaada utakapikuwa sheria.
 
Kuiondoa ccm madarakani sio solution. Solution hapa ni Mfumo wa Bima ya Afya kwa wote ambao utakua mfumo rfiki wa kuhakikisha Matibabu kwa wote yanakua sawa
Bima ya afya kwa wote si ndiyo wanavutana huko bungeni? Tuambie nini kimekwamisha huo muswaada bunge la juzi?
 

Kama unavyowaona hapa:

 
Hana lolote huyu bima ya afya imefilisika kutokana na serikali ya ccm kuchota pesa hovyo hovyo, wanataka kufufua kwa lazima kwa kunyonya wananchi
Bima ya afya kwa wote si ndiyo wanavutana huko bungeni? Tuambie nini kimekwamisha huo muswaada bunge la juzi?
 
Hana lolote huyu bima ya afya imefilisika kutokana na serikali ya ccm kuchota pesa hovyo hovyo, wanataka kufufua kwa lazima kwa kunyonya wananchi

Yaonesha mawaziri na warendaji kuwa na majukumu 2 makuu:

1. Kumsifia sifia mwenyekiti kwa lolote hata kama halina tija.
2. Kufanikisha kuchukua pesa kwa wananchi kwa namna yoyote hata kama ni kwa unyang'anyi.

Uzi huu hapa umejielekeza:

Watendaji CCM jukumu la kwanza ni kusifia sifia
 
Bima ya afya iliyoboreshwa inaweza kulipia magonjwa ya Figo na moyo? NHIF inaweza kufanya kipimo cha MRI? inaweza kufanya Dialysis au kuzibua mishipa ya moyo? Hebu nisaidie tafadhali.
 
Kwanza ni kwa mazingira gani mtanzania wa kawaida ataweza kulipa bima ya afya sh laki tatu? Ile ya elfu 40 tuu huko vijijini imeshindikana sembuse laki tatu? Mwaka jana nilitembelea shule moja ya msingi huko mikoa ya magharibi aisee zaidi ya 70 % ya wanafunzi wako pekupeku, yaani hata zile yebo yebo za buku jero imeshindikana kununuliwa. Jamani huko vijijini watu wako hoi kweli kweli.
 
Kuna mtu hapa dar analipwa sh 3500 kwa siku masaa kumi na mbili kiwandani , piga hesabu kwa mwezi, halafu fanya Kama unatoa kwa laki tatu

Huyu mtu ana familia halafu kapanga, huyu Ni wa mjini Kijiji Ni hali mbaya zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…