Gharama kufuru za matibabu hospitali za umma ni kwa uhalali upi?

Mimi huwa najiuliza ikiwa tuu NHIF, ambayo wenye hiyo bima nchi nzima ni wachache, je hii bima ya afya kwa wote ndiyo itawezekana kweli?
Kwa gharama zinazotozwa kuwa kubwa kuliko uhalisia, unaenda kuleta ufisadi wa kutisha na kuua mfuko au mfuko kushindwa kugharamia matibabu inavyotarajiwa. Inafikia kipindi mnaenda mnaambiwa kipimo hiki hakimo kwenye bima, dawa hii haitolewi na bima, matibabu haya hayatolewi na bima, mnaambiwa mtoe pesa......
 
Ukilazwa siku 10 kwa nini kila siku unalipishwa gharama za daktari, manesi etc halafu mbaya zaidi huko wodini wanaokuwa na wagonjwa ni madaktari wanafunzi, maktari bingwa huwaoni lakini unalipishwa costs zao why?
 
Kama ilivyo sekta zingine pana haja ya hizi bei kuwa kuwa regulated. Watu hawawezi kujipangia tu kiholela hivi. Labda tu kama lengo ni kuwafilisi watu au hiyo mifuko kama inavyojili.
Naunga mkono hoja kuwe na chombo cha ku regulate gharama za mahospitalini kama ilivyo LATRA nk
 
Umeshindwa kuja na justifications unaanza kuita watu pimbi. Na hili ni tatizo lingine la wafanyakazi wa serikali, kibri na dharau, kama yule waziri aliyesema wenzake wakajadili hoja za uganga wa kienyeji... Watu kama ninyi unaweza kukuta eti ndiyo mmepewa jukumu la kupanga bei, so ni lazima kuwa na chombo cha kuwa regulate na kuwarudisha kwenye mstari.
 
Mimi nina bili hapa kitanda kwa siku 50,000....
 
Ukilazwa siku 10 kwa nini kila siku unalipishwa gharama za daktari, manesi etc halafu mbaya zaidi huko wodini wanaokuwa na wagonjwa ni madaktari wanafunzi, maktari bingwa huwaoni lakini unalipishwa costs zao why?
Wapi huko?
 
Angalia gharama hizi za bima Ili kuyalipia hayo uliyoorodhesha:

Masharti mapya bima afya yaanza
 
Tuna nchi ya hovyo sana kiuongozi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…