Gharama kufuru za matibabu hospitali za umma ni kwa uhalali upi?

Kwangu hii ni nyuzi bora ya mwaka....achana na mambo yale ya jukwaa letu pendwa la kimasikhara!!
 
Mapendekezo ili gharama ziwe ndogo zinatakiwa kuwa kiasi gani?

Kwa nini isiwe haku bin haki?

Tuangalie nini mchango wa umma kwenye uwekezaji, tuangalie gharama halisi ya uendeshaji tujue Bei ya matumizi.

Kama gharama ni zero na iwe bure, kama ni 1/- na iwe hivyo.

Kuna wasi wasi kuwa gharama zimewekwa kuwa za kufuru kwa vile ni suala la kifo mtu asipofanyiwa dialysis. Hivyo manunda mnaona zitalipwa tu hata kama 100m/-.

Nisiache kusema wizi huu sikubaliani nao iwe mnamwibia mtu moja kwa moja au indirectly kupitia bima.

Bado hujaelewa tu ndugu? A Kwako Bei ni kwenye magunia tu?
 
Anyway, Mimi sijui Kama Bei ni kubwa ama ndogo ila kwa uzoefu wangu vituo vya serikali vya Afya Pamoja na hizo gharama bado ni tegemezi wa fedha za wafadhili (Basket Fund ).

Unakuta kituo kina budget ya mwaka labda milioni 40.

Nusu ya hiyo pesa ununue Dawa na vitendanishi.

Pesa inayobaki ulipe vibarua wa usafi, mortuary attendant, Mlinzi na sometimes Mhasibu kea mwaka mzima.

Hujalipa Calls za madaktari, uniform za Wauguzi, Outreach programs, extra duty.

Unabaki na Nini hapo?

Hapo hujalipa pesa ya Mafuta ya Ambulance, na matengenezo, ujenzi na vifaa ( furniture, electronic devices, Data )
 

Mteja analindwa na mamlaka fulani mfano EWURA, LATRA nk ambako tunaaminishwa bei elekezi hutegemea vikokotoo kadha wa kadha.

Haikushangazi kuwa huku ni ule mwendo wa Bashe na bei za vyakula vya wakulima tu? Kwamba kama vipi tuanzishe hospitali zetu?

Kwanini gharama halisi zisizingatiwe badala ya maneno yako matupu yasiyovunja mfupa?
 
Kwani Bei za Hospitali zinapangwa na mtu yeyote?


Si ni serikali hiyo hiyo ndio inapanga?

Au unamaanisha waoange Bei kwenye Hospitali binafsi?
 
Kwani Bei za Hospitali zinapangwa na mtu yeyote?


Si ni serikali hiyo hiyo ndio inapanga?

Au unamaanisha waoange Bei kwenye Hospitali binafsi?

Kwa gharama hizi mgonjwa huyu bora angekwenda India na labda huko hata angepona:

 
We nae unazingua sasa
Ko kisa dawa za umma zitolewe bure ?
Kisa majengo ya umma yatumike bure ? Utayakarabati wewe?
Maji utalipia bure ?!
Umeme je ?
Hizo pesa za kulipa wafanyakazi utatoa wapi ? Mind you serikali ndo inalipa mishahara mikubwa kwa bongo

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 
Wapi nimesema hospitali za umma bei ni kubwa kuliko private.

Tatizo ni kuwa bei hizi ni kubwa mno nje ya uhalisia. Zingatia pia bei hIzi hatuna ridhaa nazo na haijulikani ni Kwa vigezo zipi huku kodi na tozo tunalipa.
Huo uhalisia unaupima kwa vigezo gani ? Unaweza leta bill ya huduma moja nikupe ufafanuzi kama inaendana na uhalisia au unatumia hisia tu mkuu

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 
Una uhakika nauli mwendokas ni kubwa kuliko daladala?
Unadhani kwann watu wanapanga folen kwenye mwendokasi kwa nusu saa kama ni gharama kuliko daladala zilizo jaa muda wote

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 
Anakuambia utaje huduma, au bei ya dawa ambayo unaona haina uhalisia wake wew unaleta habari ya bashe

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 
Usipokuwa na Bima kwasasa ni changamoto kubwa,nawashauri kateni Bima hata ya peke yako laki 2 na chenji kidogo itakusaidia kuliko kwenda kavukavu
 

Unayasoma wapi hayo ya bure ewe mbuzi?

 
Ndiyo maana tunataka break down.

Tunavilipia kiasi gani? Malipo hayo yanazingatia mchango wetu kama umma?

Kama unajua tuwekee hapa.

Bila hivyo tuna mashaka tunapigwa Kwa kuuziwa mbuzi kwenye magunia.
Ushawahi lazwa ? Mbna ile final list inakujaga na kila kitu had sindano ulizotumia pale unaandikiwa ulitumia lini na zinacost kiasi gani, achen kutumia hisia ndugu zangu katika Tanzania

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 
Sasa mkuu pvt si lodge hio
Na lodge 25 ni kawaida kabisa

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 

Bei hupangwa na bodi za hospitali husika kwa kuhusisha wadau na kuzingatia uliyoyataja pia levels/daraja la kituo au hospitali husika na hali ya uchumi wa eneo husika.

Ingawa pia ungekuja na mifano ya huduma husika ikiwa na gharama yake na useme hii kwa serikalini level hiyo ni shilingi ngapi na private kwa level hiyo ni shilingi ngapi.

Wakati mwingine twaweza kushituka na limbikizo la gharama bila kujua mgonjwa alikaa/hudumiwa hospitalini kwa muda gani na ni nini kilifanyika kuanzia alipopokelewa mpaka anatoka.

Kuhusu uwazi, kwa kila malipo huja na kinacholipiwa, kama kuna kutokuelewa au kutokukubaliana kuna nafasi ya kutoa hoja ili kuangalia uhalali wa vilivyotajwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…