Bei hupangwa na bodi za hospitali na mteja anawasilishwa na nani? Nani anaangalia maslahi ya mteja kwamba hanyonywi na wajanja?
Kwanini MRI, CT scan, dialysis, operation nk ni bei kubwa hizi tunazozifahamu? Ni dawa, majengo, ujuzi, ugonjwa au ni nini?
Kwanini dialysis kwa mfano kuwa huko kwenye bei zilizopo? Bei zilizopo zimezingatia nini? Kwanini si 5,000/-, 20,000/-, 50,000/-, 100,000/- 1,000,000/-, 10,000,000/- au hata zaidi?
Kwanini siyo haki bin haki?
Tafadhali tambua maswali haya ni ya msingi bila kujali mlipaji ni nani.
Zaidi sana tambua wagonjwa wengi na hasa Muhimbili wanabambikiwa sana kwenye list na hasa dawa.
Siyaandiki haya tokea hewani.
Changamoto Kwa wagonjwa na wanaowauguza zinawaweka kwenye nafasi kubwa ya exploitation.
Zingatia nani analipa ni bima au binafsi siyo suala linaloongelewa hapa.