Gharama kufuru za matibabu hospitali za umma ni kwa uhalali upi?

Gharama kufuru za matibabu hospitali za umma ni kwa uhalali upi?

Mkuu hIzi bei hazitoki Kwa Mungu bali zinapangwa hapa hapa na watu kama sisi.

Kwanini bei hIzi ziwe kubwa hivi kwenye hospitali za umma?

Zingatia kwenye hospitali hizo wadau ni sisi kupitia kodi na tozo mbalimbali.

Wafanyakazi wanalipwa mishahara na serikali na pia Kuna allocation ya bajeti Kila mwaka.

Kwanini ICU ni laki 5 kwa siku Kwa mtu? Kwenye laki 5 tufahamishane kimoja kimoja isiwe mbuzi kwenye gunia.

Huo ndiyo msingi wa hoja mkuu.
Kubwa unalinganisha na nini?

Nenda kaione ICU na mahitaji yake, siyo isolation.
Ni vizuri kuwa tuko.pamoja kwenye kwamba hatupingi bima wala kulipa.

Tunapinga ujanja ujanja.

Mjini wanasema "bongo nyoso."

Panq harufu kubwa ya upigaji.

"Tuungane kuwakataa wahuni. Wahuni SI watu wazuri."

Bahati mbaya wahuni wanaweza kuwa wapo Hadi ikulu.
Ponga wote hao wanatukwamisha sisi wazalendo wa kweli.
 
Bajeti ya matibabu ya 10m/- kwa mwanafamilia kwenye nchi yenye tozo na kodi zote zilizopo nchini haiwezekani.

Hali kadhalika hakuna bima ya Afya itaacha kufilisika Kwa bei hizo.

Zingatia msingi wa hoja:

Bei ni kwa kigezo cha ugonjwa, ujuzi, dawa, vifaa au majengo?

Bila kusahau kuwa wawekezaji kwenye vyote hivyo ni sisi wananchi.

Juzi mwanangu ana bima NHIF lkn nikaambiwa nitoe 250000 kwa ajir ya ctscan aisee kidogo nizimie lkn shukran kwa wanandugu walisapot sana within a minute ilipatikana [emoji1545]
 
Kubwa unalinganisha na nini?

Nenda kaione ICU na mahitaji yake, siyo isolation.

Ponga wote hao wanatukwamisha sisi wazalendo wa kweli.
Si ndiyo maana tunahitaji break down mkuu?

Tunajua ICU Iko kwenye laki 5.

Tutapenda kujua yaliyomo moja moja na vikorombwezo vyake kujua gharama halisi.

Kwani Pana taabu tena hapo?
 
Juzi mwanangu ana bima NHIF lkn nikaambiwa nitoe 250000 kwa ajir ya ctscan aisee kidogo nizimie lkn shukran kwa wanandugu walisapot sana within a minute ilipatikana [emoji1545]

Ndiyo hiii mambo mkuu. Wajanja wanalenga sisi kwa kuchelea vifo wanataka vyote tulivyo navyo.

Pana siku tusipokomaa tutaambiwa bei ni vyote tulivyo navyo tulete.

Tujiulize CT scan consumables ni zipi? Ni umeme?

Mheshimiwa Lukonge mwongozo tafadhali.
 
Si ndiyo maana tunahitaji break down mkuu?

Tunajua ICU Iko kwenye laki 5.

Tutapenda kujua yaliyomo moja moja na vikorombwezo vyake kujua gharama halisi.

Kwani Pana taabu tena hapo?
Nampa tu taarifa kwani kuna kosa. Ai iko kwenye hadidu za rejea?
 
Ndiyo hiii mambo mkuu. Wajanja wanalenga sisi kwa kuchelea vifo wanataka vyote tulivyo navyo.

Pana siku tusipokomaa tutaambiwa bei ni vyote tulivyo navyo tulete.

Tujiulize CT scan consumables ni zipi? Ni umeme?

Mheshimiwa Lukonge mwongozo tafadhali.
Orodhesha tangu unaingia kwenye jengo kwa ajili ya CT mpaka unapata ripoti yako.
 
Nampa tu taarifa kwani kuna kosa. Ai iko kwenye hadidu za rejea?
Iko kwenye hadidu za rejea ila huyo ni mjumbe mpya tuepuke upotoshaji.

Kuna mjumbe alitozwa CT scan 250,000/- kuwa bima yake hailipi. Consumables za CT scan unaweza kutupa japo kamwongozo kidogo?
 
Ndiyo halipi umeme. Upo tu, TANESCO inajiweza itaipatia. Walipoeleza kukatia taasisi za serikali zenye madeni ulifikiri ni taasisi za Ujerumani.
Hospitali ya umma haitakiwi hata kidogo kuuziwa umeme na shirika la umma.
 
Orodhesha tangu unaingia kwenye jengo kwa ajili ya CT mpaka unapata ripoti yako.
Ila tusisahau tunahitaji break down hadi ya component moja moja mfano ventilator, CT scan, MRI nk.

Huko si tumeshatoka mkuu kulikoni kupiga reverse tena?
 
Iko kwenye hadidu za rejea ila huyo ni mjumbe mpya tuepuke upotoshaji.

Kuna mjumbe alitozwa CT scan 250,000/- kuwa bima yake hailipi. Consumables za CT scan unaweza kutupa japo kamwongozo kidogo?
Una pre empty kazi yako.

Kuna tatizo mahali. Usibebe kila kitu jaribu kufanya kazi yako kwanza.

Bima ipi? Ni ya kiasi gani?
Alipewa masharti yoyote/gani kabla ya kuikata?
Ni kituo gani alitaka kupiga CT?
Amewauliza watu wa bima tatizo ni jini?
Namba za msaada ziko nyuma ya kazi yake, je aliambiwaje?

Muruzi mingi hii.
 
Zingatia si pre-empty lolote.

Issue si bima gani?

Consumables gani kwenye CT scan?

Hapa ni ka mwongozo tu mkuu. Ile habari kubwa yaja.
 
Bila kusahau bajeti za malipo kama hayo kuna bajeti za uendeshaji tokea bungeni.

Kumtaka mgonjwa tokea dongo beshi kulipia kiyoyozi cha Prof. Janabi ofisini kwake mbona itakuwa kuchekesho cha mwaka ndugu?
 
Yote yatazingatiwa, baada ya kujua gharama unapiga hodi manispaa au wizara ya afya kujua ni kiasi gani hupelekea kule. Mbona mambo yako wazi. Tumjue mchawi wa mwanetu.
 
Back
Top Bottom