DOKEZO Gharama mpya ambazo Aga Khan wanataka walipwe kwa wateja wa NHIF ni kuhujumu nchi. Haikubaliki

DOKEZO Gharama mpya ambazo Aga Khan wanataka walipwe kwa wateja wa NHIF ni kuhujumu nchi. Haikubaliki

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

grOg

Member
Joined
Feb 3, 2023
Posts
22
Reaction score
11
WhatsApp Image 2024-08-14 at 15.51.41.jpeg

Hospitali ya Aga Khan wanataka kutoza Shilingi 6,000,000/= kwa huduma za kujifungua kwa njia ya upasuaji wakati Hospitali nyingine zenye hadhi sawa ya rufaa ya Kanda wanatoza kiasi cha Shilingi 230,000/= huku bei ya juu katika baadhi ya Hospitali ikijumlisha na huduma ziada hutoza kiasi cha Shilingi 600,000/=. Aga Khan wanataka kulipwa maradufu kwa asilimia 100 zaidi kuliko Hospitali nyingine.

Huduma ya kulaza wagonjwa mahututi katika Hospitali ya Aga Khan wanataka kulipwa kiasi cha Shilingi 2,278,933, huduma hii kwenye Hospitali nyingine huwa ni kiasi cha shilingi 500,000/= na Shilingi 700,000/= ambayo ni bei ya juu katika baadhi ya Hospitali ukijumuisha na huduma za ziada.

Aga Khan wanataka kutoza kiasi cha Shilingi 334,546 kwa huduma za uchunguzi kwa kupitia CT-Scan huku Hospitali nyingine zinatoza 120,000 hadi 150,000 ikiwa ni bei ya juu katika baadhi ya Hospitali ukijumuisha na huduma za ziada. Kwanini bei iwe juu hivi? CT-Scan hizi hizi ambazo tumeona Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan amezinunua na sasa huduma zinapatikana nchi nzima kwenye Hospitali zote za Rufaa za Mikoa na nyinginezo ngazi za juu. Najiuliza Gharama zote hizo zinakuja kwa msingi upi?

Hospitali ya Aga Khan inaomba NHIF isitishe mkataba wake wa utoaji wa huduma kwa sababu za kiuendeshaji.

Inastua sana. Hakika inauma sana kuona hospitali hii inalazimisha ilipwe mamilioni ya fedha na NHIF katika utoaji wa huduma zake, bei ambazo hata katika Hospitali nyinginezo tena zilizo ngazi ya juu ya rufaa ya matibabu.

Katika hili kuna madudu mengi ambayo Aga Khan inataka kuibebesha Serikali mzigo wa kuongeza gharama zaidi za huduma kwa wateja wa NHIF kuliko kiwango cha juu kabisa cha malipo kwa huduma.

Nitatoa mifano michache ya huduma za kawaida kabisa ambazo Aga Khan imekuwa ikidai kuongezewa gharama hizo kwenye huduma wanazotoa kwa wateja wa NHIF.

Hospitali ya Aga Khan wanataka kutoza Shilingi 6,000,000/= (Milioni sita) kwa huduma za kujifungua kwa njia ya upasuaji wakati Hospitali nyingine zenye hadhi sawa ya rufaa ya Kanda wanatoza kiasi cha Shilingi 230,000/= huku bei ya juu katika baadhi ya Hospitali ikijumlisha na huduma ziada hutoza kiasi cha Shilingi 600,000/=. Aga Khan wanataka kulipwa maradufu kwa asilimia 100 zaidi kuliko Hospitali nyingine.

Huduma ya kulaza wagonjwa mahututi katika Hospitali ya Aga Khan wanataka kulipwa kiasi cha Shilingi 2,278,933, (zaidi ya Milioni Mbili) huduma hii kwenye Hospitali nyingine huwa ni kiasi cha shilingi 500,000/= (Laki tano) na Shilingi 700,000/=(Laki saba) ambayo ni bei ya juu katika baadhi ya Hospitali ukijumuisha na huduma za ziada.

Aga Khan wanataka kutoza kiasi cha Shilingi 334,546 (Zaidi ya Laki tatu) kwa huduma za uchunguzi kwa kupitia CTScan huku Hospitali nyingine zinatoza 120,000 (Laki moja na elfu ishirini) hadi 150,000(Laki moja na nusu) ikiwa ni bei ya juu katika baadhi ya Hospitali ukijumuisha na huduma za ziada.

Kwanini bei iwe juu hivi?

CT-Scan hizi hizi ambazo tumeona Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan amezinunua na sasa huduma zinapatikana nchi nzima kwenye Hospitali zote za Rufaa za Mikoa na nyinginezo ngazi za juu. Najiuliza Gharama zote hizo zinakuja kwa msingi upi?

Ifahamike kuwa Aga Khan sio Hospitali ngazi ya Taifa hivyo bado rufaa zao zote wanalazimika kuzipeleka Hospitali ya Taifa Muhimbili, hata kama ni Hospitali Binafsi ukiweka gharama za juu pamoja na huduma za ziada hawapaswi kuwa na tofauti kubwa ambayo inatishia uhai wa Mfuko.

Kama Taifa ifike mahali tutafakari endapo Aga Khan wana nia kweli ya kutoa huduma za matibabu au la? Je ni wananchi wangapi wataweza kupata huduma kwa gharama hizi katika hospitali hii? Au wamelenga tabaka gani la kulitibia?

Hata hivyo niipongeze sana Serikali kwa hatua kubwa ya kuboresha huduma za matibabu nchini huduma ambazo awali yawezekana zilipatikana nje ya nchi lakini sasa zinapatikana katika hospitali zetu za umma. Kwa hili kongole kwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Viongozi wa na Watendaji wa Wizara ya Afya wakiongozwa na Waziri jembe kabisa Mhe. Ummy Mwalimu.

Ninaamini kwamba katika utoaji wa huduma za matibabu, utu hupaswa kuwa kipaumbele cha kwanza na kuweka maslahi mapana ya kuokoa maisha ya binadamu.

Kwa leo niwaache na tafakari hii ya gharama kubwa zisizo na uzalendo za Aga Khan.

Bei zinazopendekezwa na Aga Khan katika baadhi ya huduma.

Na
Aina ya Huduma
Bei
inayopendekezwa na
Aga Khan
Bei katika
Hospitali zingine
Bei ya juu katika baadhi ya hospitali pamoja na huduma za ziada
1​
Huduma ya Uzazi kwa njia ya upasuaji​
6,000,000​
230,000​
600,000​
2​
Kulazwa chumba cha wagonjwa mahututi​
2,278,933​
500,000​
700,000​
3​
Huduma ya CT-Scan bila dawa ya kuangalia mishipa ya damu​
334,546​
120,000​
150,000​
 
Kwanza Agakani tofauti na kufanya usafi kwenye tiba wana Madaktari Intern wote yaani hamna kitu pale
Ukienda na Mkeo hata kama hana shida ya kujifungua lazima afanyiwe upasuaji ingawa hili limekua janga la nchi nzima hasa miji mikubwa kila mtu kujifungua ni upasuaji ni aibu sana
 
View attachment 3069948Hospitali ya Aga Khan wanataka kutoza Shilingi 6,000,000/= kwa huduma za kujifungua kwa njia ya upasuaji wakati Hospitali nyingine zenye hadhi sawa ya rufaa ya Kanda wanatoza kiasi cha Shilingi 230,000/= huku bei ya juu katika baadhi ya Hospitali ikijumlisha na huduma ziada hutoza kiasi cha Shilingi 600,000/=. Aga Khan wanataka kulipwa maradufu kwa asilimia 100 zaidi kuliko Hospitali nyingine.

Huduma ya kulaza wagonjwa mahututi katika Hospitali ya Aga Khan wanataka kulipwa kiasi cha Shilingi 2,278,933, huduma hii kwenye Hospitali nyingine huwa ni kiasi cha shilingi 500,000/= na Shilingi 700,000/= ambayo ni bei ya juu katika baadhi ya Hospitali ukijumuisha na huduma za ziada.

Aga Khan wanataka kutoza kiasi cha Shilingi 334,546 kwa huduma za uchunguzi kwa kupitia CT-Scan huku Hospitali nyingine zinatoza 120,000 hadi 150,000 ikiwa ni bei ya juu katika baadhi ya Hospitali ukijumuisha na huduma za ziada. Kwanini bei iwe juu hivi? CT-Scan hizi hizi ambazo tumeona Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan amezinunua na sasa huduma zinapatikana nchi nzima kwenye Hospitali zote za Rufaa za Mikoa na nyinginezo ngazi za juu. Najiuliza Gharama zote hizo zinakuja kwa msingi upi?
Kama hizo hospital zingine wanatoa huduma sawasawa na Agakhan si muende huko.
 
Soda kwenye duka la mangi unainywa kwa shilingi 600, soda hiyo hiyo ukitaka kuinywa pale Samaki samaki mlimani City utainywa kwa shilingi 3000, gharama mara tano zaidi. Umeelewa nini?

Kinachoamua bei ya bidhaa au huduma ni Class ya mtoa huduma iliyolenga Class fulani ya wateja.
 
Umelazimishwa, si uende Mwananyamala ama Mloganzila ambapo uwezo wako unaweza.
Inaonekana uelewa wako mdogo. Mteja wa NHIF akienda pale Aga khan au hata Saifee huduma kama ni hiyo ya Uzazi kwa njia ya upasuaji yeye atahudumiwa sawa na yule aliyekuwa Saifee au hata Mbeya. Ishu hapa iko kwa NHIF ambaye analipia huduma ambayo mwanachama wake amepata. Huduma hiyo Aga Khan anataka alipwe 6m wengine kama saifee wanachaji 600k. Na hapo kumbuka Aga khan sio wateja wote wa NHIF wanapokelewa. Hatari na nusu.
 
Ukienda na Mkeo hata kama hana shida ya kujifungua lazima afanyiwe upasuaji ingawa hili limekua janga la nchi nzima hasa miji mikubwa kila mtu kujifungua ni upasuaji ni aibu sana
Sijui shida imetoka wapi, kuna mtu nilimsikia akisema mkewe lazima apasuliwe ili ku maintain flavour🙊
 
Inaonekana uelewa wako mdogo. Mteja wa NHIF akienda pale Aga khan au hata Saifee huduma kama ni hiyo ya Uzazi kwa njia ya upasuaji yeye atahudumiwa sawa na yule aliyekuwa Saifee au hata Mbeya. Ishu hapa iko kwa NHIF ambaye analipia huduma ambayo mwanachama wake amepata. Huduma hiyo Aga Khan anataka alipwe 6m wengine kama saifee wanachaji 600k. Na hapo kumbuka Aga khan sio wateja wote wa NHIF wanapokelewa. Hatari na nusu.
Hiyo hospital ya Agha Khan ilijengwa Kwa ajili ya Wahindi nyie waswahili mnaoishi Manzese Kwa mfuga mbwa mnafata Nini?
 
Kuna mtu anajua bei mpya ya kujifungulia muhimbili?kama hauna ela usiende
 
Back
Top Bottom