DOKEZO Gharama mpya ambazo Aga Khan wanataka walipwe kwa wateja wa NHIF ni kuhujumu nchi. Haikubaliki

DOKEZO Gharama mpya ambazo Aga Khan wanataka walipwe kwa wateja wa NHIF ni kuhujumu nchi. Haikubaliki

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kwenda Agha khan na hauna hela ni kutafutia watu waonekane wabaya tuu...Si kuna Hizi Kairuki, Kitemgule, Bochi na zipo vizuri tuu
Unajua watz wana matatizo ya akili , hao Bochi tu wenyewe wa hapo kimara hawataki kuiona hiyo bima ya NHIF ,anayebisha aende na hiyo takataka ya NHIF pale aone na alete mrejesho hapa
 
Yaani Agha Khan kumejaa wagonjwa malofa kibao mtu anaharisha mbio Agha Khan

Dunia nzima Kuna hotel za VIP,Shule na vyuo vya VIP , Hospital za VIP nk
Huwezi geuza hospital kama ya Agha Khan iwe kama ya serikali Cha wote kutaua quality na status

Bima ndogo waende hospital serikali

Bima zote za NHIF waende hospital za serikali tunakoambiwa Kila siku kuwa huduma zimeboreshwa kuanzia majengo,madaktari na huduma za Afya
Ni Bima tu inawapeleka hapo,Mbona shule watoto wenu mnawapeleka wanakochezaga 😂😂😂😂
 
Hapo kuna wakati fulani mgonjwa wetu alikaa jengo la pavilion
Na alilazwa week 3 huo mkeka ulivyotoka syo poa
Pale waende wenye kibunda,ila all in all mm binafsi napakubali sana muhimbili

Ova
Kweli hapo lazima uwe na kibunda au bima kubwa ,ila kwa sisi mpeche mpeche ,pangu pa kavu hapatufai.

Yes muhimbili kuna vifaa vingi sema inahujumiwa na wala rushwa tu.
 
Propaganda hizi ujue...hiyo hospitali mliyoiingiza ya Saifee, gharama ya uzazi kwa kisu ni tsh 4,000,000

Sasa hiyo tsh 700,000 ni ya wapi?
Kuna mdau amenifungua macho hapo juu, kama kweli Aga Khan wana MoU na serikali, wanafaidi msamaha wa kodi kuliko taasisi nyingine yeyote hapa TZN, basi hawastahili kufanya haya...

Mwenye MoU nao achukue hatua zaidi ya hiyo!
 
Hii ni crisis katika utoaji wa huduma za afya nchi nzima na issue ni kwamba raia wengi ni masikini na hawawezi kumudu gharama za matibabu , wanategemea hivyo visenti vya NHIF (shirika linaloekea kufirisika kutokana na mismanagement ) ,na malipo hayawafikii hao watoa huduma kwa wakati , na matokeo ndio hayo hospitali zinaanza kupunguza vituo vya huduma kama kufunga baadhi ya hospitali na kukataa kupokea wagonjwa wa bima za NHIF .

Sasa spinning ya wanasiasa wa ccm na majitu yasiyokuwa kufanya analysis yanaona kosa ni la watoa huduma ,wakati failure ni ya serikali yenyewe
 
Uko sahihi Kila siku serikali inaimba hospitali za serikali na huduma zake zimeboreshwa waende huko hospital za private waachie wale wa Private sector ndio watumie hizo huduma ambao wengi Wana bima za Afya private sio hizo za NHIF

Wa NHIF serikali iwaambie kabisa kuwa mtatibiwa hospitali za serikali tu

Hizo private hospitals waachane nazo
Hao wenye NIHIF wanaotibiwa aghakhan unawaambia serekali iwaambie unawajua mkuu
 
Unajua watz wana matatizo ya akili , hao Bochi tu wenyewe wa hapo kimara hawataki kuiona hiyo bima ya NHIF ,anayebisha aende na hiyo takataka ya NHIF pale aone na alete mrejesho hapa
Uende ukatibiwe kairuki na takataka yako hiyo ya NHIF ,una wazimu au ?
Suala ni lile lile ufisadi na incompetence ya uendeshaji wa hilo shirika la bima ambalo walikuwa wanakopeshsna bilioni kumi na tano wafanyakazi wa NHIF , ambazo ni ( senti za raia masikini wa Tz ) as if ni saccos
 
Kama huko serikalini tu ambapo wanapata ruzuku kila siku toka wizara , unaenda unaambiwa hii dawa hamna mara sijui upuuzi gani na huduma mbovu ,uchafu ,negligence na kero nyingine .
Jiulize watoa huduma binafsi wemebeba mzigo kiasi gani
 
Kwanza Agakani tofauti na kufanya usafi kwenye tiba wana Madaktari Intern wote yaani hamna kitu pale
Ukienda na Mkeo hata kama hana shida ya kujifungua lazima afanyiwe upasuaji ingawa hili limekua janga la nchi nzima hasa miji mikubwa kila mtu kujifungua ni upasuaji ni aibu sana
Sasa kama Utrasound inaonesha mtoto ni mkubwa, solution ni nini kama sio upasuaji?
Mtu afe ?
 
Hawa wanasiasa wenyewe wakiugua hata malaria hawaendi hospitali za serikali , kama huko ni kuzuri mbona hawaendi ?
 
Cha muhimu serikali iboreshe huduma kwenye hospitali zake. Hayo mabilioni ya kulipa wapuuzi Aga Khan ayatumie kuajiri wafanyakazi wa kutosha mahospitalini. Serikali ikifanya hivyo hao kina Aga Khan na wahuni wengine wataufyata.
 
Mbongo kwa mhindi unafuata nn
Si wahindi tu hata hospitali za binafsi nyingi za wabongo wakikuona na hicho kikadi chako cha NHIF watakufukuza kama mbwa na hautaamini .
Wamechoka na utapeli wa NHIF , watu wamewekeza pesa ndefu kwenye hizo hospitali , sio charity hiyo
 
Hospitali hizo ni private enterprises ni lazima waingize pesa ili kuweza kusustain kutoa huduma
 
View attachment 3069948
Hospitali ya Aga Khan wanataka kutoza Shilingi 6,000,000/= kwa huduma za kujifungua kwa njia ya upasuaji wakati Hospitali nyingine zenye hadhi sawa ya rufaa ya Kanda wanatoza kiasi cha Shilingi 230,000/= huku bei ya juu katika baadhi ya Hospitali ikijumlisha na huduma ziada hutoza kiasi cha Shilingi 600,000/=. Aga Khan wanataka kulipwa maradufu kwa asilimia 100 zaidi kuliko Hospitali nyingine.

Huduma ya kulaza wagonjwa mahututi katika Hospitali ya Aga Khan wanataka kulipwa kiasi cha Shilingi 2,278,933, huduma hii kwenye Hospitali nyingine huwa ni kiasi cha shilingi 500,000/= na Shilingi 700,000/= ambayo ni bei ya juu katika baadhi ya Hospitali ukijumuisha na huduma za ziada.

Aga Khan wanataka kutoza kiasi cha Shilingi 334,546 kwa huduma za uchunguzi kwa kupitia CT-Scan huku Hospitali nyingine zinatoza 120,000 hadi 150,000 ikiwa ni bei ya juu katika baadhi ya Hospitali ukijumuisha na huduma za ziada. Kwanini bei iwe juu hivi? CT-Scan hizi hizi ambazo tumeona Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan amezinunua na sasa huduma zinapatikana nchi nzima kwenye Hospitali zote za Rufaa za Mikoa na nyinginezo ngazi za juu. Najiuliza Gharama zote hizo zinakuja kwa msingi upi?

Hospitali ya Aga Khan inaomba NHIF isitishe mkataba wake wa utoaji wa huduma kwa sababu za kiuendeshaji.

Inastua sana. Hakika inauma sana kuona hospitali hii inalazimisha ilipwe mamilioni ya fedha na NHIF katika utoaji wa huduma zake, bei ambazo hata katika Hospitali nyinginezo tena zilizo ngazi ya juu ya rufaa ya matibabu.

Katika hili kuna madudu mengi ambayo Aga Khan inataka kuibebesha Serikali mzigo wa kuongeza gharama zaidi za huduma kwa wateja wa NHIF kuliko kiwango cha juu kabisa cha malipo kwa huduma.

Nitatoa mifano michache ya huduma za kawaida kabisa ambazo Aga Khan imekuwa ikidai kuongezewa gharama hizo kwenye huduma wanazotoa kwa wateja wa NHIF.

Hospitali ya Aga Khan wanataka kutoza Shilingi 6,000,000/= (Milioni sita) kwa huduma za kujifungua kwa njia ya upasuaji wakati Hospitali nyingine zenye hadhi sawa ya rufaa ya Kanda wanatoza kiasi cha Shilingi 230,000/= huku bei ya juu katika baadhi ya Hospitali ikijumlisha na huduma ziada hutoza kiasi cha Shilingi 600,000/=. Aga Khan wanataka kulipwa maradufu kwa asilimia 100 zaidi kuliko Hospitali nyingine.

Huduma ya kulaza wagonjwa mahututi katika Hospitali ya Aga Khan wanataka kulipwa kiasi cha Shilingi 2,278,933, (zaidi ya Milioni Mbili) huduma hii kwenye Hospitali nyingine huwa ni kiasi cha shilingi 500,000/= (Laki tano) na Shilingi 700,000/=(Laki saba) ambayo ni bei ya juu katika baadhi ya Hospitali ukijumuisha na huduma za ziada.

Aga Khan wanataka kutoza kiasi cha Shilingi 334,546 (Zaidi ya Laki tatu) kwa huduma za uchunguzi kwa kupitia CTScan huku Hospitali nyingine zinatoza 120,000 (Laki moja na elfu ishirini) hadi 150,000(Laki moja na nusu) ikiwa ni bei ya juu katika baadhi ya Hospitali ukijumuisha na huduma za ziada.

Kwanini bei iwe juu hivi?

CT-Scan hizi hizi ambazo tumeona Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan amezinunua na sasa huduma zinapatikana nchi nzima kwenye Hospitali zote za Rufaa za Mikoa na nyinginezo ngazi za juu. Najiuliza Gharama zote hizo zinakuja kwa msingi upi?

Ifahamike kuwa Aga Khan sio Hospitali ngazi ya Taifa hivyo bado rufaa zao zote wanalazimika kuzipeleka Hospitali ya Taifa Muhimbili, hata kama ni Hospitali Binafsi ukiweka gharama za juu pamoja na huduma za ziada hawapaswi kuwa na tofauti kubwa ambayo inatishia uhai wa Mfuko.

Kama Taifa ifike mahali tutafakari endapo Aga Khan wana nia kweli ya kutoa huduma za matibabu au la? Je ni wananchi wangapi wataweza kupata huduma kwa gharama hizi katika hospitali hii? Au wamelenga tabaka gani la kulitibia?

Hata hivyo niipongeze sana Serikali kwa hatua kubwa ya kuboresha huduma za matibabu nchini huduma ambazo awali yawezekana zilipatikana nje ya nchi lakini sasa zinapatikana katika hospitali zetu za umma. Kwa hili kongole kwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Viongozi wa na Watendaji wa Wizara ya Afya wakiongozwa na Waziri jembe kabisa Mhe. Ummy Mwalimu.

Ninaamini kwamba katika utoaji wa huduma za matibabu, utu hupaswa kuwa kipaumbele cha kwanza na kuweka maslahi mapana ya kuokoa maisha ya binadamu.

Kwa leo niwaache na tafakari hii ya gharama kubwa zisizo na uzalendo za Aga Khan.

Bei zinazopendekezwa na Aga Khan katika baadhi ya huduma.

Na
Aina ya Huduma
Bei
inayopendekezwa na
Aga Khan
Bei katika
Hospitali zingine
Bei ya juu katika baadhi ya hospitali pamoja na huduma za ziada
1​
Huduma ya Uzazi kwa njia ya upasuaji​
6,000,000​
230,000​
600,000​
2​
Kulazwa chumba cha wagonjwa mahututi​
2,278,933​
500,000​
700,000​
3​
Huduma ya CT-Scan bila dawa ya kuangalia mishipa ya damu​
334,546​
120,000​
150,000​
Hawa biashara yao kubwa ni upasuaji.
Mzazi pale hatoki bila upasuaji.
Na pia nawachukia kwa sababu walitaka kuua jamaa yangu kwa vipimo vya uongo.
Kumbe ni malaria tu ndio tatizo. Wao walisema hakuna malaria.
 
Back
Top Bottom