View attachment 3069948
Hospitali ya Aga Khan wanataka kutoza Shilingi 6,000,000/= kwa huduma za kujifungua kwa njia ya upasuaji wakati Hospitali nyingine zenye hadhi sawa ya rufaa ya Kanda wanatoza kiasi cha Shilingi 230,000/= huku bei ya juu katika baadhi ya Hospitali ikijumlisha na huduma ziada hutoza kiasi cha Shilingi 600,000/=. Aga Khan wanataka kulipwa maradufu kwa asilimia 100 zaidi kuliko Hospitali nyingine.
Huduma ya kulaza wagonjwa mahututi katika Hospitali ya Aga Khan wanataka kulipwa kiasi cha Shilingi 2,278,933, huduma hii kwenye Hospitali nyingine huwa ni kiasi cha shilingi 500,000/= na Shilingi 700,000/= ambayo ni bei ya juu katika baadhi ya Hospitali ukijumuisha na huduma za ziada.
Aga Khan wanataka kutoza kiasi cha Shilingi 334,546 kwa huduma za uchunguzi kwa kupitia CT-Scan huku Hospitali nyingine zinatoza 120,000 hadi 150,000 ikiwa ni bei ya juu katika baadhi ya Hospitali ukijumuisha na huduma za ziada. Kwanini bei iwe juu hivi? CT-Scan hizi hizi ambazo tumeona Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan amezinunua na sasa huduma zinapatikana nchi nzima kwenye Hospitali zote za Rufaa za Mikoa na nyinginezo ngazi za juu. Najiuliza Gharama zote hizo zinakuja kwa msingi upi?