DOKEZO Gharama mpya ambazo Aga Khan wanataka walipwe kwa wateja wa NHIF ni kuhujumu nchi. Haikubaliki

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Umaskini mbaya sana ndugu yangu
Kabisa, ujue Kuna watu wanalipa cash hawatumii na Wana uwezo wao, hivyo sisi wa Hali ya chini twende hosp za size zetu, kulalamika hakufai Kila 1 anakula urefu wa kamba yake.🤪
 
Mkuu kuna kitu kinaitwa class hata bima za nhif baadhi tu wanaotibiwa pale na wala huwezi kusikia wanalalamika ila wenzangu na mm lazima uone mil 6 nyingi.
 
Dah aisee hatari sana.

Wahindi nao bila shaka wanalipa gharama hizohizo wakienda kutibiwa?
 
View attachment 3069948Hospitali ya Aga Khan wanataka kutoza Shilingi 6,000,000/= kwa huduma za kujifungua kwa njia ya upasuaji wakati Hospitali nyingine zenye hadhi sawa ...
Kwa kifupi mnajipeleka kujichanganya na hawa wahindi lakini hawakutaka muende huko.

Ni hospitali yao na ni kwaajili ya wao matajiri.

Walianza kupokea NHIF majuzi tu lakini wao walikuwa wanpokea Strategies, AAR, VISA BUD na kadi zingine za kimataifa.

Huwezi kuwapangia bei, mnbona hamlalamiki soda pale kempisky inauzwa elfu kumi na tano?

Hospitali ya Aga Khan inamilikiwa na Aga Khan Development Network (AKDN), ambayo ni mtandao wa mashirika yanayoongozwa na Imam Aga Khan, kiongozi wa kiroho wa Waismailia. AKDN inahusisha mashirika kadhaa yanayojihusisha na sekta mbalimbali, ikiwemo afya, elimu, maendeleo ya kiuchumi, na utamaduni, lengo likiwa ni kuboresha hali ya maisha ya watu katika nchi zinazoendelea.

Hospitali ya Aga Khan ni sehemu ya mtandao wa huduma za afya zinazomilikiwa na kuendeshwa na AKDN.
 
Wasifunge hospital tu, wafunge na shule zao waondoke. Agha Khan ni taasisi ambayo inasamehewa kodi nyingi kuliko taasisi nyingine yoyote hapa nchini. Mwanzoni wakiingia MoU na Serikali waliomba wasamehewe kodi ili watoe huduma nafuu kwa Watanzania walio wengi. Mwisho wa siku huduma zimekuwa ghali kuliko mahala pengine popote. Hawa waondoke wala wasisumbue watu.
 
Watu wanapiga hela tu 🤣 nchi ya kitu kidogo
 
Hapo kuna wakati fulani mgonjwa wetu alikaa jengo la pavilion
Na alilazwa week 3 huo mkeka ulivyotoka syo poa
Pale waende wenye kibunda,ila all in all mm binafsi napakubali sana muhimbili

Ova
Hahahah Aga Khan tulimpeleka ndugu alipata ajali ya pikipiki mfupa wa paja ukavunjika baada ya week bili ilikuja 25M yani bahati nzuri jamaa ni staff wa absa tena wa kwenye senior position ofisi ikasimamia show.
 
Wateja gani hawapokelewi Aga Khan?
 
Kwani ni lazima wateja wa NHIF kutibiwa Aga Khan ?
Uko sahihi Kila siku serikali inaimba hospitali za serikali na huduma zake zimeboreshwa waende huko hospital za private waachie wale wa Private sector ndio watumie hizo huduma ambao wengi Wana bima za Afya private sio hizo za NHIF

Wa NHIF serikali iwaambie kabisa kuwa mtatibiwa hospitali za serikali tu

Hizo private hospitals waachane nazo
 
aAgha Khani ni wezi miaka mingi walikuwa hawajashtukiwa tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…