Gharama na taratibu za kufungua sanduku la posta


Yani, Nimesubiri mpaka nimechoka, mwanzoni waliniambia wiki mbili, lakini sasa miezi minne imeisha
Yani ili kupata kitu kwenye Box mpaka siku ya kazi tu. Naona bosi wa shirka la posta inabidi ashughulikie hili jipu
 
Ulikwenda kufungua box maeneo gani? Pale magomeni ni wasumbufu lakini posta niliipata Kwa wiki moja tuu
 
Wamelala hawa. Hata Iringa ilikuwa hivi hivi.
 
Kupata sanduku la Posta ni rahisi sana. Ukiwa Posta mpya nenda chumba namba 7. Vaa miwani myeusi. Waambie wahudumu una biashara ndogo. Utalipa shs 35400/+17000/+2000 /. =54400/nenda na picha kabisa stamp size. Ukiona unazinguliwa jifanye unaulizia 'Hivi boss wenu yupo?' Jamaa ni waoga sana. Utapata faster.
 
Naomba kujua gharama za kufungua sanduku la barua Posta no shilingi ngapi na kwa hapa Dar masanduku yanapatikana?
 
Hii kufungua box Kwa miaka hii tena ilitakiwa iwe online kuondosha usumbufu, kwakua Kama inakua box iko tayari unapokea email tuu.
 
Aisee magomeni nimejaribu nimeshindwa vipi maeneo mengine?

Jaribu Posta mkuu Kama uko Dar, Ukifika kuna kadirisha Kwa nyuma kuna dada ongea nae vizuri kupunguza usumbufu Mjini Watu hawategemei mishahara
 
Nipime nikuelekeze weka 70 iwe tayar
 
Mwenye makadirio ya gharama za kufungua sanduku la posta hapa Dar es Salaam, naomba anipe mwangaza kidogo.

Natanguliza shukrani.
 
nenda posta utapata taratibu zote

Nilitaka mwongozo ili nikija kwenda nijue iwapo mtu ameweka cha juu au vipi. Nilikuwa najua mwisho wa siku inabidi kwenda posta kwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…