Gharama na taratibu za kufungua sanduku la posta

Gharama na taratibu za kufungua sanduku la posta

Mkuu hiyo sahau zaidi ya miezi miwili,hao jamaa ni wasumbufu sana mwanzo wanasema baada ya wiki mbili baada ya hapo utasikia fundi ni mmoja hvy anafunguo nyingi na maneno mengi ya kuudhi tu na usiombe ukapelekwa kule Sokoine Drive kuna jamaa mmoja bonge hivi bingwa wa kuahidi.

Yani, Nimesubiri mpaka nimechoka, mwanzoni waliniambia wiki mbili, lakini sasa miezi minne imeisha
Yani ili kupata kitu kwenye Box mpaka siku ya kazi tu. Naona bosi wa shirka la posta inabidi ashughulikie hili jipu
 
Ulikwenda kufungua box maeneo gani? Pale magomeni ni wasumbufu lakini posta niliipata Kwa wiki moja tuu
 
Asante sana aise sintolichezea tena walah, huweziamini kila mwaka huwa nalilipia mwezi wa kwanza ila naweza extend mpaka mwezi wa pili nikalikuta lipo tu, du asante sana maana sikuwa najua kama ni kitu adimu, next year ntalipia tarehe mbili mwezi wa kwanza kabisa du ebwana ee
Kupata sanduku la Posta ni rahisi sana. Ukiwa Posta mpya nenda chumba namba 7. Vaa miwani myeusi. Waambie wahudumu una biashara ndogo. Utalipa shs 35400/+17000/+2000 /. =54400/nenda na picha kabisa stamp size. Ukiona unazinguliwa jifanye unaulizia 'Hivi boss wenu yupo?' Jamaa ni waoga sana. Utapata faster.
 
Naomba kujua gharama za kufungua sanduku la barua Posta no shilingi ngapi na kwa hapa Dar masanduku yanapatikana?
 
Hii kufungua box Kwa miaka hii tena ilitakiwa iwe online kuondosha usumbufu, kwakua Kama inakua box iko tayari unapokea email tuu.
 
Aisee magomeni nimejaribu nimeshindwa vipi maeneo mengine?

Jaribu Posta mkuu Kama uko Dar, Ukifika kuna kadirisha Kwa nyuma kuna dada ongea nae vizuri kupunguza usumbufu Mjini Watu hawategemei mishahara
 
Mwenye makadirio ya gharama za kufungua sanduku la posta hapa Dar es Salaam, naomba anipe mwangaza kidogo.

Natanguliza shukrani.
 
nenda posta utapata taratibu zote

Nilitaka mwongozo ili nikija kwenda nijue iwapo mtu ameweka cha juu au vipi. Nilikuwa najua mwisho wa siku inabidi kwenda posta kwenyewe.
 
Back
Top Bottom