Hata uwe makini. Kuna siku mchana pale Tazara trafik light nimesimama na pikipiki ikaja daladala nyuma haina breck, kelele za watu ndio zikaniokoa nikaluka nikaacha honda ikanyagwe. Sasa kama ingekuwa usiku? Hapa nilikuwa makini mimi ila umakini wa vyombo vingine ni tatizo..
Kilichotokea daladala ile inayotoka Gongo lamboto ikapanda pikipiki na kugonga gari ingine kwa nyuma. Dereva wa ile daladala kitendo cha kuipanda pikipiki akajua kamkanyaga na mtu, akachanganyikiwa kafungua mlango wake kashuka nje anakimbia. Sasa pale Tazara kama unaingia Buguruni kuna ubize flan. Watu wakaanza kumgombania kama mwizi. Kwa kuwa sikuumia popote nikasema nikamuokoe. Nikaanza kwenda muelekeo ule, nikiwa nakaribia machale yakanicheza nikageuka nyuma kuangalia pikipiki yangu. Daa... kuna masela nikawaona wanaanza kuitamani japo imekanyagwa. Mmoja kashika site mirror akaanza kufungua. Ikabidi nigeuze niende kulinda masalia ya chombo changu. Baada ya hali kutulia dereva anasema twwnde trafik mjini vikapimwe malipo bosi wake anadai bima ndio italipa. Zoezi jingine jipya likaanza.
Kwa ujumla pikipiki sio chombo cha kuingia nacho main load. Ni usafiri unaotakiwa uwe mbadala wa baiskeli huko mashambani na vichochoroni.