Gharama ya maisha Marekani sio mchezo, hebu ona bei ya hizi bidhaa

Ndio hapo mimi huwa nashindwa kuelewa ni wapi wenye uchumi mzuri kati yetu na wao..ikiwa kwa hapa Bongo bidhaa zote hizo sio zaidi ya elfu 50 -80.
 
Huyu ni modo wa kimataifa. Tena tajiri kweli kweli. Si ajabu kaenda kwenye maduka ya bei mbaya kwa ajili ya watu mashuhuri. Na pia naona vitu ni organic. Bei ya vitu hivi kwa kawaida huwa ghali sana. Kwa hali yake wala haishangazi na nadhani hata hiyo post yake ni kama kukejeli tu.

Watu wa kawaida tunaenda Costco huko na Sam's Club. Kwa hiyo pesa napata vitu vya kula mwezi mzima kama niko peke yangu!
 
Kwa nchi zilizoendelea ni kawaida tu. Kama ameweza kununua mahitaji yote hayo basi pesa ipo.
Uliza kiingilio cha mpira uingereza ni shilingi ngapi kwa mechi kama Real madrid vs Liverpool. Ukumbuke kuna watu walikosa tiketi yaani ziliisha. Huku bongo hata uweke kiingilio buku haujazi uwanja labda km inacheza simba na yanga.
Aiseeeeeee laki 2 kwa vutu hivyo! mbona sio mchezo ,hapo hamna hata nyama!!!!duh kasheshe!
 
She just being pompous
 
Ndio hapo mimi huwa nashindwa kuelewa ni wapi wenye uchumi mzuri kati yetu na wao..ikiwa kwa hapa Bongo bidhaa zote hizo sio zaidi ya elfu 50 -80.
Ukifananisha na ukukwetu utateseka kuna mzungu aliniambia Norway vitu bei chini sana mkate Euro 3 mimi nikamshangaa ukiigeuza hiyo Euro 3 kwa shilingi ni zaidi ya elfu 6 nikabaki kuduwaa maana Bongo mkate ni nusu dollar
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…